JE, UNAJUA CHAKULA UNACHOTAKIWA KUTUMIA WAKATI WA UJAUZITO?

Je, lishe wakati wa ujauzito humaanisha nini? Tunaposema lishe wakati wa ujauzito, hatuzungumzii juu ya kujizuia kula vyakula vyenye wingi wa calories au kujaribu kupunguza uzito wa mwili. Lishe ya kupunguza uzito wakati wa ujauzito inaweza kusababisha hatari au madhara kwako wewe mwenyewe au mtoto aliyemo tumboni, hasa pale uzito wa mwili unapopungua unaweza kukufanya ukapungukiwa madini ya chuma, folic acid pamoja na vitamin na madini mengine yenye umuhimu.

Diet During Pregnancy

Kwahiyo, tunapendekeza ujiepushe na vyakula vingine kama vile, chips, sambusa, keki, tambi, chapatti, vitumbua, nk.

Aina ya vyakula tunavyokushauri utumie wakati wa ujauzito vitakuweka kwenye tabia ya kula vyakula vizuri ili kuhakikisha kuwa unapata lishe ya kutosha kwa ajili ya afya yako pamoja na mtoto wako. Ulaji mzuri wenye afya wakati wa ujauzito unafaa sana kumfanya mtoto aliye tumboni aweze kukua. Ili kupata virutubishi unavyohitaji, unapaswa kula makundi tofautitofauti ya chakula, ikiwemo matunda, mbogamboga, mkate, nafaka, vyakula vyenye wingi wa protini, nk.

 

Makundi Ya Chakula

 

 

Kama mama mjamzito, yafaa sana ule vyakula mbalimbali kutwa nzima ili uweze kupata virutubishi katika mwili wako na mwanao pia. Hapa unaweza kuangalia makundi ya chakula na virutubishi vyake vinavyoweza kusaidia kutengeneza afya yako unapokuwa mjamzito.

 

 

 

  1. Matunda Na Mboga Za Majani

 

 

Matunda pamoja na mbogamboga huwa yana virutubishi vingi vizuri kwa ajili ya ujauzito hasa, vitamin C na Folic Acid. Wanawake wajawazito wanahitaji angalau milligram 70 za vitamin C kila siku, ambayo hupatikana kwenye matunda kama vile machungwa, mizabibu, na mboga mboga kama vile mchicha, chanya, broccoli, na mnafu.

Diet During Pregnancy: Food Groups

NUKUU: Chanzo kizuri cha Folic Acid kinaweza kupatikana kwenye mboga za majani. Pia zinapatikana kwenye bamia. Hivyo unapaswa utumie aina 2-4 za matunda au aina 4 za mbogamboga kila siku.

 

Diet During Pregnancy: Fruits and Vegetables

 

 

 

  1. Mkate Na Nafaka

 

 

Chanzo kikuu cha nishati ya mwili kwa mjamzito hutokana na wanga inayopatikana kwenye vyakula vya nafaka. Nafaka ambayo haijakobolewa na vyakula vyenye wingi wa virutubishi kama vile madini ya chuma, Vitamini B, fiber, na protini. Unaweza ukapata kiwango kinachotakiwa chenye wingi wa folic acid kutoka kwenye nafaka.

 

 

  1. Vyakula Vya Protini

 

 Nyama, samaki, mayai, pamoja na maharage huwa vina wingi wa protini, Vitamini B na madini ya chuma yanayohitajika kwa mama mjamzito. Mtoto wako anayeendelea kukua tumboni huwa anahitaji wingi wa protini hasa anapofikisha kipindi cha miezi 5-9. Madini ya chuma husaidia kubeba hewa ya oksijeni na kuipeleka kwa mtoto akiwa tumboni, na pia husaidia kupelekea hewa ya oksijeni kwenye misuli yako ili kusaida kuzuia dalili kama vile uchovu, udhaifu, msongo wa mawazo, nk.

 

  1. Maziwa

 

 

Angalau milligram 1000 za Calcium huhitajika sana kila siku ili kusaidia ujauzito. Madini ya Calcium yafaa sana katika kujenga mifupa na meno, damu nzuri itokapo inaganda haraka kwenye jeraha, pamoja na utendaji kazi wa misuli. Pamoja na kuwa mtoto anayekuwa tumboni anahitaji kiwango kizuri cha madini ya Calcium, lakini bado mwili wako utahitaji kuchukua madini hayo kwa ajili ya mifupa yako ikiwa kama hutakula chakula cha kutosha chenye wingi wa madini ya Calicum, hali ambayo inaweza kupelekea kuwapo kwa matatizo mabaya baadaye kama vile mifupa kuwa laini.

Diet During Pregnancy: A Complement to Nutrition

Chanzo kizuri cha madini ya Calcium ni maziwa, supu ya samaki, nk. Baadhi ya madini ya Calcium pia hupatikana kwenye mboga za majani, dagaa, na maharage.

 

  1. Vidonge Vya Kuongeza Virutubishi(Vitamini na Madini)

 

 

 

Ingawa chanzo kikuu cha vitamin na virutubishi vinavyohitajika wakati wa ujauzito kinapaswa kutoka kwenye vyakula unavyokula, lakini vidonge vya kuongeza lishe mwilini vinaweza kusaidia kuziba pengo dogo ikiwa kama hupati vyakula vya lishe vya kutosha. Vidonge vya kuongeza virutubishi mwilini vinapaswa vitumiwe ndani ya miezi mitatu kabla hujabeba ujauzito, ikiwezekana.

 Madre embarazada tomando vitaminas prenatales

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

James & Ferdinand Herbal Clinic tunapatikana Arusha-Mbauda, pia Njombe-Makambako.

 

 

Karibuni sana

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

One thought on “JE, UNAJUA CHAKULA UNACHOTAKIWA KUTUMIA WAKATI WA UJAUZITO?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *