Epuka Kabisa Ulaji Wa Vyakula Hivi, Ili Ujilinde Na Magonjwa!

Ni kweli kwamba watu wengi tunapenda kununua vyakula kutoka “supermaket” kutokana na ubora wa bidhaa zake na wakati mwingine hata unafuu wa bei. Lakini ni vyema kujua pia kuwa siyo vyakula vyote vilivyomo humo ni vizuri kiafya.

Katika makala ya leo, nakuletea orodha ya baadhi ya vyakula maarufu vinavyopatikana kwenye ‘supermarket’, restaurant, na maduka mengine ya bidhaa za vyakula, ambavyo hununuliwa na watu wengi bila kujua madhara yanayowakabili kwa kutumia vyakula hivyo mara kwa mara.

  1. Nyanya Za Kopo (Tomato Sauce)

Nyanya kama ilivyo katika uasili wake, haina madhara, lakini namna inavyohifadhiwa ndiko kunakoiharibu na kuifanya kuwa na madhara kwa afya yako. Ili iweze kukaa kwa muda mrefu, ni lazima iwekewe kemikali na kopo la kuhifadhiwa nalo, lazima liwekewe kemikali za kulifanya lisipate kutu.

Diamond Platnumz - Ukifika dukani usiseme unataka tomato sema unataka REDGOLD TOMATO SAUCE!!! Ndio habari ya mujini 󾥫󾥶󾁕󾥧 | Facebook

Vitu hivyo havibaki kwenye kopo wakati wa kuitoa nyanya, bali hutoka pamoja na nyanya na mwisho huingia jikoni na kuliwa. Hivyo basi, nyanya ya kopo inaharibika na kuwa hatari kwa afya yako kutokana na kuwekewa kemikali za kuhifadhia. Katika mazingira ya kitanzania ambapo nyanya halisi zipo nyingi hadi zinaoza, huna sababu ya kula nyanya za kopo na uache nyanya halisi zinazouzwa masokoni kila mahali.

  1. Nyama Za Kopo

Nyama za kopo (beef) nayo inaingia kwenye orodha ya vyakula hatari vya supermaket kutokana na kuwekewa kemilaki na chumvi nyingi ili kuifanya ikae kwa muda mrefu bila kuharibika. Ukiacha dosari hiyo, nyama nyingi za makopo, hutokana na ng’ombe wa kufugwa ambao huishi kwa kulishwa nafaka badala ya nyasi na hulishwa madawa mbalimbali ambayo huhatarisha afya ya mlaji.

Beef Corned Tin Stock Illustrations – 65 Beef Corned Tin Stock Illustrations, Vectors & Clipart - Dreamstime

Nyama bora na yenye kukidhi faida za kiafya ni ile inayotokana na ng’ombe wanaofugwa katika mazingira ya kula nyasi na mimea asilia (organic farming). Kwa mazingira ya kitanzania, huna sababu ya kununua nyama za kopo wakati nyama ipo nyingi buchani. Pia elewa kwamba hata katika nchi zilizoendelea, hivi sasa zinapiga vita ulaji wa nyama za makopo na badala yake zinahimiza ulaji wa nyama ‘fresh’ na wanaofugwa kiasili.

  1. Viazi, Maziwa, Na Samaki

Imebainika kuwa kuna ‘viazi ulaya’, maziwa na samaki feki ambavyo vinapatikana kwa wingi katika ‘supermaket’ nyingi nchini. Imeelezwa kuwa ulimaji wa kisasa wa mazao mengi, vikiwemo viazi hutumia madawa ya kuongeza ukubwa wa mazao kwa teknolijia inayojulikana kama GMO (Genetically Modified Organisms).

17,900+ Milk Packet Photos Stock Photos, Pictures & Royalty-Free Images - iStock

Teknolojia hiyo, ambayo kwa sasa inapigwa vita sana dunia nzima, hulifanya zao kuwa kubwa na kuonekana bora kuliko kawaida kwa kutumia ‘madawa’ ambayo yana madhara kwa mlaji. Chips na crips nyingi zinazouzwa supermarket hutengenezwa kutokana viazi vinavyolimwa kwa teknolijia hiyo.

Hali hiyo haiko kwenye mazao tu, bali pia iko kwenye samaki na maziwa. Samaki tunaouziwa ni wale wa kufugwa ambao hulishwa vyakula vya kutengenezwa ili kuwafanya wazaane kwa wingi na kuwa wanene.

Halikadhalika, maziwa mengi ya paketi hutokana na ng’ombe wa kufugwa ambao nao inaelezwa kuwa hulishwa madawa ya kuwawezesha kutoa maziwa kwa wingi na hulishwa vyakula vitokanavyo na nafaka kama vile pumba na mahindi, badala ya nyasi kama ilivyo asili yake.

Mwisho, napenda niseme hivi, suala la kuchagua chakula kilichobora unapoenda supermarket ni jambo jema, kwani huko kuna vyakula vingi vizuri na vyenye manufaa kwa afya yako, lakini pia kuna vyakula hatari iwapo utaenda kununua kwa kufuata utamaduni wa kimagharibi kwa kuamini kila kinachoingizwa kutoka nje ndiyo bora kuliko vile vilivyomo nchini mwako.

Mungu awabariki sana wapendwa, katika makala hii, napenda niishie hapa. Nakaribisha kipindi cha maswali, karibuni sana!!

Je, unahitaji pia huduma? Basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *