Hakuna sababu ya kukufanya uache kufanya tendo la ndoa kwakuwa umeshapata ujauzito, isipokuwa tu kama utakuwa umepewa maelekezo na daktari wako. Mtoto wako anakuwa amelindwa vizuri majiamji ya amniotic ndani ya mfuko wako wa uzazi ambayo humzunguka mtoto. Hivyo tendo la ndoa au kufika kileleni mwanaume au mwanamke hakutaleta madhara kwa mtoto.
NUKUU: Daktari anaweza kupendekeza usifanye tendo la ndoa mapema upatapo ujauzito ikiwa kama uliwahi kuwa na tatizo la mimba kuharibika. Tendo la ndoa linaweza kuzuiliwa ikiwa kama una matatizo mbalimbali, kama vile kujifungua mtoto kabla muda haujakamilika au kutokwa na damu ukeni wakati wa ujauzito. Utahitaji kumuuliza daktari wako ili aweze kubaini endapo kama hutahitaji kuingiliana na mwanaume au kuwa na hamu ya tendo la ndoa, kadiri matatizo tofauti tofauti yatahitaji vizuizi mbalimbali.
Wasiliana Na Mwenza Wako Kuhusu Tendo La Ndoa
Umuhimu wa kutengeneza ukaribu na mwenza wako wakati wa ujauzito huwa ni kufunua hisia zako, hasa unapokuwa na msongo wa mawazo juu tendo la ndoa wakati wa ujauzito.
Mtie moyo mwenza wako ili aweze kuongea na wewe, hasa unapoona mabadiriko katika muitikio wa mke wako. Kuongea na mwenza wako kunaweza kuwasaidia wote wawili kutambua hisia na matumaini yenu.
Je, Hamu Ya Tendo La Ndoa Wakati Wa Ujauzito Inaweza Kubadirika?
Ni kawaida hamu yako ya tendo la ndoa kubadirika na kuwa tofauti unapokuwa mjamzito. Uonapo hivyo, tambua kuwa hiyo ni afya kamili. Kubadirika kwa homoni au vichocheo husababisha baadhi ya wanawake kuwa na hamu kubwa ya tendo la ndao wakati wa ujauzito. Lakini wengine wanaweza wasijihisi kufanya tendo la ndoa kama walivyokuwa kabla hawajapata ujauzito.
NUKUU: Wakati wa wiki 2, 3, 4-12 za ujauzito, baadhi ya wanawake hupoteza kabisa hisia au hamu ya kufanya tendo la ndoa kwakuwa hujihisi hali ya kuchoka na kutokuwa na raha kabisa. Wengine huendelea kuwa na hamu tu ya kufanya tendo la ndoa na kutamani kuwa na mwanaume muda wote. Na ndio maana baadhi yao hutamani hata kuwa na nguo ya mume wake karibu au kuivaa kwa mfano, shati au T-sheti,nk.
Je, Unawezaje Kufanya Tendo La Ndoa Kwa Furaha Zaidi Wakati Wa Ujauzito?
Kubadiri mitindo au style wakati wa kufanya tendo la ndoa, kunaweza kuwa kwa lazima kadiri ujauzito unavyozidi kuwa mkubwa. Hii itakufanya kuwa na raha unapokutana na mwenzi wako, na pia itakusaidia baada ya mtoto kuzaliwa.
NUKUU: Unaweza pia kuhisi uhitaji wa kutumia mafuta kupakaa eneo la uke wakati wa kufanya tendo la ndoa. Hupaswi kuhisi maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa. Wakati wa kupiga mshindo au kufika kileleni, mfuko wa uzazi hujikaza au kujibana. Ikiwa kama kutatokea mbanano wowote wenye kuleta maumivu, basi unapaswa uonane na daktari haraka. Pia acha kushiriki tendo la ndoa na ufike hospitali bila kuchelewa ikiwa kama unatokwa na damu ukeni au kama yanatoka majimaji. Hakuna kinachotakiwa kuingia ukeni baada ya majimaji kutoka.
NUKUU: Kama daktari kakuzuia kushiriki tendo la ndoa, au kama hujisikii hamu ya kufanya tendo la ndoa, basi kuwa na muda mzuri wa kuwa karibu na mwenza wako. Upendo unaweza kuonyeshwa kwa namna nyingi mbalimbali. Jikumbusheni wenyewe upendo uliowafanya mpaka kumkaamua kutengeneza mtoto wenu tumboni. Fuhieni muda wenu pamoja, huku mkijitahidi kutembea pamoja, kula pamoja, na kuoga pamoja. Ikiwezekana mwanaume umsaidie mkeo kazi za jikoni asubuhi au jioni utokapo kazini.
Baada Ya Kujifungua Mtoto, Je Mwanamke Unatakiwa Kufanya Tendo La Ndoa Muda Gani?
Unaweza kuanza kufanya tendo la ndoa unapokuwa umepona kabisa, na pale wewe na mwenzi wako mnajisikia amani na furaha tele.
NUKUU: Baada ya kujifungua, baadhi ya wanawake maeneo yao ya uke huwa makavu. Hivyo huhitaji vitu vya kupakaa ukeni ili kufanya eneo liwe laini wakati wa kushiriki tendo la ndoa ili kupunguza maumivu na ukavu ukeni.
Je, Mwanamke Anaweza Kupata Ujauzito Tena Wakati Anapokuwa Akinyonyesha?
Wanawake wanaonyonyesha huchelewa kupevusha mayai yao, na ndio maana vipindi vya hedhi huwa havionekani muda huo. Lakini upevushaji wa mayai huanza kabla hawajaanza kuona siku zao za hedhi tena. Kwahiyo kumbuka kwamba, mwanamke unaweza kuendelea kuwa mjamzito wakati wa kipindi cha kunyonyesha. Fuata maelekezo ya daktari wako katika kutumia njia sahihi ya mpangilio wa kushiriki tendo la ndoa na mwenza wako.
Nipende kuishia hapa mpendwa msomaji, nikukaribishe tu kwa maswali, karibu sana.
Je, unahitaji pia huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626.
Arusha-Mbauda.
Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATSSAP tukakupatia link yetu ili uweze kujiunga katika darasa letu la afya katika mtandao wa TELEGRAM.
Karibuni sana!