Atukuzwe Mungu wetu wa Mbinguni! Karibuni katika kipindi chetu cha semina ya afya juu ya magonjwa ya uvimbe tumboni. Kwanini matatizo haya yanatokea kwa kasi na jinsi gani unaweza kuyatibu na kujikinga nayo.
Leo nitazungumzia juu ya uvimbe katika mfuko wa uzazi(Fibroid).
NUKUU: Uvimbe katika mfuko wa uzazi wa mwanamke hujulikana kama uterine myoma(yuteraini mayoma) au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi. Tatizo hili huwakumba wanawake wengi ambapo huwapata kwa asilimia tano wanawake wenye umri kati ya miaka 20 hadi 30, asilimia karibu 20 kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 40, na zaidi ya asilimia 40 kwa wale wenye umri zaidi ya miaka 40. Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa fibroids ni aina ya uvimbe unaowapata wanawake wengi hasa katika umri wa miaka ya uzazi. Hii inamaanisha kuwa kadiri umri unavyokuwa mkubwa mwanamke ana nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huu, pia ni tatizo ambalo linashuhudiwa sana katika jamii kwa sasa na pengine ni kutokana na jinsi watu wanavyoishi.
Kuna aina kuu 3 za fibroids, nazo ni kama ifuatavyo:
- Intramural Fibroids: Huu ni uvimbe unaotokea ndani ya nyama ya kizazi
- Subserol Fibroids: Huu ni uvimbe unaotokea nje kwenye ukuta wa kizazi.
- Submucosal Fibroids: Huu ni uvimbe unaotokea kwenye tumbo la uzazi na unaweza kuwa ndani ya kizazi.
NUKUU: Uvimbe katika mfuko wa uzazi huwapata zaidi kina mama ambao wako katika umri wa kuweza kuzaa (reproductive age). Uvimbe huu huwa wa ukubwa tofauti kwani huanza kidogo na baadaye kuwa mkubwa sana na hata baadhi ya wakati mwanamke kuonekana kama ni mjamzito.
Uvimbe huu unaweza kuwa mmoja lakini baadhi ya wakati hutokea uvimbe zaidi ya mmoja ambao hutanda katika mfuko wa uzazi. Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa tatizo hili hivi sasa limekuwa likiwapata zaidi wanawake ambao hawajazaa kabisa au wamekaa muda mrefu bila kuzaa, ama wanawake wanene. Naomba wapendwa mnaosoma makala hii hebu jaribu kuyashika na kuyazingatia hayo ninayoyaeleza hapo juu.
Napenda kuwashauri kina mama wenye miili mikubwa au wanene ni vyema ukapata vipimo mapema kwenye kizazi ili kuzuia na kujiepusha na janga hili la fibroids. Uvimbe huu umekuwa ukiwashambulia Sana wanawake wengi wenye miili mikubwa Kama unavyoona kwenye picha hapo juu.
NUKUU: Wengine walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu wa fibroids ni pamoja na wale wanaopata hedhi mapema. Inafaa kuelewa kuwa, fibroids sio kansa bali ni uvimbe wa kawaida tu ambao hukuwa kwa kutegemea kichocheo au hormone ya estrogen na ndio maana wakati wa kupata uvimbe huo ni kuanzia kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi. Hata hivyo ingawa fibroids si saratani, lakini uvimbe wa aina hii umekuwa tishio kwa wanawake wengi duniani na kusababisha wengi wao kuondolewa vizazi. Pamoja na kuwa sababu kuu ya uvimbe katika kizazi haijajulikana, lakini zipo sababu ambazo zimehakikiwa kusababisha mwanamke kupata uvimbe wa fibroid. Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya estrogen ambavyo vipo katika miili ya wanawake na vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake.
Mara nyingi uvimbe huu huwa unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu ili kulinda makuzi ya mtoto. Unapaswa kujua kuwa, kwa watu waliofikia kikomo cha hedhi au menopause huwa hawapati fibroids na kama wakipata basi huwa na hatari ya kuwa kansa. Hili naomba mwanamke mahali popote ulipo napenda ulitambue.
Je, Dalili Za Uvimbe Katika Kizazi Zinakuwaje?
Uvimbe katika kizazi cha mwanamke ukiwa mdogo unaweza usiwe na dalili zozote na dalili hutegemea sehemu ulipo kwenye mfuko wa uzazi na pia ukubwa wake. Hata hivyo dalili za ugonjwa huu mara nyingi huwa kama ifuatavyo:
- Kupata maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi,
- Maumivu makali ya tumbo
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa,
- Kutotunga mimba au mimba kuharibika na kutoka,
- Ugumba
- Maumivu ya mgomgo na kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe hukandamiza kibofu cha mkojo.
- Kutokwa damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida, au kutokwa damu isiyo ya kawaida katikati ya mwezi au hedhi zisizokuwa na mpango.
NUKUU: Tatizo la uvimbe katika kizazi mara nyingi huambatana na maradhi mengine. Maradhi hayo ni kama, upungufu wa damu, kufunga choo, matatizo ya figo na mara chache huweza kuwa saratani. Pia uvimbe wa fibroid unapokuwa mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo kama vile; mkojo kubaki kwenye kibofu, haja kubwa kuwa ngumu, miguu kuvimba na kupungukiwa damu.
Je, Vipimo Vinafanyikaje?
Ni rahisi kwa mtaalamu kugundua ugonjwa huu au uvimbe katika mfuko wa uzazi kwa kumkagua, au kumpima mgojwa (bimanual examination). Daktari anaweza kuhisi uvimbe kwa kutumia mikono miwili anapokuwa ana pima tumbo, hata hivyo kipimo cha Ultrasound ya nyonga hutumika kugundua uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke. Kipimo cha MRI pia huweza kutumika kupata usahihi wa ukubwa na eneo uvimbe ulipo.
NUKUU: Fibroids zinaweza kuzuia kupata mtoto kwa njia tofauti. Kwanza kabisa uvimbe huu unapokuwa sana hukandamiza mirija ya kupitisha mayai kutoka kwenye ovari au sehemu mayai yanapotengenezwa. Uvimbe huu pia unaweza kuzuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi hasa ikiwa ni submucosal fibroids. Pia hufanya mfuko wa kizazi ukaze na hivyo kushindwa kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.
TIBA ZAKE
James & Ferdinand Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya uvimbe katika mfumo wa uzazi wa mwanamke, nazo ni REDEEMER, FRESH HERB na VITAMAKA.
Je, unahitaji huduma? Kwa mawasiliano tupigie namba: 0752389252 au 0712181626
Arusha Mbauda
Karibuni sana.