Ikiwa kama kila ukifanya tendo la ndoa halafu mwanamke ukatokwa na manii dakika chache mara baada ya kumaliza tendo la ndoa hata kama haujainuka kusimama, tambua kuwa hiyo ni dalili mojawapo ya kwamba mbegu za mumeo au mwenzi wako sio bora. Ndugu msomaji naomba usome makala hii kwa makini kabisa mpaka uimalize halafu utambue suluhisho la tatizo hili.
Je, Ubora Wa Mbegu Za Mwanaume(Sperm Analysis) Unakuwaje?
Kwa kawaida kazi ya uchunguzi wa ubora wa mbegu za mwanaume hufanyika hospitalini ambapo mbegu zako huchukuliwa na kuchunguzwa na daktari mwenye uzoefu. Lakini inafahamika wazi kuwa unaweza kufanya tendo la ndoa kila siku za hatari na bado usimtungishe mimba mkeo ama mpenzi wako. Tatizo linaweza kuwa kwa baba au mama au wote wawili. Kwa upande wa mwanaume unaweza kujitambua kuwa huna mbegu bora kutokana na muonekano wa manii zako pamoja na kiasi cha shahawa kinachotoka katika kila tendo la ndoa moja.
Je, Unaweza Kuzitambuaje Mbegu Zako?
- Wingi Wa Mbegu Za Mwanaume
Mbegu za mwanaume kila tendo moja kamilifu linalofanywa zinatakiwa zisipungue milioni 40. Kiasi hiki sio rahisi kukitambua tu kwa macho. Lakini kila unapotoa uteute kidogo wa mbegu, basi kuna uwezekano wa kuwa na mbegu chache tu. Mshindo dhaifu au kufika kileleni haraka sana(kirahisi rahisi) ni moja wapo ya dalili kwamba mbegu unazotoa sio nyingi, zinaweza kuwa na maji maji mengi badala ya kuwa na mbegu nyingi.
- Uzito Wa Mbegu Za Mwanaume Na Kuchelewa Kuyeyuka
Kwa kawaida majimaji ya mbegu huwa na mbegu, na uteute huo huwa ni majimaji yanayobeba mbegu za mwanaume. Kazi ya uteute ni kusafirisha mbegu za mwanaume katika hali ya usalama mpaka kulifikia yai la mwanamke.
NUKUU: Ikiwa shahawa zitakuwa nyepesi sana, basi unaweza ukaona zinatengana na mbegu haraka mno mara tu zinapotoka nje, na hivyo kuathiri uwezo wa mbegu kusafiri haraka na kulifikia yai.
- Uwezo Wa Mbegu Kuogelea Na Kwenda Mbele
Kwa kawaida mbegu za mwanaume zenye afya bora zina kichwa kikubwa kilichochongoka na mkia mrefu unaoanza mkubwa kichwani na kuishilia mdogo mkiani. Sifa hizi zinazipatia mbegu uwezo wa kuogelea kwenda mbele katika mstari ulionyooka. Lakini ikiwa kama mbegu za mwanaume zitasafiri katika mstari wa kupindapinda au maumbomaumbo, basi ndipo hupoteza uwezo wa kufika haraka ili kuliwahi yai. Hii ni kwasababu zinachoka haraka. Mbegu zinazoenda katika mstari mnyoofu zinawahi kufika kwakuwa safari inakuwa ni fupi tu.
- Uwezo Wa Kuishi Kwa Mbegu Za Mwanaume
Mbegu bora inafaa iishi sio chini ya masaa 72 kuanzia muda ule inapotoka kwa mwanaume na kuingia kwa mwanamke, maisha mafupi ya mbegu yanaifanya mbegu kuwa na wakati mgumu wa kuliwahi yai ili kulirutubisha.
- Je, Rangi Bora Ya Mbegu Za Mwanaume Inakuwaje?
Kwa kawaida uteute wenye mbegu zilizo bora huwa una rangi nyeupe inayoelekea kuwa ya kijivu, na kwa wazee inakuwa nyeupe na kuelekea kuwa ya njano. Kwahiyo huwezi kuona rangi hii mara kwa mara kwasababu mbalimbali za kiafya, hasa kutokana na ulaji wa chakula na hali ya hewa. Lakini kwa watu wazima kuanzia miaka 40 kwenda juu, ni kawaida sana kuonekana wenye rangi nyeupe au njano.
Je, Nini Chakufanya Ili Uweze Kuona Dalili Hizi?
Unapoona dalili hizi au unapopimwa na kukutwa na dalili kama hizo, ikiwa kama ndoa yako upatikanaji wa mimba unakuwa mgumu, na ikiwa kama mama mara kwa mara hujikuta mbegu za mwanaume zinamtoka na kuchuruzika muda mchache tu mara baada ya tendo la ndoa, basi tambua kuwa ubora wa mbegu zako ni mdogo na hivyo unahitaji utatuzi wake ili kuondoa tatizo. Hivyo basi, unashauriwa kutumia tiba huku ukijitahidi kula vyakula vyenye wingi wa madini ya Zinki na Chuma.
Tahadhari
Unashauriwa usitumie pombe, sigara, madawa ya kulevya, kupiga punyeto, ulevi wa kupindukia, nk.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!