Maambukizi ya bakteria pamoja na uvimbe huwa visababishi vya kawaida vya hali ya kushisi kuwaka moto au maumivu wakati unapokojoa.
Hali ya kuhisi moto au maumivu wakati unapokojoa inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali yanayopelekea kuwapo kwa hali ya kawaida au mbaya kabisa katika afya ya mwili wako.
NUKUU: Maumivu au hali ya kuhisi moto mara nyingi unaweza kuihisi maeneo ya njia ya mkojo, mrija ambao hubeba mkojo na kuutoa nje ya kibofu cha mkojo, au maeneo ya tupu ya mwanamke au mwanaume.
Chanzo kikuu cha kuhisi moto wakati wa kukojoa huwa ni maambukizi katika njia ya mkojo yaani UTI(Urinary Tract Infection).
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Zipo dalili mbalimbali tofauti zinazomfanya muhusika kuhisi hali ya kuwaka moto(Dysuria). Kukojoa kwa kuhisi maumivu kunaweza kukufanya kuhisi hali ya kuwaka moto, kuwashwa, au kuchomwa chomwa, na inaweza kutokea pindi unapoanza kukojoa, wakati unapokojoa, au baada ya kumaliza kukojoa.
NUKUU: Watu wanaohisi maumivu mwanzoni wanapoanza kukojoa mara nyingi huwa wana maambukizi ya UTI. Masumbufu baada ya kumaliza kukojoa yanaweza kuwa ni ishara kwenye kibofu cha mkojo au tezi dume.
Unapaswa ufike hospitali haraka kwa ajili ya vipimo ikiwa kama utahisi dalili kama zifuatazo:
- Kutokwa na uchafu kwenye uume au uke
- Mkojo mchafu au wenye harufu mbaya
- Kukojoa mara kwa mara
- Mawe kwenye figo
- Damu kwenye mkojo
- Kuhisi kichefuchefu au kutapika
- Muwasho maeneo ya uke au uume
- Maumivu ya mgongo au pembeni mwa nyonga
NUKUU: Yafaa pia kuwasiliana na daktari wako ikiwa kama unahisi hali ya kuwaka moto wakati unapokojoa pindi unapokuwa na ujauzito, au endapo kama maumivu wakati wa kukojoa yatakaa muda mrefu sana zaidi ya masaa 24.
Visababishi Vya Kawaida Vya Maumivu Wakati Unapokojoa Ikiwa Pamoja Na Maamukizi Pamoja Na Uvimbe
Kisababishi cha kawaida cha maumivu wakati wa kukojoa huwa ni maambukizi ya chini katika njia ya mkojo(Low Urinary Tract Infection au UTI). Maambukizi hutokea wakati bakteria wanapoingia katika njia ya mkojo na kusafiri mpaka kwenye kibofu cha mkojo.
Wanawake wenye umri wa mika 20-50 wapo kwenye hatari ya kupata maambukizi kwenye vibofu vya mkojo(cystitis), na baadaye kuwa na maumivu wakati wanapokojoa. Wanawake wajawazito, watu wenye magonjwa ya kisukari, wanawake wanaokosa hedhi kabla ya muda wao haujawadia, pamoja na watu wenye magonjwa kwenye vibofu vya mkojo pia wapo katika hatari ya maambukizi katika vibofu vyao vya mkojo na hivyo kupelekea kuhisi hali ya kuwaka moto.
Maambukizi sehemu za juu za njia ya mkojo, au maambukizi kwenye figo, pia yanaweza kusababisha hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa. Figo hupata maambukizi wakati bakteria wanaposafiri kutoka kwenye kibofu cha mkojo na kufika kwenye figo. Wanawake wajawazito, watu wenye kisukari, watu wenye matatizo ya mawe kwenye figo, na waume wenye tezi dume iliyovimba, vile vile huwa wana maambukizi katika njia ya mkojo maeneo ya juu.
Kuvimba kwa uke pia kunaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa. Hali ya kuvimba kwa uke inaweza kusababishwa matatizo ya mizio au aleji kutokana na matumizi ya vitu vyenye kemikali kali kama vile sabuni, nk, kushuka kwa viwango vya homoni ya estrogeni, maambukizi ya fangasi, au maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Kuvimba kwa njia ya mkojo kunaweza pia kusababisha maumivu wakati wa kukojoa. Visababishi kwa kawaida huwa ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na pangusa, nk.
Visababishi vya kuwaka moto au maumivu wakati wa kukojoa pia vinaweza kutofautiana kwa jinsia ya mtu. Wanawake mara nyingi huwa na hali hiyo kwa namna ifautavyo:
- Muwasho kwenye tishu ya uke
- Maambukizi ya mkanda wa jeshi maeneo ya tupu
- Matatizo ya kupungukiwa lishe.
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Kuvimba kwa tishu za uke kutokana na kupungua kwa homon ya estrogen(Atrophic vaginitis) wakati wa kukoma hedhi
NUKUU: Wanaume wanaweza kuwa na hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa endapo kama wana magonjwa ya tezi dume au salatani. Wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50 wapo katika hatari ya kupata matatizo kwenye kibofu cha mkojo kutokana na matatizo ya tezi dume.
Kwa nyongeza tu katika visababishi vya maumivu wakati wa kukojoa pande zote mbili, wanaume na wanwake yanaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Maumivu makali kabisa wakati wa kukojoa(Interstitial cystitis)
- Kuharibika kwa kibofu cha mkojo kwasababu ya tiba ya mionzi
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
Je, Jinsi Gani Unaweza Kubaini Kile Kinachosababisha Maumivu Wakati Unapokojoa?
Ili kubaini chanzo cha maumivu wakati unapokojoa, basi daktari anaweza kupima mkojo ili kuweza kuona kiwango cha chembe nyeupe za damu, chembe nyekundu za damu, protini, glukozi, pamoja na kemikali kwenye mkojo wako. Uwepo wa chembe nyeupe za damu kwenye mkojo unaweza kuonyesha maambukizi katika njia ya mkojo au UTI.
Daktari pia anaweza kufanya vipimo vya mkojo ili kubaini aina gani ya bakteria wanaosababisha maambukizi katika njia ya mkojo(UTI) na ni dawa gani nzuri utakazopaswa kuzitumia ili kutibu maambukizi.
Vipimo vingine vya nyongeza vinaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Kupima maji maji yanayotoka ukeni
- Vipimo vya nyonga
- Vipimo vya mrija wa mkojo
- Vipimo vya figo kupitia ultrasound
- Vipimo vya MRI(Magnetic resonance imaging)
- CT(computerized tomography) scan
- Vipimo vya magonjwa ya zinaa.
Tiba Zake
James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya maambukizi ya UTI, nk, nazo ni NEOTONIC, FRESH HERB na MULTICURE POWDER.
Je, unahitaji huduma? Tupigie namba hizi:
Arusha Mbauda: 0752389252 au 0712181626
Njombe-Makambako: 0744 531 152 au 0716 158 086
Karibuni sana
Amen