Takribani asilimia 15% ya wanandoa ni wagumba. Hii inamaanisha kwamba hawana uwezo wa kuzaa mtoto, ingawa wamekuwa wakifanya tendo la ndoa miaka mingi bila kutumia kinga. Zaidi ya theruthi ya wanandoa hawa, tatizo la ugumba kwa wanaume ndilo limekuwa likionekana.
Ugumba wa mwanaume hutokana na uzarishaji mdogo wa mbegu, utendaji kazi wa mbegu za mwanaume usio wa kawaida au hali ya kuziba ambayo huzuia usafirishaji wa mbegu. Maradhi, ajari, matatizo sugu katika afya yako, mitindo ya maisha uliyochagua pamoja na vigezo vingine vinaweza kusababisha hali ya ugumba kwa mwanaume.
NUKUU: Kutokuwa na uwezo wa kumbebesha mimba mwanamke kunaweza kukufanya kuwa na msongo wa mawazo mkubwa sana, lakini nipende kukujulisha tu kuwa, hali ya ugumba kwa mwanaume inatibika vizuri sana.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Ishara za ugumba wa mwanaume ni kutokuwa na uwezo wa kumbebesha ujauzito mwanamke. Kunaweza kusiwepo na dalili au ishara zingine zilizo wazi. Kwa maana hiyo, hata hivyo, matatizo ya msingi kama vile magonjwa ya kurithi, kutokuwa na uwiano sawa wa homoni, mishipa inayokuwa kwenye koroda kuvimba au ugonjwa ambao huifanya njia ya mbegu au shahawa kuziba na kusababisha ishara na dalili.
Ijapokuwa wanume wengi wenye tatizo la ugumba huwa hawaoni dalili zaidi ya kutokumtungisha mimba mwanamke, ishara na dalili zinazoambatana na ugumba wa mwanaume ni kama ifuatavyo:
- Maumivu, uvimbe kwenye eneo la korodani
- Maambukizi katika mfumo wa upumuaji
- Kutokuwa na uwezo wa kunusa
- Matiti kuwa makubwa
- Kupungukiwa kwa homoni hasa ya testosterone
- Kuwa na kiwango kidogo cha mbegu(chache sana chini ya mbegu milioni 15 kwa mililita za shahawa au kiwango kamili cha mbegu chini ya milioni 39 kwa kila unapotoa mbegu).
- Kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa, kwa mfano; kushindwa kufika kileleni au kutoa kiwango kidogo cha mbegu, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, au uume kushindwa kusimama.
Je, Visababishi Vyake Ni Nini?
Uwezo wa mwanaume kupata mtoto huwa ni mchakato mkubwa. Kumfanya mwanamke kuwa mjamzito, mambo yafuatayo yanapaswa kutokea:
- Unapaswa Kutoa Mbegu Zenye Afya
Hapo awali, hii inajumuisha ukuaji na utengenezaji wa viungo vya uzazi wakati wa ujana. Angalau moja ya korodani zako lazima ziwe zinafanya kazi vizuri, na mwili wako lazima utoe homoni ya testosterone pamoja na homoni zingine ili kufyatua na kutengeneza uzarishaji wa mbegu.
- Mbegu Zinapaswa Zibebwe Kupitia Shahawa
Mbegu zinapozarishwa kwenye korodani, mirija maridi iliyopo huzisafirisha mpaka zichanganyikane na shahawa na kisha hutolewa nje kupitia uume.
- Kuna Uhitaji Wa Kutosha Mbegu Kuwa Kwenye Shahawa
Ikiwa kama idadi ya mbegu kwenye shahawa zako ziko chini(mbegu kidogo), hupunguza uwezo wa mbegu zako kurutubisha yai la mkeo au mwenza wako. Kiwango kidogo cha mbegu huwa chache chini ya milioni 15 kwa mililita za shahawa au chini zaidi ya milioni 39 kwa kila unapomwaga mbegu.
- Mbegu Lazima Zifanye Kazi Na Ziwe Na Uwezo Wa Kusafiri
Kama mwendo(motility) au utendaji kazi wa mbegu zako sio mzuri, basi mbegu zinaweza zisiwe na uwezo wa kulifikia au kupenya kwenye yai la mwenza wako.
Unaweza kuona hapo jinsi mwendo wa mbegu unavyokuwa hata kulifikia yai.
Je, Sababu Za Kiafya Zinakuwaje?
Matatizo ya uwezo wa mwanaume kuzaa yanaweza kusababishwa na shida mbalimbali za kiafya pamoja na matibabu. Baadhi ya haya matatizo ni:
- Kuvimba kwa mirija ya kusafirisha mbegu
- Maambukizi kama vile kisonono au HIV
- Mbegu kutoka kwenye korodani na kuingia kwenye kibofu cha mkojo
- Kuathirika kwa tezi ya hypothalamus, pituitary, thyroid na adrenal, na hivyo kusababisha kutokuwa na uwiano sawa wa homoni
- Kuharibika kwa mirija inayosafirisha mbegu
Je, Mitindo Ya Kimaisha Pamoja Na Vyakula Vingine Vyaweza Kuwa Chanzo?
Baadhi ya visababishi vingine vya ugumba kwa mwanaume vyaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Utumiaji Wa Madawa
Steroidi za anaboliki zinazotumiwa ili kusisimua nguvu za misuli zinaweza kusababisha korodani kusinyaa na uzarishaji wa mbegu kupungua.
Utumiaji wa madawa ya kulevya au bangi yanaweza kupunguza kwa muda kiwango na idadi ya mbegu.
- Matumizi Ya Pombe
Unywaji wa pombe unaweza kushusha viwango vya homoni ya testosterone, na kusababisha uume kushindwa kusimama na kupunguza uzarisha wa mbegu za mwanaume.
Ugonjwa wa ini uliosababishwa na unywaji wa pombe wa kupindukia pia unaweza kupelekea mwanaume kuwa na tatizo la ugumba.
- Msongo Wa Mawazo
Msongo wa mawazo unaweza kuingiliana na homoni mbalimbali zinazohitajika kwa ajili ya kuzarisha mbegu. Msongo wa mawazo wa muda mrefu, hasa matatizo ya kutokupata mtoto, yanaweza kuathiri kiwango chako cha mbegu.
- Uzito
Unene unaweza kuharibu uwezo wa mwanaume kuzaa kwa namna mbalimbali, ikiwemo kuathirika kwa mbegu zenyewe moja kwa moja pamoja na kusababisha mabadiriko ya homoni ambayo hupunguza uwezo wa mwanaume kubebesha ujauzito mwanamke.
- Huzuni:
Utafiti unaonyesha kwamba uwezekano wa ujauzito unaweza kuwa ni mdogo kama mwenza wa kiume atakuwa na huzuni kubwa. Kwa nyongeza, huzuni kwa wanaume inaweza kusababisha uume kushindwa kusimama kwasababu ya kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, uume kushindwa kudindisha, au kuchelewa kufika kileleni.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252/071218162
Arusha-Mbauda
Pia tuna darasa zuri kabisa katika mtandao wa TELEGRAM, tunatoa masomo mbalimbali ya afya na ushauri pia. Ukitaka kujiunga na darasa letu, tuma namba yako ya WHATSSAP upate link yetu.
Karibuni sana.