JE, UNAJUA VYANZO VYA NYONGA KUUMA? JE, NINI MADHARA YAKE?

Maumivu ya nyonga huwa ni maumivu sehemu ya tumbo la chini pamoja na nyonga zenyewe. Kwa wanawake, maumivu ya nyonga yaweza kuwa viashiria au dalili za matatizo yaliyoko kwenye mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo au mfumo wa usagaji chakula au mifupa pia.

Picha inayohusiana

NUKUU: Kulingana na chanzo chake, maumivu ya nyonga yanaweza kuwa ya kawaida tu au yakawa makali kabisa; yanaweza kuwa ya mfululizo au muda tu yanatoweka. Maumivu ya nyonga yanaweza wakati mwingine yakapenya yakaingia kiunoni, matakoni au mapajani. Wakati mwingine unaweza ukahisi maumivu ya nyonga kwa muda Fulani, kama vile wakati unapokojoa au unapofanya tendo la ndoa.

 

Maumivu ya nyonga yanaweza kujitokeza ghafla, au yakawa makali sana au yakawa sugu. Maumivu sugu ya nyonga yanaweza yakadumu kwa muda wa miezi sita au zaidi.

 

 

Je, Nini Husababisha Hali Hii?

 

 

 

Aina mbalimbali za magonjwa pamoja na maradhi zinaweza kusababisha maumivu ya nyonga. Maumivu sugu ya nyonga yanaweza kusababishwa na ugonjwa mmoja au zaidi. Kama nilivyosema awali kuwa, maumivu ya nyonga yanaweza kutokana na matatizo yanayokuwa kwenye mfumo wa usagaji chakula tumboni, mfumo wa uzazi, au mfumo wa mkojo.

 

 

Je, Mfumo Wa Uzazi Wa Mwanamke Unakuwaje?

 

 

Maumivu ya nyonga yanayotokana na mfumo wa uzazi wa mwanamke, nayo  yanaweza kusababishwa na maradhi kama yafuatayo:

 

  • Uvimbe kwenye shingo ya kizazi

 

  • Mimba nje ya kizazi(ectopic pregnancy)

 

 

  • Maumivu wakati wa hedhi

 

  • Mimba kuporomoka

 

  • Salatani ya vifuko vya mayai

 

 

  • Uvimbe kwenye vifuko vya mayai

 

  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID

 

 

  • Uvimbe kwenye mfuko wa kizazi(fibroids)

 

 

 

 

Je, Visababishi Vingine Kwa Wanawake Au Wanaume Vinakuwaje?

 

Mifano mingine ya maumivu  ya nyonga kwa wanawake au wanaume husababishwa na mambo mfano kama ifuatavyo:

 

  • Kukosa choo muda mrefu

 

  • Tatizo la dole tumbo(appendix)

 

 

  • Utumbo kukunjamana

 

  • Mawe kwenye figo

 

 

  • Maambukizi katika njia ya mkojo au UTI

 

  • Vidonda vya tumbo.

 

 

 

Tiba Zake

 

 

James & Ferdinand Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya maumivu ya nyonga ikiwa kama utapata vipimo hospitalini na kugundua vyanzo au visababishi vyake

 

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

 

Arusha-Mbauda.

 

 

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *