JE, NINI TOFAUTI KATI YA MAAMBUKIZI YA KISONONO NA PANGUSA?

Ujue Ugonjwa Wa Kisonono Na Pangusa.

 

 

 

Pangusa(Chlamydia) na kisonono(Gonorrhea) huwa ni maambukizi ya magonjwa zinaa yanayosababishwa na baketria. Nayo yanaweza kuambukizwa kwa kujamiiana au kwa kunyonyana ulimi.

Dalili za magonjwa haya mawili ya zinaa zinafana, hivyo kama una moja ya dalili hizo, wakati mwingine huwa ni vigumu daktari kuzihakiki bila kutumia vipimo.

Picha inayohusiana

Baadhi ya watu wenye maambukizi ya kisonono au pangusa wanaweza wasiwe na dalili. Lakini pale dalili zinapojitokeza, huwa kuna mifanano, kama vile hali kutokuwa ya kawaida, uchafu wenye harufu mbaya kutoka ukeni au kwenye uume au kuhisi hali ya kuwaka moto pale unapokojoa.

Je, Dalili Za Maambukizi Haya Zinafananaje?

 

 

 

Wanaume na wanawake wanaweza kupata maambukizi ya pangusa au kisonono na kamwe wasiendelee kuona dalili zozote.

Kwenye maambukizi ya pangusa, dalili zinaweza zisionekane kwa wiki chache baada ya kuambukizwa ugonjwa huo. Na kwenye kisonono, wanawake kamwe wanaweza wasione dalili zozote hata kidogo au wanaweza wakaona dalili za kawaida tu, wakati wanaume wao huona dalili mbaya zaidi tena kwa muda mfupi tu.

NUKUU: Dalili za magonjwa haya mawili hufanana kwa wanaume na wanawake kama vile:

 

  • Kuhisi hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa

 

  • Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ukeni au kwenye uume

 

 

  • Kutokwa na uchafu sehemu za njia ya haja kubwa

 

  • Kuhisi maumivu sehemu za njia ya haja kubwa

 

 

  • Kutokwa na damu sehemu ya njia ya haja kubwa

 

Je, Dalili Za Pangusa Zinakuwaje?

 

 

Katika ugonjwa wa pangusa, wanawake wanaweza kupatwa na dalili mbaya endapo kama maambukizi yataenea kupanda juu kwenye mfuko wa uzazi(uterus), mpaka kwenye mirija ya uzazi. Hali hii inaweza kusababisha maambukizi katika via vya uzazi au PID.

 

PID au maambukizi katika via vya uzazi yanaweza kusababisha dalili kama vile:

 

  • Homa

 

  • Kujihisi kuumwa

 

 

  • Kutokwa na damu ukeni hata kama hauko kwenye kipindi cha hedhi

 

  • Maumivu makali sehemu za nyonga

 

Picha inayohusiana

 

NUKUU: Napenda nikushauri tu kwamba, jitahidi kupata vipimo haraka endapo kama utaanza kuona dalili hizo nilizozitaja hapo juu.

 

Je, Dalili Za Kisonono Zinakuwaje?

 

Kwa maambukizi ya kisonono, unaweza pia kuona dalili katika maeneo ya njia ya haja kubwa kama vile muwasho, vidonda na maumivu wakati unapojisaidia haja kubwa.

Wanawake pia wanaweza kuona dalili za kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

 

Je, Nini Husababisha Magonjwa Haya Mawili?

 

 

 

Magonjwa haya mawili husababishwa na kukua kwa bakteria. Pangusa husababishwa na kuku kwa bakteria wanaoitwa, “Chlamydia trachomatis”.

 

Kisono husababishwa na kukua kwa bakteria wanaoitwa, “Neisseria gonorrhoeae”.

 

Je, Ni Jinsi Gani Kila Ugonjwa Huambukizwa?

 

 

Magonjwa yote haya ya zinaa husababishwa na maambukizi ya bakteria ambayo huambukizwa kupitia ngono bila kinga. Ni rahisi kupata maambukizi kupitia ngono kama ukikutana na mwenza ambaye tayari ana maambukizi hayo.

 

Pia maambukizi ya magonjwa ya zinaa unaweza kuyapata hata kama ukitumia kinga na ikapasuka. Magonjwa ya zinaa yanaweza kuambukizwa hata kama huonyeshi dalili za maambukizi. Maambukizi ya magonjwa haya yanaweza pia kuambukizwa kwa mtoto wakati mama anapojifunga endapo kama mama mwenye ana maambukizi hayo.

 

 

Je, Ni Nani Aliye Kwenye Hatari Zaidi?

 

 

 

 

Uko kwenye hatari zaidi kwenye kuendelea na matatizo haya pamoja na magonjwa mengine ya zinaa ikiwa kama:

 

 

  • Utakuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja

 

  • Hutatumia vizuri kinga kama vile kondom

 

  • Utakuwa ukitumia marashi maeneo ya uke ili kuua bakteria

 

  • Umeathiriwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kabla

 

Tabia mbaya ya ngono inaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya kisonono pamoja na pangusa. Jitahidi kupata vipimo mapema iwezekanavyo kama umewahi kufanya uasherati na mtu usiyemjua historia yake vizuri.

 

Je, Jinsi Gani Kila Ugonjwa Hupimwa?

 

 

Magonjwa yote haya mawili ya zinaa yanaweza kupimwa kwa kutumia vipimo vya aina moja.

Picha inayohusiana

Daktari wako anaweza kuvitumia vipimo hivi mara moja au zaidi ili kuhakiki kwamba kipimo kiko sahihi na kwamba tiba barabara kabisa inatolewa baada ya kufanya:

 

  • Uchunguzi wa mwili ili kuona dalili za magonjwa ya zinaa na kubaini afya ya mwili wako wote

 

  • Vipimo vya damu kwa ajili ya kuona dalili za maambukizi ya bakteria

 

 

  • Uchunguzi wa kuchukua sampuli ya uchafu unaotoka kwenye uume au uke au njia ya haja kubwa ili kupima na kuona dalili au ishara za maambukizi.

 

Je, Ni Jinsi Gani Kila Ugonjwa Unatibiwa?

 

 Magonjwa yote haya mawili ya maambukizi yanatibika na yanaweza kutibiwa kwa dawa za asili, lakini unaweza ukaambukizwa tena kama uliwahi kupatwa na magonjwa haya hapo awali. Dawa hizo ni BEST GREEN na FRESH HERB.

NUKUU: Jihadhari kufanya tendo la ndoa mpaka pale daktari wako atakapokuambia kwamba maambukizi yameshaisha mwilini mwako. Yaweza kuchukua wiki 2-3 au zaidi maambukizi kuweza kuondoka kabisa mwilini, na wakati huo, unaweza kuendelea kuambukiza ugonjwa kwa mtu mwingine ikiwa kama utafanya tendo la ngono.

 

Je, Ni Madhara Gani Yanaweza Kutokea Katika Magonjwa Haya Mawili?

 

 

Baadhi ya madhara ya maambukizi haya ya zinaa yanaweza kujitokeza kwa mtu yeyote. Mengine huwa ni ya pekee kwa kila jinsia kutokana na tofauti zinazokuwepo katika kujamiiana. Kisonono kina madhara mengi na kinaweza kusababisha matatizo ya ugumba ya muda mrefu kwa mwanaume na mwanamke pia.

 

Madhara ambayo yanayoweza kuonekana kwa mtu yeyote yanaweza kuwa:

 

  • Kupatwa kwa urahisi na magonjwa mengine ya zinaa
  • Maumivu kwenye viunganishi vya mifupa(hii ni pangusa peke yake). Hali hii hutokana na maambukizi kwenye njia ya mkojo(mrija wa mkojo, kibofu cha mkojo, figo na mirija inayoungana na figo zako kushuka kwenye kibofu cha mkojo(ureters), au utumbo mpana. Dalili za hali hii husababisha maumivu, uvimbe, au viunganishi vya mifupa na macho kukaza, pamoja na dalili mbalimbali.

 

  • Maharibifu kwenye viungo vya uzazi au mbegu za mwanaume zinaweza kuleta changamoto kubwa, na kumfanya mwanamke kushindwa kubeba ujauzito au mwanaume kushindwa kumpa ujauzito mwanamke.

 

 

  1. Je, Kwa Wanaume Inakuwaje?

 

 

 

 

  • Maambukizi kwenye Korodani: Bakteria wa Pangusa au Kisonono wanaweza kuenea kwenye mirija ya korodani zako na kusababisha kuvimba kwa korodani. Hali hii inaweza kusababisha korodani kuvimba au kuwa na maumivu makali.

 

  • Maambukizi kwenye tezi dume: Bakteria kutokana na maambukizi haya mawili wanaweza kuenea kwenye tezi dumu yako, hali ambayo huongeza majimaji kwenye manii zako wakati unapofika kileleni. Hali hii inaweza kufanya maumivu makali pale unapofika kileleni au unapokojoa, na kusababisha homa au maumivu kwenye kiuno chako.

 

  1. Je, Kwa Wanawake Inakuwaje?

 

 

 

  • Maambukizi Katika Via Vya Uzazi Au PID: Maambukizi haya hutokea wakati mfuko wako wa uzazi(uterus) au mirija ya uzazi inapopata maambukizi. PID huhitaji tiba haraka ili kuzuia maharibifu kwenye viungo vyako vya uzazi.

 

  • Magonjwa yote haya mawili ya zinaa yanaweza kuambukizwa mtoto mchanga wakati mama anapojifungua huku akiwa na maambukizi haya. Hali hii inaweza kujitokeza kwenye madhara kama vile maambukizi kwenye macho au pneumonia.

 

  • Mimba Kutunga Nje Ya Uzazi: Magonjwa haya ya zinaa yanaweza kusababisha yai lililorutubishwa likajipachika kwenye tishu nje ya mfuko wa uzazi. Aina hii ya ujauzito huwa haudumu na unaweza ukamtia hofu mama mjamzito na hata maisha yake ya ujauzito baadaye.

 

 

Je, unahitaji huduma? Kwa mawasiliano tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

 

Tunapatikana Arusha-Mbauda pia Njombe Makambako.

 

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *