Uvimbe aina ya cervicitis kwa kawaida huwa ni uvimbe unaojitokeza kwenye shingo ya kizazi, mwishoni kabisa mwa eneo finyu la chini ya mfuko kizazi(uterus), ambalo huacha uwazi ndani ya uke.
NUKUU: Dalili zinazojitokeza mara kunapokuwapo na hali ya shingo ya uzazi kuvimba huwa ni kutokwa na damu kabla ya muda wa hedhi haujawadia, au maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa, kutokwa na uchafu mbaya, au wakati unapofanyiwa uchunguzi na daktari hasa anapozamisha kidole ndani ya uke. Lakini hata hivyo unaweza kupatwa na hali hii ya uvimbe pasipo kuona dalili zozote.
Dalili kuu za tatizo hili huwa ni kutokwa na damu ya hedhi mara 2 kwa mwezi, kuhisi maumivu makali, nk. Lakini kuvimba kwa shingo ya kizazi hutokana na maambukizi kama vile pangusa(Chlamydia), au kisonono(gonorrhea). Hali ya kuvimba kwa shingo ya kizazi inaweza kuwepo hata bila ya maambukizi pia. Unahitaji kuondoa tatizo la kuvimba kwa shingo ya kizazi unapaswa kutibu chanzo cha uvimbe huu.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Mara nyingi uvimbe kwenye shingo ya kizazi huwa hauonyeshi dalili, na unaweza kujifunza tu kuwa una tatizo hilo baada ya kupata vipimo kwenye nyonga kutokana na sababu nyingine. Ikiwa kama unataona dalili, huenda zinaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Uchafu mwingi usio wa kawaida utokao ukeni
- Maumivu ya mara kwa mara unapokojoa
- Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
- Kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi
- Kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa isiyo ambatana na hedhi
Je, Nini Kitakufanya Ufike Hospitali Ili Kumuona Daktari?
Fika hospitali haraka mara utakapoona mambo yafuatayo:
- Kuendelea kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni
- Kutokwa na damu isiyo ya hedhi
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
Je, Nini Husababisha Shingo Ya Kizazi Kuvimba?
Vyanzo halisi vya kuvimba kwa shingo ya kizazi huwa kama ifuatavyo:
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Kutokufanya usafi maeneo ya uke
- Kuwa na aleji ukeni kama vile sabuni zenye marashi au kemikali, nk
- Kuondoka kwa bakteria wa asili wanaokuwa kwenye uke.
Je, Kunakuwa Na Madhara Au Matatizo Gani?
Kumbuka kwamba shingo ya kizazi hufanya kazi kama kizuizi cha kuzuia bakteria au virusi wasiingie kwenye mfuko wa kizazi(uterus). Lakini shingo ya kizazi pale inapopata maambukizi au inapodhurika, huwa kuna uhatari mkubwa mno kiasi kwamba bakteria wa maambukizi huweza kusafiri mpaka kwenye mfuko wa uzazi(uterus).
NUKUU: Uvimbe wa shingo ya kizazi uliosababishwa na kisonono au pangusa unaweza kusambaa na kuenea mpaka kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi na kwenye mirija ya uzazi, hali ambayo husababisha maambukizi katika via vya uzazi yaani (PID), maambukizi yanayokuwa kwenye viungo vya uzazi ambayo yanaweza kusababisha matatizo ya ugumba kwa mwanamke ikiwa kama yataachachwa bila kutibiwa.
Hali ya kuvimba kwa shingo ya kizazi inaweza kuleta hatari ya mwanamke kupata maambukizi ya HIV kutoka kwa mtu aliyeathirika.
Je, Unawezaje Kujiepusha Tatizo Hili Lisikupate?
Ili kupunguza hatari ya kuvimba kwa shingo ya kizazi kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, basi unapaswa utumie Kondom kila ufanyapo mapenzi na mtu usiyemwamini. Kondom husaidia sana katika kuzuia kusambaa kwa magonjwa ya ngono kama vile kisonono na pangusa, ambayo yanaweza kusababisha shingo ya kizazi kuvimba.
TIBA ZAKE
James & Ferdinand Herbal Clinic tuna dawa nzuri zenye mchanganyiko wa mimea ya asili, nazo ni antibiotic zenye uwezo wa kuondoa uvimbe huo nazo ni REDEEMER, FRESH HERB na VITAMAKA. Lakini kama uvimbe huo umesababishwa na vimelea wa maambukizi, utapaswa pia kupata dawa nzuri ambayo ni MULTI-POWDER.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626
Tupo Arusha-Mbauda, pia Njombe Makambako Mtaa Wa Kahawa.
Karibuni sana!