Mwanamke kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa ni jambo la kawaida. Ingawa mara nyingi huitwa kutokwa na damu ukeni, lakini mara nyingi hali ya kutokwa na damu kwa wanawake wenye umri mdogo hutokea kwenye mlango au shingo ya kizazi. Hata hivyo maeneo mengine ya sehemu za siri za mwanamke pamoja na mfumo wa mkojo nazo zinaweza kuhusika.
Zipo sababu nyingi kwanini mwanamke hutokwa na damu baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa. Tatizo hili kitaalamu tatizo hili huitwa, “Postoital bleeding.”
NUKUU: Kama unatokwa na damu ukeni baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa, basi jitahidi kutafuta ushauri hospitali kwa daktari wa mambo ya uzazi.
Je, Ni Husababisha Damu Kutoka Ukeni?
Kutokwa na damu ukeni baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa, huwa ni ishara au dalili magonjwa haya yafuatayo:
- Salatani ya mlango wa kizazi
- Kuvimba kwa mlango wa kizazi
- Maambukizi katika via vya uzazi(PID)
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile pangusa, nk
- Uke kukauka kutokana na kupungua kwa ute au kukoma kwa hedhi
- Kuharibika kwa uke kutokana na msuguano wakati wa tendo la ndoa
- Kuchubuka kwa shingo au mlango wa uzazi
- Mzunguko wa hedhi kubadirikabadirika
- Vidonda ukeni vitokanavyo na maambukizi ya zinaa
- Salatani ya tumbo la uzazi
- Mlango wa kizazi kutokeza nje ya uke
NUKUU: Kwa mifano hii, kutokwa kwa damu baada ya tendo la ndoa kunaweza kuwa ni ishara ya salatani ya uke au mlango wa kizazi.
Je, Vipimo Vyake Hufanyikaje?
Kutegemeana na dalili zozote zingine pamoja na historia ya matibabu uliyowahi kutumia, basi daktari anaweza kupendekeza baadhi ya vipimo kama vile;
- Vipimo vya uzazi au ujauzito(kutegemeana na umri wako)
- Vipimo kwenye nyonga ambapo daktari huingiza vidole viwili ukeni
- Kuangalia kwenye mlango wa uzazi kwa kutumia chombo kiitwacho, “speculum.
NUKUU: Kama tatizo linasababishwa na ukavu wa uke, basi wanaweza kupendekeza kwamba ujaribu kutumia mafuta kupakaa ukeni wakati unapotaka kufanya tendo la ndoa.
Vipimo Vya Uchunguzi Wa Shingo Ya Mlango Wa Uzazi
Yafaa kwamba wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 25-64 waweze kupata vipimo mara kwa mara kwa ajili ya shingo ya kizazi ili kusaidia kuzuia salatani ya shingo ya kizazi.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda
Pia tunatoa ushauri bure na masomo ya afya kila siku katika GROUP letu katika mtandao wa TELEGRAM. Unahitaji kujiunga na darasa letu, tuma namba yako ya WHATSSAP tuweze kukupatia link yetu.
Karibuni sana!