Hali ya mwanamke kutokwa na damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi, kitaalamu huitwa ‘Menorrhagia’. Ingawa hali ya kutokwa na damu nyingi huonekana kama jambo la kawaida kwa baadhi ya wanawake, lakini wengi wao huwa hawapatwi na hali ya kuishiwa damu.
NUKUU: Lakini inaonekana kuwa, mwanamke unapopatwa na tatizo hili hushindwa kufanya kazi zako hata kama ni ofisini, nyumbani, nk, kwasababu unatokwa na damu nyingi ikiambatana na hali ya vichomi. Napenda kukushauri kuwa uonapo tatizo hili tafadhari uongea na daktari wako mahali popote hospitali. Hakika zipo tiba kamili za ugonjwa huu.
Je, Dalili Za Ugonjwa Huu Zinakuwaje?
Kwa kawaida ishara ama dalili za tatizo hili huwa kama ifuatavyo:
- Kubadili pedi kila baada ya lisaa limoja
- Kuamka kila mara usiku kubadili pedi kutokana na kububujika kwa damu
- Kutokwa na damu zaidi ya siku 7
- Kutokwa na mabonge ya damu makubwa
- Kushindwa kufanya kazi kwasababu ya kutokwa na damu nyingi mfululizo
- Dalili za kupungukiwa damu, kama vile uchovu, au kuishiwa pumzi.
Je, Ni Wakati Gani Unapaswa Umuone Daktari Hospitalini Ili Uweze kupata Ushauri?
Napenda kukushauri kuwa yafaa utafute msaada wa tiba mapema kabla hujaanza kupata vipimo ikiwa utaona dalili zifuatazo:
- Uonapo damu inatoka nyingi ukeni na kulowanisha pedi ndani ya lisaa limoja tu
- Uonapo damu inarudia kutoka mara baada ya hedhi au kutokwa na damu ukeni mara kwa mara
- Uonapo hali yoyote ya kutokwa na damu ukeni baada ya siku zako za hedhi kukoma(Menopause?
NUKUU: Uonapo dalili kama hizo, ni vyema ukafika hospitali mapema ili kupata ushauri wa daktari kabla hujaanza vipimo.
Je, Ni Nini Husababisha Tatizo Hili La Kutokwa Na Damu Nyingi Wakati Wa Hedhi?
Kwa kawaida hali ya kutokwa na damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi husababishwa na mambo yafuatayo:
- Kutokuwa na uwiano sawa wa vichocheo(Hormone Imbalance):
Katika mzunguko wa kawaida wa hedhi, uwiano kati ya vichocheo(hormones) vya estrogen na progesterone hurekebisha ongezeko la utando wa uteute katika ukuta(endometrium) wa mfuko wa kizazi (uterus), ambao humwagwa wakati wa hedhi ili kuulinda ukuta wa kizazi.
Ikiwa kama hali ya kutokuwa na uwiano sawa wa vichocheo(hormone imbalance) ikitokea, basi tishu ya ukuta wa mfuko wa kizazi huendelea kuvimba na hatimaye humwagiwa damu nyingi ya hedhi.
Zipo hali mbalimbali zinazoweza kusababisha kutokuwa na uwiano sawa wa vichochezi(hormone imbalance), nazo ni vivimbe kwenye vifuko vya mayai, unene uliopindukia, matatizo katika tezi ya thyroid, nk.
- Vifuko Vya Mayai Kushindwa Kufanya Kazi
Ikiwa kama vifuko vyako vya mayai vinashindwa kuachia au kuruhusu mayai kutoka wakati wa mzunguko wa hedhi, hivyo mwili wako hushindwa kuzarisha vichochezi vya progesterone(hormone progesterone), inapohitajika wakati wa mzunguko wa kawaida wa hedhi. Hali hii husababisha kutokuwepo kwa uwiano sawa wa vichochezi(hormone imbalance), na inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi mfululizo wakati wa hedhi.
- Uvimbe Kwenye Mfuko Wa Kizazi(Uterine Fibroids)
Hali hii ya uvimbe aina ya Fibroid ambao sio saratani huota kwenye mfuko wa kizazi, nao huonekana wakati wa kipindi chako cha umri wa kuzaa. Uvimbe wa Fibroid unaweza kusababisha mwanamke kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi.
- Vivimbe Vidogovidogo
Vivimbe vidogovidogo vinavyoota kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi kwa ndani vinaweza kusababisha hali ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kwa mwanamke.
- Kuvimba Kwa Ukuta Wa Mfuko Wa Kizazi(Adenomyosis):
Hii huwa ni hali ambayo ukuta wa ndani wa mfuko wa kizazi(endometrium) hupenya na kuingia kwenye ukuta wa msuli wa ndani wa mfuko wa kizazi(Myometrium).
NUKUU: Kuvimba kwa ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus), unaweza kusababisha hali ya chango wakati wa hedhi, maumivu ya tumbo chini ya kitovu, na tumbo kuunguruma kabla ya kuingia kipindi cha hedhi na inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi sana mwanamke anapokuwa hedhini.
- Vidonge Vya Uzazi Wa Mpango:
Hali ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi wakati mwingine hujulikana kama madhara yatokanayo na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango. Baadhi ya wanawake hutumia vidonge vya uzazi wa mpango pasipo kufuata masharti ama ushauri wa daktari. Na ieleweke kuwa unapomuona daktari akakupa ushauri wa matumizi ya mpango wa uzazi, atakusaidia kujiepusha na madhara mbalimbali katika mfumo wako wa uzazi.
- Saratani Ya Shingo Ya Kizazi(Cervix Cancer)
Ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi unaweza kusababisha mwanamke kutokwa na damu nyingi mfululizo wakati wa hedhi, hasa ikiwa kama umeshafikia kipindi cha kukoma kwa hedhi(Menopausal). Baadhi ya wanawake wenye ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, mara nyingi hupatwa na dalili ya kutokwa damu nyingi ukeni kwa muda mrefu.
NUKUU: Uonapo dalili kama hii, ni vyema ukawahi hospitali ili kupata vipimo na kuweza kuhakiki kuwa ni tatizo gani linalosababisha kuwepo kwa hali kama hiyo.
Je, Nini Madhara Ya Kutokwa Na Damu Nyingi Wakati Wa Hedhi?
Hali ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi inaweza kusababisha madhara yafuatayo:
- Kupungukiwa Damu(Anemia):
Kutokwa damu nyingi kwa muda mrefu wakati wa hedhi kunaweza kusababisha kupungukiwa damu kwa kupunguza idadi ya mzunguko wa chembe hai chekundu za damu. Kiwango cha mzunguko wa chembe hai nyekundu za damu hupimwa na hemoglobin ambayo ni protini inayosaidia chembe hai nyekundu za damu kubeba hewa ya oksijeni na kuipereka kwenye tishu za mwili wako.
Upungufu wa madini ya chuma hutokea wakati mwili wako unapojaribu kufidia chembe hai za damu zilizopotea kwa kutumia akiba ya madini yako ya chuma ili kutengeneza hemoglobin nyingi, ambayo inaweza tena kubeba hewa ya oksijeni kwenye chembe hai nyekundu za damu. Hali ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi inaweza kusababisha kupungua kwa kiwango cha madini ya chuma na hivyo kusababisha kupungukiwa na damu mwilini.
NUKUU: Dalili zinazompata muhusika huwa ni ngozi au macho kupauka na kuwa nyeupe, mwili kuwa dhaifu na kuchoka. Japokuwa lishe husaidia kuongeza madini ya chuma, lakini tatizo husababishwa na kutokwa na damu muda mrefu wakati wa hedhi.
- Maumivu Makali Ya Tumbo:
Pamoja na kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, mwanamke anaweza akapatwa na maumivu makali wakati wa hedhi. Wakati mwingine vichomi kama chango husababisha maumivu makali ambayo huhitaji tiba ili kumsaidia mwanamke katika hali hiyo.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626,
Arusha-Mbauda.
Pia tunatoa masomo mazuri kabisa kila siku kwenye GROUP letu la mtandao wa TELEGRAM, hivyo unaweza ukatuma namba yako ya WHATSSAP tukakurushia link yetu ukajiunga na darasa.
Karibuni sana