Kuna aina tofauti za ugonjwa wa homa ya ini ambao kitaalamu wanaita, “Hepatitis”, yaani Hepatitis A, B, C, nk ambao unaweza kutofautiana kila mmoja lakini magonjwa yote haya huonyesha uvimbe wa seli za ini.
Virusi hivi ni moja ya aina mbalimbali za virusi vya homa ya ini ambavyo husababisha uvimbe na kuathiri ini uwezo wa ini lako kuweza kufanya kazi.
Unaweza ukapata virusi vya hepatitis A kutokana na vyakula au maji yaliyotumiwa na mtu au kitu kilichoambukizwa. Ugonjwa wa kawaida wa homa ya ini aina ya hepatitis A hauhitaji matibabu. Watu wengi walioambukizwa hupona moja kwa moja bila kuwa na madhara au ini kuharibika.
NUKUU: Kuwa na tabia ya kufanya usafi mzuri, hasa katika kuosha mikono yako mara kwa mara, ni njia mojawapo ya kukulinda wewe usiweze kupatwa na maambukizi ya ugonjwa wa ini.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili za homa ya ini au hepatitis A huwa hazionekani mpaka utakapokuwa na virusi kwa muda wa wiki chahche. Lakini sio kila mmoja mwenye homa ya ini au hepatitis A anaweza kupatwa na dalili hizo. Kama utakuwa na dalili hizo, basi zitakuwa kama hivi unavyoona hapa chini:
- Kuhisi uchovu
- Kuhisi kichefuchefu ghafla na kutapika
- Tumbo kuuma hasa upande wa juu wa kulia chini ya mbavu zako za chini
- Kinyesi chenye rangi ya udongo
- Kukosa hamu ya kula
- Kuhisi homa
- Mkojo mweusi
- Viungo vya mwili kuuma
- Muwasho mkubwa mwilini.
NUKUU: Dalili hizi zinaweza kuwa za kiasi tu na kisha kutoweka kwa muda wa wiki chache tu. Wakati mwingine hata hivyo, maambukizi ya homa ya ini au hepatitis A hutokana na ugonjwa sugu ambao hudumu kwa muda wa miezi kadhaa.
Je, Ni Muda Gani Unapaswa Umuone Daktari?
Jitahidi ufike hospitali ikiwa kama unaona dalili za ugonjwa wa homa ya ini au hepatitis A. Upatapo chanjo ya homa ya ini ndani ya wiki 2 baada ya kuona dalili zake kunaweza kukusaidia usipate madhara. Muulize daktari au muhudumu yeyote wa afya aliye karibu yako jinsi ya kupata chanjo ya homa ya ini ikiwa kama;
- Uliwahi kufanya tendo la noda na mtu mwenye maambukizi ya homa ya ini.
- Umewahi kusafiri nje ya nchi ambako ugonjwa huu umeenea.
- Mgahawa ambapo uliwahi kula chakula lakini kumetolewa taarifa juu ya ugonjwa huo
- Kuna mtu uliyekuwa karibu naye kama vile muhudumu au mwenzi ambaye amewahi kupimwa na akakutwa na ugonjwa wa homa ya ini
Je, Nini Visababishi Vyake?
Homa ya ini(hepatitis A) husababishwa na virusi ambavyo huathiri seli za ini na kusababisha uvimbe. Uvimbe huo unaweza kuathiri jinsi ini lako linavyofanya kazi na kusababisha dalili zingine za homa ya ini(hepatitis A).
Virusi kwa kawaida huenea unapokula au kunywa kitu kilichochafuliwa na vitu vyenye kinyesi hata kama ni kwa kiwango kidogo. Ugonjwa huu hauenei kwa njia ya kikohozi au kukoroma.
Hapa kuna njia maalumu zinazoonyesha jinsi ugonjwa wa homa ya ini unavyoenezwa, nazo ni kama ifuatavyo:
- Kunywa maji machafu
- Kufanya tendo la ndoa na mtu mwenye virusi vya homa ya ini
- Kula chakula kilichoshikwa na mtu mwenye virusi ambaye haoshi mikono yake vizuri baada ya kutoka chooni
- Kuwa karibu na mtu ambaye tayari ana maambukizi hata kama mtu huyo hana dalili
Je, Madhara Yake Yanakuwaje?
Homa ya ini(hepatitis A) huwa haisababishi uharibifu wa ini wa muda mrefu, na wala hauwezi kuwa sugu. Sio kama aina ya virusi vingine vya homa ya ini
NUKUU: Homa hii ya ini(hepatitis A) huwa ni mara chache sana kuweza kusababisha ini kushindwa kufanya kazi kwa ghafla, hasa kwa watu wenye umri mkubwa au watu wenye magonjwa sugu ya ini. Hali sugu ya ini kushindwa kufanya kazi huhitaji muda wa kukaa hospitali ili kusimamiwa na kuhudumiwa kwa matibabu. Baadhi ya watu wenye tatizo sugu la ini kushindwa kufanya kazi wanaweza kuhitaji kupandikiziwa ini.
Je, Unawezaje Kuwa Na Tahadhali Pale Unapokuwa Safirini?
Kama unasafiri kuelekea sehemu mbalimbali za mikoa au nje ya nchi zilizo na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya ini(hepatitis A), basi chukua hatua hizi ili kuzuia maambukizi:
- Osha na umenye matunda unapotaka kula
- Usile nyama ambayo haikupikwa au kuchomwa vizuri ikaiva
- Kunywa maji ya kwenye chupa(kama vile Uhai, Kilimanjaro, nk)
- Epuka vinywaji vyote usivyovifahamu vizuri
- Kama maji ya chupa hayapatikani, basi jitahidi kuchemsha maji kwanza
NUKUU: Osha mikono yako vizuri mara kwa mara, hasa baada ya kutoka chooni na kabla hujaanza kuandaa chakula.
Napenda kuishia hapa wapendwa wasomaji wote juu ya makala hii ya “Hepatitis A”. Je, unahitaji huduma juu ya tatizo hili? Basi tupigie kwa namba hii: 0752 389 252 au 0712 181 626-Mbauda Arusha.
Pia tunakukaribisha katika darasa letu la masomo ya afya katika mtandao wa Telegram, unaweza ukatuma namba yako ya WHATSSAP au TELEGRAM tukakuunganisha ukajipatia masomo bure.
K aribuni sana!