Korodani huwa ni viungo vya uzazi vya mwanaume, nazo huwa zina kazi mbili muhimu sana kwa ajili ya mfumo wa uzazi wa mwanaume; kwani huzarisha mbegu za uzazi(shahawa) na hutengeneza vichocheo au homoni.
Je, Korodani Zina Muonekano Gani?
Korodani huwa ni zenye umbo la mviringo, nazo hukaa kwenye pumbu, nyuma ya uume. Kila korodani huwa ina uzito wa gram 10-15. Nazo zina urefu wa sentimita 5, na upana wa sentimita 3.
NUKUU: Pumbu huwa ni ngozi tepetepe kama kifuko fulani hivi, ambacho hutunza korodani na hufanya kazi ya kurekebisha mfumo wa joto kwenye korodani. Korodani sharti ziwe kwenye joto la chini kidogo kuliko la mwili kwa ajili ya kutengeneza kiwango cha kawaida cha mbegu za mwanaume. Misuli katika ukuta wa pumbu hurusu kukaza na kuregea, kuzipeleka korodani karibu na mwili kwa ajili ya kutia joto au kuzishusha chini ili zipoe, utaona pumbu inashuka chini.
Kila korodani huwa ina mirija mingi midogomidogo ambazo zina seli za kuzarisha mbegu pamoja na homoni.
Je, Kazi Za Korodani Ni Nini?
Mbali na kuzarisha mbegu za mwanaume, lakini pia korodani huzarisha homoni zinazoitwa, “androgens”. Homoni hizi huongoza jinsi ya kukua kwa mfumo wa uzazi wa mwanaume, pamoja na kutengeneza sura ya mwanaume kama vile kidevu na sauti nzito ya mwanaume.
Lakini pia husaidia katika kutia hisia au nyege kwa mwanaume.
Homoni za angrogen hushughulika sana na uzarishaji wa mbegu za mwanaume. Korodani zikiwa na afya njema zina uwezo wa kuzarisha homoni zenye ujazo wa milligram 6 kila siku.
NUKUU: Lakini kumbuka kuwa korodani pia zina uwezo wa kutengeneza kiwango cha mbegu 200,000 kwa dakika 1. Hata hivyo, kadiri mwanaume anavyozidi kufikia umri mkubwa kuanzia miaka 30, kiwango cha homoni za androgens zinazozarishwa na korodani hanza kushuka na huendelea kupungua.
Je, Magonjwa Gani Yanayopatikana Kwenye Korodani?
Kwa kawaida kila mwanaume huzariwa akiwa na korodani mbili. Nazo huanza kuumbika pale anapokuwa tumboni mwa mama yake, na hushuka kwenye pumbu baada ya miezi 7 ya ujauzito.
Wakati mwingine, ingawa korodani hushindwa kushuka, na hivyo mtoto huzariwa na hali ya matatizo ya korodani. Hali hii hujitokeza kwa asilimia 2 ya wanaume, na katika asilimia 10 za matatizo hayo, korodani zote mbili huwa haziko katika hali yake inayo takiwa, yaweza kuwa moja kubwa na nyingine ndogo sana.
NUKUU: Korodani zinaposhuka mtoto akiwa tumboni wakati mama akiwa mjamzito, kwa kawaida huwa hazikai maeneo zinapotakiwa kuwa. Hivyo basi, korodani hizo huingia maeneo ya nyonga. Na inapokamilika miezi 9 ya mama kujifungua, mtoto atazaliwa huku korodani zikiwa maeneo hayo.
Kwa kawaida itatakiwa utaalamu ufanyike, na hivyo daktari hufanya majukumu yake ili kuzirudisha korodani katika maeneo yake sahihi ambayo ni pumbu.
Je, Korodani Zinapokuwa Hazina Afya Inakuwaje?
Korodani zisizokuwa na afya zinaweza kusababisha uzarishaji duni wa mbegu na homoni za mwanaume. Kuwa na uzito bora wa mwili kutachangia kuwa na korodani nzuri zenye afya kwa mwanaume. Hali ya ugumba huongezeka asilimia 10 kwa mwanaume anapokuwa na uzito mkubwa.
NUKUU: Napenda nikushauri kuwa jihadhari sana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, msongo wa mawazo, uvutaji sigara, ulevi wa pombe, na ulaji wa vyakula duni. Kumbuka kuwa unapotunza korodani zako katika joto la kawaida kunaweza kusaidia kuongeza uwezo wa uzarishaji wa kiwango cha mbegu katika ubora wake.
Njia rahisi ya kuziweka korodani katika joto la kawaida ni kuvaa nguo za ndani zisizobana, na kutumia vinywaji vya moto au vuguvugu unapokuwa katika mazingira yenye ubaridi.
Je, unahitaji huduma? Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626
Arusha Mbauda
Karibuni sana.
Natumai muazima wa Afya..
Suali: Je, Korodani moja kuwa kubwa na moja kuwa ndogo lakini haina maumivu yoyote.. Je! Hili ni tatizo??
Nashkuru nimefaidika sana na mungu awabariki kwa kazi yenu mzuri
Amina
Mwanangu korodan moja ipo kwenye nyonga na anaumri wa miaka 7 tatizo ni nini
Inakuwaje mwanaume ambaye hana pumbu kabsa
Je, mwanaume alieondolewa korodani Moja anaweza kumpa mwanamke mimba ?
Ni vigumu na huwa haiwezekani