JE, YAWEZA KUWA MIGUU KUWAKA MOTO NI DALILI ZA UGONJWA?

Hali ya miguu kuwaka moto huwa ni hisia zinazojitokeza miguuni mwako pale inapouma kwa kati tu au zaidi. Wakati mwingine maumivu ya miguu kuwaka moto yanaweza kuwa makali sana kiasi kwamba yakakunyima raha na kukukosesha usingizi usiku. Kwa hali hiyo basi, maumivu ya miguu kuwaka moto yanaweza pia kuambatana na hali kama ya kuchomwa chomwa sindano au miguu yote kufa ganzi kabisa.

Je, Nini Husababisha Miguu Kuwaka Moto?

 

Ijapokuwa hali ya uchovu wa mwili au maambukizi ya ngozi yanaweza kusababisha miguu kuwaka moto au kuvimba, hali ya kuwaka moto mara nyingi inaonekana  kuwa dalili za kuharibika kwa mishipa ya fahamu. Kuharibika kwa mishipa ya fahamu huwa kuna visababishi vingi mbalimbali kama vile:

  • Kisukari
  • Matumizi ya pombe ya muda mrefu
  • Mwili kujaa sumu
  • Maambukizi ya ukimwi au HIV
  • Magonjwa sugu ya figo
  • Kupungukiwa na vitamini B au virutubishi vinavyozarisha chembe za damu mwilini

Hisia za hali ya miguu kuwaka moto huja ghafla, hasa unapokuwa umeingiliwa na sumu au kemikali mwilini mwako. Kidonda mguuni mwako huonekana kuathiriwa hasa unapokuwa na tatizo la kisukari.

Je, Kuharibika Kwa Mishipa Ya Fahamu Hutokana Na Nini?

Hali ya kuharibika kwa mishipa ya fahamu inaweza ikatokea endapo kama una ugonjwa wa kisukari.  Kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu(glucose) kinaweza kuharibu mishipa ya fahamu katika mwili wako wote. Sukari inapoongezeka na kuwa nyingi kwenye damu mara nyingi inaweza kuharibu mishipa ya fahamu hasa kwenye miguu yako.

Kutokana na athari za mishipa ya fahamu, dalili zinaweza kuwa miguu kufa ganzi na kuuma na kupelekea matatizo ya umeng’enyaji chakula tumboni, njia ya mkojo, mishipa ya damu pamoja na moyo. Baadhi ya watu huwa wana dalili za kawaida. Lakini wengine wanapokuwa na tatizo la mishipa ya fahamu huharibika kutokana na ugonjwa wa kisukari, wanaweza kupatwa na maumivu makali kwenye miguu.

NUKUU: Kuharibika kwa mishipa ya fahamu kutokana na kuongezeka kwa sukari mara nyingi huwa ni tatizo la kawaida la kisukari. Lakini unaweza ukazuia tatizo la kisukari kwa kutumia tiba na kubadiri tabia au mienendo ya ulaji wa vyakula katika maisha yako.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Zipo aina nne za ganzi ya kisukari. Unaweza ukawa na aina moja au zaidi ya ganzi au miguu kuwaka moto. Dalili zake zitategemeana na aina uliyo nayo na ni mishipa gani ya fahamu iliyo athirika. Kwa kawaida, dalili hukua kwa taratibu. Unaweza usione kitu chochote kibaya mapaka pale hali ya kuharibika kwa mishipa ya fahamu itakapoonekana.

  1. Peripheral Neuropathy

 

Hii ni aina ya kawaida kabisa ya tatizo la miguu unapokuwa na kisukari. Huathiri miguu kwanza, na hufuatia mikono. Dalili za tatizo hili mara nyingi huwa ni mbaya zaidi nyakati za usiku, nazo zinaweza kuwa kama ifuatavyo:

  • Badiriko la joto mwilini au ganzi au kupungua kwa uwezo wa kuhisi ganzi
  • Kuhisi miguu kuwaka moto
  • Maumivu makali
  • Kuhisi maumivu unaposhika kitu hata kama unaondoa shuka kitandani
  • Misuli kulegea
  • Viwiko vya mikono kukakamaa
  • Mwili kulegea
  • Matatizo ya miguu kama vile vidonda, maambukizi ya fangasi, pamoja na maumivu ya mifupa au jointi.

 

  1. Mfumo Wa Fahamu

 

Mfumo wa fahamu huongoza moyo wako, kibofu cha mkojo, tumbo la chakula, utumbo mkubwa na mdogo, viungo vya uzazi pamoja na macho. Ugonjwa wa kisukari unaweza kuathiri neva za fahamu katika haya maeneo niliyoyataja, na hivyo kusababisha mambo yafuatayo:

  • Kukosa choo, au kuhisi kuharisha
  • Kuishiwa nguvu za kiume
  • Uke kuwa mkavu
  • Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa au kupoteza hisia kabisa
  • Kushindwa kumeza chakula
  • Kuongezeka au kupungua kwa joto
  • Matatizo katika kuongoza joto mwilini
  • Mabadiriko kwenye macho kutokana na hali ya mwanga au giza
  • Kuongezeka kwa mapigo ya moyo ukiwa umepumzika
  • Mchafuko wa tumbo, hali ambayo husababisha kichefuchefu, kutapika, tumbo kuunguruma au kukosa hamu ya kula.
  • Matone makali kwenye shinikizo la damu baada ya kukaa au kusimama ambayo yanaweza kupelekea wewe kuhizi kizunguzungu au kuzimia
  • Kukosa ufahamu kutambua kuwa viwango vya sukari kwenye damu viko chini
  • Matatizo ya kibofu cha mkojo, hasa maambukizi katika njia ya mkojo(UTI)

 

  • Kufa Ganzi Kwa Neva

Matatizo ya kufa ganzi huathiri sana neva kwenye mapaja, nyonga, matakoni au miguuni. Hali hii huwatokea sana wagonjwa wenye Kisukari aina ya pili pamoja na watu wazee. Majina mengine kwa ajili ya ugonjwa huu ni, “Diabetic Amyotrophy”, Femoral Neuropathy au Proximal Neuropathy.

Dalili zake mara nyingi huwa upande mmoja wa mwili, lakini wakati mwingine zinaweza kusambaa katika maeneo mengine. Unaweza ukapatwa na;

  • Maumivu makali sehemu za nyonga au mapajani au matakano ambayo yanaweza kudumu kwa muda wa siku moja au zaidi
  • Kusinya kwa misuli ya mapajani
  • Kushindwa kuinuka pindi unapokuwa umekaa
  • Tumbo la chini kuvimba ikiwa kama limeathiriwa
  • Kupoteza uzito

NUKUU: Watu wengi hupona kwa muda tu, ingawa dalili zinaweza kuwa mbaya zaidi kabla hawajapata nafuu.

  1. Kuharibika Kwa Neva Za Fahamu Nje Ya Ubongo Na Uti Wa Mgongo(Mononeuropathy)

 

Hali hii hutokea pale mishipa ya fahamu inapoharibika maeneo ya nje ya ubongo hasa usoni, uti wa mgongo au miguuni. Hali hii huwatokea sana watu wenye umri mkubwa.

Ni hali ambayo hujitokeza ghafla na inaweza kusababisha maumivu makali sana. Hata hivyo, mara nyingi huwa haisababishi matatizo ya muda mrefu mno.  Kwa kawaida dalili zake huashiria kutoweka kwa wiki au miezi kadhaa bila kutumia tiba. Dalili zako zinategemea na mishipa iliyoharibika. Unaweza ukapatwa maumivu maeneo ya;

  • Miguu au nyayo
  • Kiunoni au nyonga
  • Mbele ya mapaja
  • Kifuani au tumbo la chini

Kuharibika kwa neva za fahamu nje ya ubongo(Mononeuropathy)kunaweza pia kusababisha matatizo ya neva kwenye macho na usoni, hali ambayo hupelekea;

  • Kushindwa kuona vizuri
  • Kuona maluweluwe
  • Kuhisi maumivu upande wa jicho moja
  • Kupooza upande mmoja wa uso wako

NUKUU: Wakati mwingine hali hii hujitokeza wakati kitu kikiwa kimekandamiza neva ya fahamu. Hali hiyo inaweza kusababisha kufa ganzi au mkono au vidole kuuma, isipokuwa kidole kidogo cha mwisho. Mkono unaweza kuishiwa nguvu, na unaweza ukadondosha vitu chini.

Je, Ni Muda Gani Inapaswa Ufike Hospitali Na Kumuona Daktari?

 

Ndugu mpendwa msomaji napenda kukusahuri kwamba, fika hospitali ikiwa kama utaona dalili kama hizi:

  • Kidonda mguuni kisichopona
  • Mikono au miguu kuuma, kuwaka moto au maumivu kutokana na kazi zako
  • Mabadiriko kwenye umeng’enyaji wa chakula
  • Mabadiriko kwenye kukojoa au tendo la ndoa
  • Kuhisi kizunguzungu.

Dalili hizi mara nyingi huwa hazimaanishi kuwa una tatizo la kuharibika kwa mishipa ya fahamu. Bali zinaweza kuwa ishara za matatizo mengine yanayohitaji kutibiwa. Vipimo na matibabu yanayofanyika mapema vinaweza kusaidia afya yako katika tatizo la kisukari na kuzuia matatizo mengine yasikupate.

Je, Visababishi Vyake Ni Nini?

Uharibifu Kwenye Neva Za Fahamu Pamoja Na Mishipa Ya Damu.

 

Hali hii huonyesha kutofautiana katika kila aina ya kufa ganzi kwa mishipa ya fahamu. Watafiti wanadhani kuwa muda wote, huenda kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kisichodhibitiwa huharibu mishipa ya fahamu na huingiliana na uwezo wa kutuma ishara, kupelekea kufa ganzi kwa mishipa ya fahamu kutokana na kisukari. Kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu pia hudhoofisha kuta za mishipa midogo ya damu ambayo huzipatia neva za fahamu hewa safi ya oksijeni na virutubishi.

Je, Nini Vihatarishi Vyake?

Mtu yeyote mwenye kisukari anaweza kuwa na tatizo la mwili kufa ganzi, lakini vihatarishi hivi humfanya muhisika kupatwa na maharibifu makubwa ya mishipa ya fahamu.

  1. Udhibiti Duni Wa Sukari Ya Damu

 

Sukari ya damu isiyodhibitiwa humuweka muhusika katika hatari yakila madhara ya kisukari, ikiwa pamoja na kuharibika kwa mishipa ya fahamu.

 

  1. Ugonjwa Wa Figo

 

Ugonjwa wa kisukari unaweza kuharibu figo zako. Uharibifu wa figo hupeleka sumu kwenye damu, hali inayoweza kusababisha mishipa ya fahamu kuharibika.

  1. Uvutaji Sigara

 

Uvutaji sigara husababisha mishipa ya ateri kuwa mifinyu tena migumu, na hupunguza mbubujiko wa damu kwenda miguuni mwako. Hali hii hupelekea vidonda kushindwa kupona kwa urahisi na hivyo huharibu mishipa ya neva.

Je, Ni Madhara Gani Anayoyapa Mgonjwa Wa Kisukari?

 

Kuharibika kwa mfumo wa fahamu kutokana na ugonjwa wa kisukari kunaweza kusababisha madhara mengi mbalimbali ikiwa pamoja na mambo haya yafuatayo:

 

  1. Kukatwa Kidole Gumba Au Mguu

 

Kuharibika kwa mishipa ya fahamu humfanya muhusika kukosa hisia kwenye miguu yake. Nyayo za miguu na vidonda vinaweza kuathiriwa vibaya kabisa au kubadirika na kuwa na vidonda. Kwa namna hiyo basi, athari zinaweza kuenea mpaka kwenye mifupa, na vidonda vinaweza kusababisha kuharibika kwa tishu. Ile hali ya kukatwa kwa kidole gumba au hata mguu inaweza kuwa jambo la lazima kabisa.

  1. Kuharibika Kwa Viungo Vya Mifupa

 

Uharibifu wa neva unaweza kusababisha jointi kupooza, na kusababisha hali ambayo kitaalamu tunaita, “Charcot joint.” Hali hii hujitokeza kwenye viunganishi vidogo vya mifupa vya kwenye miguu. Dalili ikiwa pamoja na jointi kufa ganzi na kuvimba, na wakati mwingine jointi kuharibika. Matibabu ya haraka yanaweza kukusaidia kuponya na kuzuia uharibifu mwingine wa jointi zako.

 

  1. Maambukizi Katika Njia Ya Mkojo(UTI) Na Mkojo Kutoka Bila Kujua

 

Kama mishipa ya fahamu inayodhibiti kibofu chako cha mkojo ikiharibika, unaweza kushindwa kukojoa na kumaliza mkojo kwenye kibofu chako. Bakteria wanaweza kukusanyikana kwenye kibofu cha mkojo na figo, na kusababisha maambukizi katika njia ya mkojo yaani UTI. Kuharibika kwa neva kunaweza pia kuathiri uwezo wako wa kuhisi ni muda gani unahitaji kukojoa au kudhibiti misuli inayoachilia mkojo, na kupelekea mkojo kutoka bila kujua.

  1. Kutojua Mapungufu Ya Glukozi Kwenye Mkondo Wa Damu(Hypoglycemia)

 

Sukari ya damu ya chini(chini ya miligramu 70 kwa deciliter), kwa kawaida husababisha mwili kutikisika, kutoa jasho sana na mapigo ya moyo kwenda mbio. Lakini ikiwa kama una ugonjwa wa neva wenye kujiendesha wenyewe, unaweza usione ishara hizo.

  1. Matone Makali Katika Shinikizo La Damu

 

Uharibifu katika neva zinazodhibiti mbubujiko wa damu unaweza kuathiri uwezo wako wa mwili kurekebisha shinikizo la damu. Hali hii inaweza kusababisha matone makali kwenye shinikizo unaposimama baada ya kuinuka, hali ambayo inaweza kupelekea kizunguzungu na kupepesuka.

  1. Matatizo Ya Usagaji Chakula

 

Kama uharibifu wa neva ukipata njia katika tumbo la usagaji chakula, basi unaweza ukapata hali ya kukosa choo au kuharisha. Matatizo ya neva yatokanayo na ugonjwa wa kisukari yanaweza kupelekea kuharibika kwa mwendo ndani ya utumbo, hali ambayo tumbo hutoa uchafu nje pole pole kabisa au likashindwa kutoa kabisa uchafu.

NUKUU: Hii hali inaweza kuingiliana na usagaji chakula na kuathiri kabisa viwango vya sukari ya damu pamoja na virutubishi. Ishara na dalili ni pamoja na kichefuchefu, na kutapika na tumbo kuunguruma.

 

  1. Kukosa Hisia Ya Tendo La Ndoa

 

Kuharibika kwa neva mara nyingi huharibu neva zinazodhibiti viungo vya uzazi. Wanaume wanaweza wakapatwa na hali ya kutokudindisha. Wanawake wanaweza kukosa kabisa hisia au hamu ya tendo la ndoa na uke kuwa mkavu kutokana na kukosa uteute.

  1. Jasho Kuongezeka Au Kupungua

 

Kuharibika kwa neva kunaweza kuvuruga jinsi tezi zako za jasho zinavyofanya kazi na kuufanya mwili wako kushindwa kudhibiti joto lake kwa ufasaha. Baadhi ya watu wenye tatizo hili hupatwa na jasho jingi hasa mida ya usiku au wanapokula chakula. Kutokwa na jasho kidogo sana au kutokuona jasho kabisa hata kidogo inaweza kuwa ni tishio katika maisha yako.

 

Nipende kuishia hapa mpendwa msomaji. Tunakukaribisha katika Group letu la WHATSSAP au TELEGRAM ili uweze kujifunza zaidi na kuweza kupata huduma. Tuma namba yako ya WHATSSAP ili uunganishwe na GROUP letu.

 

Je, unahitaji huduma yetu? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

 

Arusha-Mbauda.

 

Karibuni sana

 

14 thoughts on “JE, YAWEZA KUWA MIGUU KUWAKA MOTO NI DALILI ZA UGONJWA?

  1. Nashukuru Sana Sana Nimeelewa, maana miguu imekuwa ikiwaka moto sana na ganzi na wakati mwingine vidole kukakamaa.
    Dawa zake ni Nini
    0784301710

    1. Pole sana, dawa zake zipo utapata maelezo ukishauliza kwenye group letu la whatsap, tayari tumeshakuunganisha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *