JINSI YA KUTAMBUA MABADIRIKO KWENYE UTE UTE UNAOTOKA KWENYE SHINGO AU MLANGO WA UZAZI(CERVICAL MUCUS).

Ute ute utokao kwenye mlango wa kizazi hutajwa kwa majina mengi, lakini kuja kuutambua jinsi unavyobadirika katika mzunguko wako wote wa hedhi, na nini kinachoufanya ubadirike, na ukishagundua maana yake kabisa, utakuwa umeshapata somo kubwa tena lenye nguvu.

NUKUU: Hapo chini kuna picha nimeonyesha jinsi uteute huo unavyobadirika ndani ya mzunguko mmoja wa hedhi. Kumbuka kila mwili unajitegemea na huwa wa pekee kabisa, na ndio maana kuna kuwa na tofauti kwa kila mwanamke.

 

  1. Uteute Unaotoka Kabla Ya Yai Kupevuka

 

 

Yai kupevuka huwa ni hali ya kuachiliwa kwa yai lililokomaa, nalo huchukua kama wiki chache baada ya siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi. Uzarishaji wa ute ute huwa ni matokeo ya mabadiriko ya homoni au vichochezi ambavyo hutokeza wakati wa kipindi hiki. Ute wako huendelea kubadirika kati ya siku ya kwanza ya kipindi chako cha hedhi pamoja na siku yai linapopevuka, na hivyo mlango au shingo yako ya kizazi unaweza kuanza kuutengeneza muda wowote baada ya hedhi yako kukoma(na hata kabla kipindi chako cha hedhi hakijakoma endapo kama una kipindi kirefu).

dry / cell slough – The Cervical Mucus Project

Sehemu hii inaonyesha mabadiriko ya ute ute ambao huwa ni wa kawaida wakati wa majuma machache ya mwanzo baada ya vindi vya hedhi kuanza.

NUKUU: Baada ya hedhi kuisha huwa hakuna uteute unaotoka.

 

Siku chache za mwanzoni baada ya kutoka hedhini, uke unaweza kuwa mkavu tu, nikimaanisha kwamba hakuna uteute unaozarishwa na mlango wako wa uzazi kama nilivyoonyesha kwenye picha hapo juu. Wakati wa kipindi hiki kinanachoonyesha ukavu ukeni, mbegu za mwanaume huwa haziwezi kuishi ndani ya uke wa mwanamke kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha joto pamoja na kuwa na wingi wa asidi kwenye maeneo ya uke wako.  Lakini hata kama wakati ute unapokuwa haupo, pia bado kunaweza kuwa na unyevunyevu ukeni, ute huu unaokuwa ukeni huwa ni wa asili ambao husaidia kuufanya uke wako kuwa katika hali yenye afya.

 

 

  1. Kuzarishwa Kwa Ute Siku Ya Kwanza: Ute Wenye Mnato Na Wenye Kuteleza.

 

 

Baada ya hedhi kuisha, mlango wako wa uzazi huanza kuzarisha uteute, nah ii humaanisha kwamba mwili wako unapambana kulifanya yai lipevuke. Lengo la uteute ni kuzifanya mbegu ziweze kuishi na kuzisaidia ziweze kulifikia yai.  Ute unapokuwapo kwenye mlango wa uzazi, mbegu zinaweza kudumu ndani ya uzazi kwa muda wa siku 5 zikisubilia yai liweze kuachiliwa.

Visualizing Changes in Your Cervical Fluid (Cervical Mucus)

NUKUU: Ute wa shingo ya kizazi kwa kawaida huanza kutoka huku ukiwa mzito, wenye kunata, na unaweza kuwa kama maziwa mgando au losheni vile. Unaweza kuchanganyikana na pia na kiwango kidogo cha ute wenye utelezi kama nilivyoonyesha hapo kwenye picha.Ute ute Unaozarishwa Siku Ya Pili: Ni Ute Wenye Kuteleza Na Wenye Kunata.

  • Ute ute Unaozarishwa Siku Ya Pili: Ni Ute Wenye Kuteleza Na Wenye Kunata.

 

 

Siku ya kwanza unapoanza kutoka ute huwa ni wenye kunata, tena wenye kuteleza. Leo hata hivyo, ute umekuwa wenye kuteleza kabisa, na una kiwango kidogo cha mnato. Ute ute utazidi kuwa wenye unyevu kabisa na kuteleza kadiri hali ya upevushaji inapokaribia siku zinazofuata.

Visualizing Changes in Your Cervical Fluid (Cervical Mucus)

 

  • Uzarishaji Wa Ute Siku Ya 3: Ute Huwa Wenye Mnato, Wenye Kuvutika.

Ute ute unaendelea kuwa wenye unyevu tena wenye kuteleza kabisa. Leo utaona ute ni wenye kuteleza na kuvutika. Kuongezeka kwa majimaji ya ute kunaweza kusaidia mbegu kuwa hai ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa muda wa siku nyingi, na huzisaidia mbegu kusafiri kutoka ukeni mpaka kwenye mirija ya uzazi ili kulifikia yai.

 

Pin on Birth

Utaona hapo juu kwenye picha jinsi ute unavyokuwa

 

  1. Uzarishaji Wa Ute Siku Ya 4: Ute Huwa Wenye Unyevunyevu, Wenye Kuteleza Pia.

 

Leo, utaona kiwango cha ute wenye majimaji, ute wenye rutuba umeongezeka sana. Ute unavutika kidogo, una unyevu sana, na unateleza sana na kuufanya uweze kuwa bora zaid kwenye mbegu za mwanaume.

Clear Watery Discharge After Menopause - Menopause Choices

Pia unaweza kuona hapo juu jinsi ute huo unavyokuwa.

 

 

Siku Ya Mwisho Kutoka Kwa Ute, Inakuwaje?

 

 

  • Uzarishaji Wa Ute Siku Ya 5: Ute Huwa Mwepesi, Wenye Unyevunyevu, Na Wenye Kuteleza.

 

Kiwango cha majimaji cha ute wa leo ni mkubwa sana, na kuufanya ute kuwa mweupe kama ute wa yai la kuku, wenye kuteleza na unaendana na mbegu za mwanaume kabisa. Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, ute huu unakuwa na rangi kama ya pink kwa mbali ambao huwa ni wa kawaida kabla ya yai kupevuka.  Kama utakavyoona kwenye picha hizo chini, kwenye siku ya 6 na ya 7, ute kwenye mlango wa uzazi huanza kukauka baada ya siku ya leo kupita.

Watery white discharge, could it be amniotic fluid??? - July 2018 ...

NUKUU: Hii huifanya siku ya leo kuwa siku ya mwisho ya ute wenye kuteleza katika mzunguko wa hedhi.

 

 

Je, Ute Baada Ya Yai Kupevuka Unakuwaje?

 

 

  1. Uzarishaji Wa Ute Siku Ya 6: Ute Huwa Mweupe, Mzito, Wala Hautelezi.

 

 

Leo, ute umegeuka na kuwa mzito, tena mweupe. Japokuwa jana ilikuwa siku ya mwisho ute kuwa wenye unyevunyevu, wenye kuteleza kabla haujaanza kukauka, inaonekana kwamba ndio siku ya kufikia mwisho mwanamke kupata ujauzito.

Visualizing Changes in Your Cervical Fluid (Cervical Mucus)

NUKUU: Baada ya yai kupevuka, vichochezi au homoni hubadirika na kusababisha ute kukauka. Mlango wa kizazi bado unatengeneza ute kuonyesha yai linapevuka, lakini utakuwa mzito, wenye kunata, wenye muonekano kama maziwa, tepetepe, au kama losheni. Hata hivyo hautakuwa wenye kuteleza na hautaweza kuendana na mbegu za mwanaume.

 

  • Uzarishaji Wa Ute Siku Ya 7: Ute Huwa Mweupe, Mzito, Wenye Kunata Lakini Hautelezi.

 

 

Baada ya yai kupevuka, mabadiriko ya homoni husababisha ute kukauka, lakini mwili wako unaweza kuendelea kuzarisha uteute mpaka kipindi chako cha hedhi kinachofuata kitakapoanza. Ute unaotoka kabla ya yai kupevuka unaweza kuwa wenye kunata, mzito, wenye muonekano kama mafuta au losheni, kama unavyouona hapo juu.

NUKUU: Hata hivyo, ute unaozarishwa baada ya yai kupevuka hautakuwa wenye kuteleza wala wenye kulainisha sehemu za uke, na hautaendana na mbegu za mwanaume.

 

Nipende kuishia hapa wapendwa wasomaji, nikaribishe kipindi cha maswali, karibuni sana.

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

Arusha-Mbauda

 

 

Karibuni sana

2 thoughts on “JINSI YA KUTAMBUA MABADIRIKO KWENYE UTE UTE UNAOTOKA KWENYE SHINGO AU MLANGO WA UZAZI(CERVICAL MUCUS).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *