Maumivu wakati wa hedhi huwa maumivu ya mkazo fulani maeneo ya tumbo la chini. Wanawake wengi wanapatwa na tatizo la maumivu kabla au wakati wanapoingia hedhini.
Baadhi ya wanawake hali hii inapojitokeza kwao huwapa usumbufu mkubwa mno na inawakera. Wengine hali ya maumivu wakati wa hedhi inaweza kuwa mbaya zaidi na kuwafanya wasiweze hata kufanya kazi zao za kila siku kwa muda wa siku au miezi kadhaa.
NUKUU: Matatizo kama vile uvimbe wa fibroid tumboni yanaweza kusababisha maumivu makali wakati mwanamke anapoingia hedhini. Lakini unapotibu tatizo kama vile uvimbe, bila shaka ndio njia pekee ya kuondoa masumbufu ya maumivu unapoingia hedhini. Lakini maumivu mengine wakati wa hedhi yanayokuja bila kusababishwa na uvimbe, yanaonekana kupungua pale mwanamke anapofikia umri mkubwa na mara nyingi huondoka baada ya kuzaa mtoto.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili za maumivu wakati wa hedhi huwa kama ifuatavyo:
- Kuhisi maumivu makali maeneo ya tumbo la chini
- Maumivu ya kichwa
- Maumivu ambayo hupenya kiunoni hadi kwenye mapaja
- Maumivu ambayo huanza siku 1-3 kabla ya hedhi huchukua masaa 24 baada ya kuanza hedhi nayo hupungua ndani ya siku 2-3.
Lakini pia baadhi ya wanawake huhisi dalili kama hizi:
- Kichefuchefu
- Kuharisha
- Kichwa kugonga
- Kizunguzungu
Je, Tatizo Hili Husababishwa Na Nini?
Wakati wa hedhi, kifuko cha uzazi(uterus) hujibana na kujikaza ili kusaidia kuondoa ile ngozi laini ya juu. Vitu vyenye muonekano wa homoni(prostaglands) vinavyojihusisha kwenye maumivu na kutuna kwa msuli wa tumbo la uzazi husababisha msuli wa mfuko wa kizazi kujibana na kukaza. Viwango vikubwa vya protaglandins huambatana na maumivu makali ya hedhi.
Maumivu wakati wa hedhi yanaweza kusababishwa na mambo yafuatayo:
- Uvimbe wa fibroid tumboni
- Uvimbe kwenye mlango wa kizazi
- Maambukizi katika via vya uzazi au PID
Mambo Hatarishi:
Unaweza kuwa katika hatari ya maumivu ya hedhi endapo kama:
- Una umri mdogo chini ya miaka 30
- Ulivunja ungo mapema, hasa umri wa miaka 11
- Unatokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
- Una vipindi vya hedhi vyenye kubadiria
Je, Madhara Yake Ni Nini?
Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huwa hayasababishi madhara, bali yanaweza kuingiliana na mambo ya shule, au kazi. Mwanamke au dada yeyote anayekuwa na tatizo hili huku akisoma linaweza kumfanya asiende shule pale hali hii inapojitokeza, na kama anafanya kazi ofisini au kazi zake binafsi linaweza kumfanya asiweze kuhudhuria kazi zake.
NUKUU: Magonjwa mbalimbali yanayoambatana na maumivu ya tumbo wakati wa hedhi yanaweza kuleta madhara kwa muhusika. Kwa mfano; maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi au PID yanaweza kusababisha michubuko kwenye mirija ya uzazi, na hivyo kuongeza uhatari katika yai lililorutubishwa lishindwe kujipachika ndani ya mfuko wa uzazi(uterus), na kusababisha mimba iwe nje ya kizazi(ectopic pregnancy).
Je, unahitaji huduma ili kuondoa hali hii? Kwa mawasiliano tupigie namba zifuatazo:
Arusha Mbauda; 0752 389 252 au 0712 181 626
Karibuni sana