Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Mwili wa binadamu hutawaliwa na mifumo ya neva au kwa kitaalamu Nervous System, ambapo katika mifumo hii kuna mfumo mkuu, central nervous system (ubongo na uti wa mgongo) na pia kuna mfumo wa pembezoni ambao ni kazi za mwili mbali na ubongo na uti wa mgongo (peripheral nervous system), mfumo huu wa pembezoni hujumuisha kazi za misuli, mapigo ya moyo, mmeng’enyo wa chakula tumboni, uwezo wa kuhisi baridi au joto, kugusa vitu na kujua ukali wa ncha ya kitu na kadhalika.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu huwa kama ifuatavyo:
- Mtu kuhisi ganzi
- Maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni au mikononi,
- Kuhisi kama umevaa soksi au gloves wakati hujavaa,
- Kuhisi kama kuna kitu cha ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole,
- Kushindwa kushika au kunyanyua kitu,
- Kuchoka kwa misuli na kadhalika.
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
- Kupungua kwa virutubishi mwilini, hasa mkusanyiko wa vitamini B(Vitamini B complex).
- Matumizi ya dawa mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya Ukimwi
- Uzito mkubwa wa mwili
- Ugonjwa wa kisukari
- Shinikizo la juu la damu
Ushauri
James Herbal Clinic tunapenda kukushauri kuwa uonapo dalili kama hizo, ni vyema ukafika katika hospitali za Wilaya au Mkoa ili kupata uchunguzi kupitia vipimo mbalimbali vya magonjwa ya moyo, kisukari, nk. Yafaa pia ukapata ushauri wa madaktari ili kutatua tatizo hilo.
MATIBABU
James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo ya kufa ganzi miguu au kuhisi baridi, nazo ni NEOTONIC, PHYTOGUARD na CARD HERB.
Je, unahitaji huduma? Naomba utupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!