Katika wanawake 10 walio katika umri wa kuzaa, wanapopimwa, basi 1 anaweza kuonekana na tatizo la mvurugiko wa homoni.
Mvurugiko wa homoni ni hali ambayo husababisha vivimbe maji vidogo vidogo kwenye vifuko vya mayai. Japokuwa vivimbe maji vyenyewe havina madhara sana, lakini mvurugiko wa homoni unaweza kusababisha ugumba kabisa na kuongeza vihatarishi vya mwanamke kupatwa na maradhi ya saratani ya kizazi, kisukari Pamoja na ugonjwa wa moyo.
Je, Nini Maana Ya Vivimbe Maji?
Vivimbe maji maana yake ni vifuko vingivingi vyenye majimaji. Pale homoni ya estrogen, progesterone Pamoja androgen zinapokuwa kwenye uwiano sawa, hupeleka ishara kwenye vifuko vya mayai ili kuachilia yai. Vivimbe maji katika hali hii, huwa ni mayai ambayo hayakuachiliwa yakatoka kwenye kifuko cha mayai kwasababu ya homoni kutokuwa na uwiano sawa.
Wakati homoni hizi zinapokuwa hazina uwiano sawa, basi vifuko vya mayai hushindwa kupokea taarifa sahihi. Yai linaweza kushindwa kuachiliwa kwa kila mwezi, au linaweza lisiachiliwe kabisa hata kidogo.
Badala yake, kifuko kilichojaa majimaji(follicle) kilicho na yai, hubaki likiwa kubwa kwenye kifuko cha yai. Baadaye, vifuko vya mayai hujaa vivimbe vingi vidogovidogo. Hali hii inaweza kupelekea kupatwa na dalili kama vile vipindi vya hedhi kubadirika, chunusi, kuota nywele nyingi kila mahali, uzito kuongezeka, nk.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kwasababu wanawake wengi hawafahamu kuwa wana tatizo la mvurugiko wa hedhi, ni vyema kuzifahamu dalili, nazo huwa kama hizi zifuatazo:
- Vipindi vya hedhi kubadirika:
Wanawake wenye vivimbe maji vingi wanaweza wasione hedhi, vipindi vya hedhi kubadirika au kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu sana. Vipindi vya hedhi kubadirika inaweza kuwa ishara kwamba vifuko vya mayai haviachilii yai kila mwezi.
- Chunusi:
Kutokwa na chunusi nyingi ukubwani ni ishara kwamba homoni zako zimevurugika.
- Kuota nywele:
Nywele huota mahali ambapo hapapaswi kuwa na nywele kama vile kwenye kidevu, mgongoni, au kifuani. Aina hii ya kuota nywele inaweza kumaanisha kwamba tayari kinazarishwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume.
- Vivimbe Maji Vingi:
Wanawake wenye mvurugiko wa homoni wanakuwa na vivimbe maji vingi sana kwenye vifuko vyao vya mayai. Kwa kawaida vivimbe maji huonekana kwa kutumia kipimo cha ultrasound.
- Nywele kuisha:
Kuisha kwa nywele kichwa ni ishara kwamba mwanamke ana kiwango kikubwa cha homoni za kiume.
- Uzito wa mwili kuongezeka:
Wanawake wenye mvurugiko wa homoni mara nyingi huwa hawapungui uzito. Hivyo wanahitaji sana kubadiri milo yao au matibabu ili kupunguza uzito.
- Ugumba:
Hali ya mvurugiko wa homoni ni chanzo cha ugumba kwa mwanamke. Wanawake wenye tatizo la mvurugiko wa homoni wanaweza kuwa na shida ya kupata mimba kwasababu wanapevusha mayai yao kwa vipindi vinavyobadirikabadirika au muda mwingine wanaweza wasipevushe kabisa. Kwasababu hii, muda wa kulenga siku za hatari kwake inaweza kuwa ni shida tu. Kwahiyo anahitaji tiba kabisa.
- Uchovu:
Wanawake wenye tatizo la mvurugiko wa homoni hupatwa na hali ya kutokupata usingizi kabisa, hali ambayo husababisha kukosa pumuzi na kuanza kujirudia mida ya usiku. Licha ya Kwenda kulala mapema na kutumia muda wa masaa 8 akiwa usingizini, lakini bado ataamka akiwa amechoka tu, na kusababisha kujisikia uchovu mwingi siku nzima.
- Kutokwa na jasho:
Kwasababu ya mvurugiko wa homoni, wanawake wenye vivimbe maji vingi pia wana vihatarishi vingi vya msongo wa mawazo, mashaka na hali ya mwili kubadirika kwa kiwango kikubwa.
- Kupata hedhi yenye maumivu makali sana:
Vivimbe maji vingi vinaweza kusababisha maumivu makali sana wakati wa hedhi na kufanya damu itoke kwa wingi sana. Hali hii inaweza kuongeza matatizo mengine kama vile, kupungukiwa damu mwilini, na mara nyingi huwa sio nzuri na inaweza ikawa ya kutisha kweli.
Hivyo ndivyo tatizo la mvurugiko linavyokuja na lina madhara makubwa ikiwa kama hutojali kufanya matibabu mapema. Uonapo dalili kama hizo, basi wahi haraka sana kafanye vipimo.
Nipende kuishia hapa ndugu msomaji nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uunganishwe na darasa letu la Afya kwa njia ya WHATSAP.
Je, Unahitaji Hududuma? Basi wasiliana nasi kwamba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda, Maua,
Karibu sana!