Katika suala zima la ugumba kwa mwanaume na mwanamke lazima kuwepo na vigezo vya uchunguzi. Kwa mwanamke mambo ya kuangalia ni historia yake katika matumizi ya madawa ya tiba alipokuwa mdogo au hata kama mama yake aliwahi kutumia aina fulani za madawa wakati wa ujauzito. Wataangalia kama ulivunja ungo kwa wakati muafaka, mfano uliwahi sana au ulichelewa sana. Muda muafaka ni kati ya miaka 12 hadi 16. Kufahamu mzunguko wako wa hedhi unavyoenda na kiwango cha damu unachopata, kama ulishawahi kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Je, ulishawahi kupata mimba? Na ulizaa au iliharibika? Je, uliwahi kutoa mimba?
NUKUU: Vile vile inahitajika kujua kama ulishawahi kufanyiwa upasuaji wowote chini ya tumbo mfano kutoa uvimbe, mimba nje ya kizazi, kuzaa mtoto kwa upasuaji. Ni muhimu pia daktari akafahamu endapo ulishawahi kupata maambukizi yoyote katika viungo vya uzazi(PID), madawa uliyokwishawahi kutumia kwa muda mrefu, ulaji wako wa vyakula, kama unakunywa pombe au unavuta sigara.
Je, Kwa Upande Wa Mwanaume Inakuwaje?
Kwa upande wa mwanaume, vigezo ni kama una kasoro katika viungo vyako vya uzazi, mfano uume ni mfupi sana(kibamia), tundu la mkojo limekaa upande, kasoro katika korodani au korodani kama zipo, zimevimba, zimesinyaa au ndogo sana, hazipo au ipo moja, zinauma au moja ndogo na nyingine kubwa.
NUKUU: Pia utahitajika kujua kama ulishawahi kusumbuliwa na maambukizi katika njia ya mkojo kwa muda mrefu, mfano kisonono au yutiai za mara kwa mara, maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa na majimaji au manii katika njia ya mkojo. Inahitajika kujua historia yako kama ulishawahi kumpa mimba mwanamke, kama una mtoto. Ufanyaji wako wa tendo la kujamiiana pia daktari itabidi ajue endapo huwezi kabisa, kumudu, unawahi kumaliza, unachoka sana baada ya tendo au unashindwa kurudia, au uume hauna nguvu za kutosha.
Ni muhimu kuelezea kama unakunywa pombe, unavuta sigara au unatumia madawa ya kulevya kama bangi, mirungi na mengineyo. Vyote hivi huathiri uzazi kwa kiasi kikubwa. Je ulishawahi kufanyiwa upasuaji hasa wa henia au ngiri ya kushuka, busha, vyote inabidi vijulikane.
NUKUU: Matumizi ya madawa ya kulevya ya hospitali kwa muda mrefu, mfano dawa kwa ajili ya vidonda vya tumbo, kifafa, moyo, kifua kikuu na mengineyo. Ulaji wako wa chakula na ufanyaji mazoezi, vile vile kuangalia unanyoa sehemu za siri na makwapani baada ya muda gani(wengine wanamaliza mwaka bila kunyoa), kwani nayo huchangia kuashiria baadhi ya dalili.
Kwa hiyo, ukiangalia kwa undani kuhusiana na suala zima la kutopata mtoto, siyo tu kwamba mtu anatumia dawa fulani na kufanikiwa. Pia suala hili halitibiwi kwa hisia na utabiri, bali ni suala la kisayansi na linahitaji uchunguzi wa kina na tiba za hospitali.
Vyanzo vya matatizo haya ni vingi na tofauti ni kubwa inayomtokea kila mwenye tatizo. Tumeona vigezo.
Je, Nini Cha Kufanya?
Tatizo hili la kutokupata mtoto au ugumba kama tulivyokwishaona hapo awali, linawahusu mke na mume, yaani watu wawili wanaotafuta mtoto kwa mwaka mzima lakini aidha mimba zinatoka au hafanikiwi kabisa. Pia tunasema tendo hilo la kujamiiana linafanyika kikamilifu.
NUKUU: Kufanya kikamilifu maana yake uume unaingia ukeni na tendo hilo linafanyika zile siku za kupata ujauzito. Lini mwanamke anapata ujauzito? Au siku za hatari za kupata ujauzito ni zipi? Kaa sawa kwa kuendelea kusoma makala hizi tutaelezea kwa undani zaidi.
Kwa hiyo, kama tulivyoelezea, hakuna sehemu ambapo utapata vipimo sahihi vya matatizo haya ya kutopata ujauzito zaidi ya kwenda katika Hospitali za mikoa ambapo utakutana na madaktari bingwa wa matatizo ya uzazi, utafanyiwa vipimo vya kisayansi wewe na mwenzio na kupata majibu sahihi kufuatana na jinsi tulivyoyachambua hayo matatizo.
Je, unahitaji huduma ya tiba? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712 181626
Arusha Mbauda