Je, Nini Maana Ya Mlango Wa Uzazi?
Mlango wa uzazi ni njia inayokuwa katikati ya uke na mfuko wa uzazi. Ni sehemu ya chini ya mfuko wako wa uzazi iliyopo juu ya uke wako na huwa ina muonekano wa umbo kama donati. Uwazi unaokuwa katikati ya mlango wa kizazi tunaita shingo ya kizazi.
Mlango wa uzazi hufanya kazi kama mlinzi wa lango, huongoza kile kinachoruhusiwa kuingia na kutokuingia kwenye mlango wa uzazi.
NUKUU: Unapokuwa mjamzito, mlango wako wa uzazi huzarisha uteute unaojulikana kama utoko. Wakati wa mwezi wa ujauzito, shingo yako ya uzazi huzarisha ute mzito ambao hufunika mlango wa uzazi, na kuzifanya mbegu za mwanaume kushindwa kupita na kuingia kwenye mfuko wa uzazi.
Unapopevusha yai lako, hata hivyo, shingo yako ya uzazi huzarisha uteute mwepesi wenye kuteleza. Shingo yako ya uzazi pia inaweza kuwa laini au ikabadiri eneo lake, na mlango wa uzazi unaweza kufunguka taratibu. Hii yote huwa ni juhudi inayofanyika ili kurahisisha mbegu za mwanaume ziweze kuingia kwenye mfuko wa uzazi.
Kabla siku za hedhi hazijaanza, mlango wa uzazi unaweza kuwa mgumu au ukabadiri nafasi. Mlango wa uzazi unaweza kuwa mfinyu ukajiandaa kujifunga katika tukio la ujauzito. Kama hakuna ujauzito, mlango wa uzazi utatulia na shingo ya uzazi itafunguka ili kuruhusu ukuta laini wa mfuko wa uzazi kutoa mwili wako kupitia uke wako.
Mlango wa uzazi uliojifunga wakati mwingine unaweza kutokea kwa muda wakati kipindi cha mzunguko wa hedhi. Wakati mwingine, mlango wa uzazi unaweza kuonekana kujifunga mara kwa mara. Hii hufahamika kama kuziba kwa mlango wa uzazi. Ni hali inayotokea pale shingo ya uzazi inapokuwa finyu au ikawa imeziba kabisa. Baadhi ya wanawake huzariwa wakiwa na tatizo la kuziba kwa mlango wa uzazi, lakini wengine hali hii huwapata baadaye katika umri wao.
Je, Dalili Zake Zikoje?
Kutegemeana na umri wako na kama unajaribu kuwa na ujauzito lakini unashindwa, huwezi ukaona dalili zozote zinazoonyesha kuwa mlango wa kizazi umefunga.
Kama hujafikia muda wa kukoma hedhi, unaweza ukaona vipindi vyako vya hedhi vinabadirika badirika au kuwa unahisi maumivu makali wakati wa hedhi. Mlango wa uzazi ulioziba unaweza pia kusababisha ugumba kwasababu mbegu au shahawa za mwanaume haziwezi kusafiri na kuingia ndani ya mfuko wa uzazi(uterus) ili kurutubisha yai la mwanamke.
NUKUU: Kama tayari umefikia umri wa kukoma hedhi, basi unaweza usione dalili zozote. Lakini madhara yanaweza kusababisha tumbo la chini kuuma. Unaweza kujisikia pia kama una uvimbe kwenye maeneo yako ya nyonga.
Je, Nini Husababisha Mlango Wa Uzazi Kufunga?
Unapozaliwa huku mlango wako wa uzazi ukiwa umefunga, basi inaweza kusababishwa na kitu kingine. Visababishi halisi ni kama hivi vifuatavyo:
- Upasuaji wa mfuko wa uzazi
- Matibabu ya shingo ya uzazi hasa pale inapokuwa na tatizo la saratani
- Saratani ya shingo ya kizazi
- Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
- Matibabu ya mionzi
- Michubuko kwenye mlango wa uzazi
Je, Mlango Wa Uzazi Uliojifunga Unapimwaje Ili Kuweza Kubaini?
Ili kupima mlango wa uzazi uliojifunga, daktari atahitaji kuchunguza maeneo ya nyonga kwa kutumia kifaa kinachoitwa speculum. Watakiingiza kifaa hiki ukeni mwako, ili kiweze kuwasaidia waweze kuona mlango wako wa uzazi. Watapima kwa uangalifu ukubwa wake, rangi yake, na umbo lake. Wanaweza pia kuchunguza na kutafuta kila uvimbe maji au dalili zingine za kitu chochote kisichokuwa cha kawaida.
Kama shingo yako ya uzazi itaonekana kuwa finyu au vinginevyo ikaonekana kuwa sio ya kawaida, basi madaktari wanaweza kujaribu kupitisha kifaa cha kupimia kina cha kidonda kwenye mlango wa kizazi. Kama wakishindwa, unaweza kupata kipimo cha kunga kwa mlango wa uzazi.
Je, Mlango Wa Uzazi Ulioziba Unaweza Kusababisha Madhara?
Kuwa na mlango wa uzazi ulioziba kunaweza kusababisha madhara mbalimbali kama haya yafuatayo:
- Ugumba au kutokushika ujauzito
- Vipindi vya hedhi kubadirika badirika
- Mkusanyiko wa majimaji kwenye mfuko wa uzazi au mirija ya uzazi.
NUKUU: Kufunga kwa mlango wa uzazi kunaweza pia kusababisha maumivu makali ya tumbo la chini, hali ambayo hutokea pale damu ya hedhi inapokusanyika kwenye tumbo lako la uzazi. Hii hali inaweza kusababisha ngozi laini za ukutwa wa mfuko wa uzazi kutuna, hali ambayo pia hupelekea tishu za mfuko wa uzazi kuvimba ndani na nje ya mfuko wa uzazi.
Kufunga kwa mlango wa uzazi kunaweza pia kutokea katika hali inayoitwa pyometra. Pyometra huwa ni mkusanyiko wa usaha ndani ya mfuko wa uzazi. Kama hali hii ikitokea, utajisikia maumivu makali sana katika maeneo ya tumbo lako la chini.
Nashukuru sana wapendwa wasomaji, naomba niishie hapa katika makala yetu hii ya leo. Nakaribisha maswali kwa kila mmoja, pia kama una maoni unaweza ukatuma ujumbe wako katika website yetu.
Je, Unahitaji huduma ili kuondoa tatizo hili? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia tunakukaribisha katika JUKWAA au GROUP letu la TELEGRAM au WHATSAP. Unaweza kutuma namba zako za telegram au whatsap ili uweze kuunganishwa na GROUP zetu uweze kujifunza zaidi.
Kama unahitji kujiunga TELEGRAM kupitia link yetu, basi unaweza kubonyeza hapa: t.me/jamesherbalclinic.
Kama unataka kuingi Jukwaa letu la Whatssap, basi bonyeza link yetu hii: https://chat.whatsapp.com/GqOmKZB5aZIJdIlH9gj4tY
Karibuni sana sana.