Uke na sura ya nje ya mashavu ya uke hutofautiana kwa asili katika umbo, rangi na saizi. Linapotokea jambo lolote linalohusiana na miili, jinsia pamoja na afya ya uzazi, watu wengi hushangaa, na kujiuliza wao wenyewe ikiwa kama kweli wapo kawaida? Jibu kuhusiana na uke ni kwamba kuna utofauti mkubwa katika sura ya uke, saizi pamoja na rangi.
Makala hii inaelezea aina mbalimbali za uke. Pia nitaelezea jinsi ya kuomuona daktari anayehusika na mambo ya uzazi.
Aina Za Uke
Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba uke hufanana umbo, lakini kwamba kuna tofauti nyingi katika urefu na upana wake.
Umbo Au Sura Ya Uke
Wakati watu wanapozungumzia uke, mara nyingi humaanisha kitu kinachoonekana, yaani sehemu ya nje ya jinsia. Lakini msemo halisi wa eneo hili huwa ni Vulva.
Vulva inaambatanisha maeneo mengi kama vile, mashavu ya uke ya nje(labia majora) pamoja na mashavu ya ndani ya uke(labia minora), au midomo ya ndani na ya nje ya uke. Hii ni mikunjo ya ngozi ambayo huzunguka mlango wa uke pamoja na njia ya mkojo. Kutegemeana na ukubwa na sura ya nje ya maeneo hayo, muonekano wa vulva unaweza kutofautiana kwa sehemu kubwa.
Ili kuzingatia aina hii, baadhi ya sifa za kawaida za uke ni kama ifuatavyo;
- Mashavu Ya Nje
Mashavu ya nje ya uke huwa ni marefu kwa baadhi ya wanawake. Mashavu yanaweza kuning’inia, na ngozi inaweza kuonekana kuwa nyembamba, au yanaweza kuwa manene na yenye kuvutika.
Mashavu ya nje ya uke huwa ni malaini na huwa hayajikusanyi sana kama yalivyo ya ndani. Baadhi ya wanawake wana mashavu ya nje ambayo huficha mashavu ya ndani kabisa pamoja na kisimi. Kwa wengine, mashavu ya nje yanaweza kupinda na kukutana mwishoni, huku yakifichua baadhi ya mashavu ya ndani kwa juu.
NUKUU: Kama mashavu ya nje yakiwa mafupi, hayawezi kukutana na yanaweza kuyafichua mashavu ya ndani kwa uwazi kabisa.
- Mashavu Ya Ndani
Ni kawaida kwa mashavu ya ndani kuonekana. naweza kuning’inia chini ya mashavu ya nje. Shavu moja la ndani linaweza kuwa refu kuliko jingine. Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa na mashavu mafupi ya ndani ambayo hufichwa na mashavu ya nje. Lakini kwa wanawake wengine, mashavu ya ndani huwa na urefu wenye kulingana. Kama mashavu ya nje na ya ndani ni madogo na yanakaribia kwenye mapaja, basi ki kofia kinachoficha kisimi, kinaweza kuonekana. Hizi ni tofauti katika sura, lakini uke wenye afya una sura nyingi zaidi pamoja na saizi.
Je, Ndani Ya Uke Panakuwaje?
Sehemu ya ndani ya uke huwa ni kama bomba refu lenye maeneo yaliyokunjamana ambayo yanaweza kutanuka na kusinyaa. Utafiti unaonyesha kwamba uke huwa ni mfinyu kuanzia kwenye malngo wake na huelekea kuwa mpana maeneo ya mlango wa uzazi. Hali hii hutengeneza umbo la “V”, ingawa upana unaweza kutofautiana.
Uke unaweza kuonekana kuwa mpana au kulegea kutokana na hali ya kujifungua watoto. Hii ni kwasababu tishu za uke hutanuka ili kutengeneza chumba kwa ajili ya mtoto kuweza kupita chini kwenye njia ya uzazi. Baada ya kujifungua, uke unaweza kurejea katika hali yake ya mwanzo au unaweza ukabaki kuwa mpana tu.
- Saizi Ya Uke
Uke unaweza ukabadirika katika saizi, au urefu unapoingiza kidole au uume, kwa mfano. Hufanya hivyo kwa kunyooka na kutanuka. Hali hii pia hukipeleka juu kizazi na mlango wa kizazi.
Urefu wa uke hutofautiana, lakini urefu wa kati, huwa chini ya inchi 4 hivi, pale mwanamke anapokuwa hana nyege au hisia ya tendo la ndoa. Hata hivyo, urefu unaweza kutofautiana kati ya inchi 2.5 hadi 5 au zaidi kutoka kwa mwanamke mwingine kwenda kwa mwingine.
NUKUU: Utafiti unaonyesha kwamba, kwa baadhi ya kesi, waliweza kubaini tofauti katika urefu na umri wa mwanamke, lakini sio uzito. Kwa mfano, mwanamke mrefu anaweza kuwa na uke mrefu.
- Rangi Ya Uke Kwa Ndani
Rangi za ngozi kwa asili hutofautiana, ikiwa pamoja na ngozi ya uke. Madaktari watafiti wanatoa taarifa za rangi ya uke kama ifuatavyo;
- Zambarau
- Pinki
- Nyekundu
Rangi pia zinaweza kutofautiana, inategemeana na mtiririko wa damu. Wakati hisia au nyege zinapopanda, mtiririko wa damu huongezeka, na uke unaweza kuonekana wenye rangi ya Zambarau.
Baadhi ya wanawake hukariri mabadiriko ya rangi wakati wanapotumia matibabu fulani ya madawa. Maambukizi ya fangasi kwa mfano, yanaweza kusababisha uke kuonekana mwekundu.
Je, Tofauti Zingine Zinakuwaje?
Mambo yafuatayo yanaweza pia kuvutia muonekano au harufu ya uke, na hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke kwa asili kabisa;
- Nywele
Mavuzi yanaweza kusaidia kulinda uke usipatwe na magonjwa yatokanayo na bakteria. Mavuzi yanaweza pia kuwa ishara ya asili kabisa kuwa kizazi kimekomaa. Kiwango, au rangi na muonekano wa mavuzi hutofautiana kati ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Mavuzi yanayokua mapema kabla ya kufikisha umri wa miaka 8, na kiwango cha mavuzi mengi sana yanaweza kuashiria vihatarishi vya tatizo la vivimbe vingi vidogo vidogo kwenye vifuko vya mayai(polycystic ovary syndrome). Mavuzi huonekana kupungua kadiri mwanamke anavyozidi kuongezeka umri, kutokana na mabadiriko ya homoni.
- Ute (Discharge)
Uchafu utokao ukeni husaidia kuziweka tishu za uke katika afya nzuri. Baadhi ya wanawake hutumia rangi za utoko au ute unaotoka ukeni ili kufuatilia uzazi wao. Kwa mfano, ute unaovutika unaweza kuonekana wakati wa yai kupevuka. Mabadiriko katika ute unaotoka ukeni yanaweza kuonyesha maambukizi, ambayo huhitaji tahadhari ya matibabu. Fika hospitali ikiwa kama ute ni wa kijani, kijivu, au wenye harufu mbaya.
NUKUU: Mwanamke anaweza kurekebisha mtiririko wa damu kwa kutumia madawa ya kurekebisha homoni kama vile, vidonge vya uzazi wa mpango. Mwanamke yeyote ambaye mtiririko wa damu ya hedhi mara nyingi pedi zake hulowana sana au kumfanya ajihisi kuwa na kizunguzungu au kushindwa kupumua vizuri, anapaswa afike hospiatali haraka sana. Mwanamke anaweza kupata hedhi ambayo inaweza kuharibu kabisa kazi zake za kila siku.
- Harufu Ya Uke
Kwa asili uke huwa una bakteria na fangasi ambao wanaweza kusababisha harufu. Harufu inaweza kutofautiana kwani inaweza kuwa ya kawaida au mbaya kabisa. Mzunguko wa hedhi wa mwanamke, afya yake kwa ujumla, harufu ya asili ya uke vyote vinaweza kuharibu harufu ya uke. Harufu mbaya ukeni ni ishara tosha kabisa kuwa tayari kuna maambukizi.
Je, Unapaswa Ufike Hospitali Muda Gani?
Yeyote mwenye tatizo la uke anapaswa afike hospitali na kuonana na daktari wa magonjwa ya uzazi. Baadhi ya dalili unazoweza kuziona ni pamoja na:
- Ute usio wa kawaida
- Harufu isiyo ya kawaida
- Badiriko la rangi katika tishu za mashavu ya uke
- Kutokwa na damu nyingi ya hedhi
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hii: 0752 389 252 au 0712 181 626.
Arusha-Mbauda
Pia tunatoa huduma ya masomo ya afya kwa njia ya matandao wa WHTWSSAP na TELEGRAM. Hivyo unaweza kutuma namba yako ukaunganishwa na DARASA letu bure.
Karibuni sana
You are highly welcomed
Be, blessed
Thanks
Sorry Niko nashida nyingine tofauti sijui mwaweza nisaidia nasumbuliwa nakuvimba navidonda naukavu katika kooo Nisha tumia dawa nyingi hospitality sijapona sijui shida Nini mpaka Sasa
Asante kwa Elimu
NINATATIZO LA NJIA YA UKE KUBANA SANA HADI UBOO HAUINGII WOTE,NA NIKILAZIMISHA MAUMIVU YANATOKEA
NINAWATOTO2 NIMEZAA KWA OPERATION
Je, una umri gani dada