JE, UNAJUA NI NINI KINASABABISHA MWANAMKE KUTOKWA NA UTELEZI WENYE DAMUDAMU BAADA YA HEDHI?

 

Unapoona hali ya kutokwa na utelezi wenye damudamu baada ya kipindi cha hedhi, basi tambua kuwa ni uchafu uliobakia ambao haukuondolewa wakati ulipokuwa hedhini.

 

Je, Hali Hii Inapojitokeza Inaweza Kukutia Wasiwasi?

 

La hasha! Hali hii isikufanye kuwa na mashaka sana kwani huwa inakoma ndani ya siku chache tu ingawa unaweza wakati mwingine kupatwa na dalili za vichomi baada ya hedhi.

Lakini pia kuna vitu vingine vinavyosababisha kutokwa na damu baada ya hedhi, navyo viko kama ifuatavyo:

 

  1. Uvimbe aina ya fibroid

 

  1. Kuvimba kwa ukuta wa mfuko wa kizazi

 

 

  1. Saratani ya shingo ya kizazi

 

  1. Vivimbe kwenye vifuko vya mayai(Poly-cystic ovaries)

 

 

  1. Maambukizi sehemu za uke

 

 

Je, Ni Kinachosababisha Mwanake Atokwe Na Uteute Wenye Damu Kabla Ya Kipindi Chake Cha Hedhi kufika?

 

Hali ya kutokwa na uteute wenye damu katikati ya kipindi cha hedhi huwa ni kwasababu ya upevushaji. Ikiwa kama uteute wenye damudamu utatoka wiki 2 kabla ya kipindi chako cha hedhi hakichawadia, basi itakuwa ni hali ya upevushaji mayai imeanza.

 

Je, Nini Kinasababisha Kutokwa Na Utelezi Wenye Damu Kabla Ya Kipindi Cha Hedhi Hakijawadia?

 

Kutokwa na utelezi wenye damu kabla ya kipindi cha hedhi kuwadia yaweza kuwa ni kwasababu uko na ujauzito. Hali ya kupachikwa kwa yai kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi husababisha baadhi ya wanawake kutokwa na damu kidogo kabla ya muda wao wa hedhi haujawadia.

 

Je, Vyanzo Vingine Vinavyomfanya Mwanamke Kutokwa Na Damu Kabla Ya Hedhi Ni Nini?

Kwa kawaida vyanzo hivi huwa kama ifuatavyo:

 

 

  1. Maambukizi ukeni

 

  1. Matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango

 

 

  1. Kuvunja ungo mapema

 

  1. Msongo wa mawazo au ulaji mbaya

 

 

  1. Uzito mkubwa wa mwili kupita kiasi

 

  1. Saratani ya ukuta wa tumbo la uzazi

 

 

Je, Nini Kinamfanya Mwanamke Kutokwa Na Uteute Wenye Damu Wakati Wa Hedhi?

 

Inaonekana kuwa hali ya kutokwa na uteute wenye damu wakati wa ujauzito inaweza kusababishwa na uvimbe kwenye shingo ya kizazi au kuporomoka kwa mimba.

Je, una ujauzito lakini unatokwa na uteute wenye damu ukeni? Je, unahisi maumivu ya tumbo la chini? Basi, uonapo dalili kama hizo, yafaa umuone daktari hospitali  haraka bila kuchelewa.

 

Je, Nini Kinasababisha Mwanamke Kutokwa Na Uchafu Wenye Michirizi Ya Damu Kabla Ya Hedhi Yake Kufika?

 

 

Hali ya kutokwa na ute wenye michirizi ya damu yaweza kusababishwa na upevushaji wa mayi, kufanya tendo la ndoa au ujauzito.

Wakati wa upevushaji unaweza pia kutokwa na utelezi mweupe wenye michirizi ya damu ambayo hutokana na kupasuka kwa vifuko vya mayai.

 

Je, umewahi kuona uchafu mweupe wenye matone ya damu mara umalizapo kufanya tendo la ndoa? Uonapo hali kama hiyo, tambua kuwa mpenzi wako hakuweza kufanya tendo la ndoa vizuri na hivyo kusababishia hali ya michubuko  ukeni au kwenye shingo ya kizazi.

 

MATIBABU

James Herbal Clinic tunatoa huduma ya tiba na ushauri pi kwa wenye matatizo ya kutokwa uchafu kutokana na maambukizi, matatizo ya shingo ya kizazi, nk.

 

Unahitaji tiba, tupigie kwa namba: 0752389252 au 0712181626

 

Karibuni sana!

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *