JE, UNAKIJUA CHANZO NA DALILI ZA KUVIMBA KWA MLANGO WA KIZAZI? JE, NINI MADHARA YAKE?

 

Na ieleweke kuwa mlango wa kizazi ni sehemu ya chini ya mfuko wa kizazi(uterus). Na huu ndio mlango ambapo damu ya hedhi hupitia kutoka kwenye mfuko wa kizazi(uterus). Wakati wa kujifungua mtoto, mlango wa kizazi hutanuka ili kuruhusu mtoto apite.

Lakini kama ilivyo tishu yoyote ndani ya mwili, hivyo, mlango wa kizazi unaweza kuvimba kutokana na sababu mbalimbali. Hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi kitaalam huitwa, “Cervicitis”.

Miongoni mwa dalili ambazo wanawake wengi huzipata ni kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi na mabadiriko ya kutokwa na uchafu ukeni.

 

 

Je, Nini Husababisha Kuvimba Kwa Mlango Wa Kizazi?

 

 

 

Chanzo kikubwa cha kuvimba kwa mlango wa kizazi ni maambukizi. Maambukizi yanayosababisha mlango kuvimba yanaweza kuenezwa kutokana na mambo ya ngono, lakini pia zipo sababu zingine. Hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi inaweza kuwa ya kaida au ikawa sugu. Uvimbe sugu wa mlango wa kizazi unaweza kuendelea kwa muda wa miezi kadhaa.

 

NUKUU: Hali ya uvimbe mbaya wa mlango wa kizazi husababishwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile:

 

  • Pangusa(Chlamydia)
  • Malengelenge(trichomoniasis)
  • Kisonono(gonorrhea)

 

Lakini pia hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi unaweza kusababishwa na maambukizi mbalimbali kama vile:

 

  • Mizio au aleji kutokana na kupasuka kwa kondom na hivyo kushindwa kutoka nje ya uke
  • Matumizi ya sababuni au vipodozi vyenye marashi makali ukeni
  • Bakteria wa kawaida ukeni kama vile fangasi
  • Kemikali zinazokuwa kwenye ped

 

 

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

 

 

Mara nyingi kuvimba kwa mlango wa kizazi kunaweza kusionyeshe dalili, na unaweza  kujifunza kuwa una hali ya uvimbe huu baada tu ya kujaribu kuweka ped. Ikiwa kama kuna dalili zozote, basi zinaweza kuwa kama hizi zifuatavyo:

 

  • Kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu kuliko kawaida

 

  • Kutokwa na uchafu mwingi ukeni wenye rangi ya njano au ukijani pamoja na usaha ukiambatana na harufu mbaya.

 

 

  • Maumivu makali ukeni

 

  • Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

 

  • Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa ambayo sio ya hedhi.

 

  • Maumivu ya mgongo

 

 

 

NUKUU: Mlango wa kizazi unaweza kuvimba ikiwa kama hali ya uvimbe itaendelea. Uchafu utokao ukeni ukeni wenye muonekano kama usaha ndio dalili za uvimbe mkubwa wa mlango wa kizazi.

 

 

 

 

Je, Nini Madhara Ya Kuvimba Kwa Mlango Wa Kizazi?

 

 

 

Hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi iliyosababishwa na kisonono, au pangusa(Chlamydia) inaweza ikaendelea kuharibu kuanzia ukuta wa mfuko wa kizazi mpaka kwenye mirija ya uzazi, na kusababisha ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi yaani PID(Pelvic Inflammatory Disease). Tatizo la maambukizi katika via vya uzazi au PID husababisha maumivu ya nyonga, kutokwa na uchafu, pia kupatwa na homa. Kumbuka tatizo la PID lisipotibiwa husababisha mwanamke kuwa mgumba.

 

Je, unahitaji huduma? James Herbal Clinic tunapatikana Arusha, tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

Karibuni sana!