Fahamu Dalili 16 Za Mvurugiko Wa Homoni(Hormonal Imbalance)

Je, Homoni Ya Estrogen Ni Nini?

Maisha ya mwanamke yanaweza kuelezewa kwa kupanda na kushuka au kubadilika kwa homoni mbili, estrogen na progesterone. Wakati homoni hizi zinapokuwa na uwiano sawa, basi maisha ya mwanamke huwa ni ya ajabu mno, kwani yeye huwa anakuwa na furaha muda wote katika maisha yake ya ndoa na mwenzi wake. Mnanipata lakini wanawake jamani!

NUKUU: Amani katika ndoa huwa kubwa sana, hivyo mahusiano, mawasiliano, upendo, nk, huzidi kuongezeka kila siku. Wakati homoni hizi zinapokuwa na uwiano usiokuwa na mlinganyo sawa(hormone imbalance), ndipo matatizo mbalimbali humfuata mwanamke baadaye. Hapo ndipo amani huanza kutoweka katika maisha ya mwanamke. Ndoa hukosa amani, mahusiano huanza kuharibika, mawasiliano kati ya mume na mke huvurugika na hivyo kukaribisha majanga makubwa katika maisha ya ndoa.  Ili kutambua matatizo na masumbufu ya homoni hizi, yatupasa kwanza kujifunza na kufahamu juu ya kazi za kawaida za homoni ya estrogen na progesterone.

Homoni ya estrogen hubeba taarifa kutoka kwenye mfumo wa fahamu na kuzipeleka kwenye mfumo wa mwili na viungo vyake. Taarifa hizi hutofautiana katika kila kiungo cha mwili. Homoni ya estrogen hutuma taarifa kwenye mfuko wa kizazi(uterus) ili kuotesha na kuweka utando ambao huenezwa au kutawanywa wakati wa kipindi cha awali kabisa mwanamke anapoingia hedhini.

NUKUU: Uwezo wa mifupa hupungua ikiwa kama kiwango cha  homoni ya estrogen kitapungua. Mifupa mara nyingi huishiwa nguvu zake na baadaye hurudishiwa. Na ieleweke kuwa homoni ya estrogen huhitajika sana kwa ajili ya kutengeneza kiwango kizuri cha mfupa na kuuzuia mwili usiweze kupoteza uwezo wake kwa mwanamke. Kazi za mfuko wa uke hufanyika kupitia uwezo wa homoni ya estrogen.

Homoni ya estrogen huufanya uke kuwa na unyevunyevu na hukizuia kibofu cha mkojo kisiweze kuvujisha mkojo.  Katika hali ya ujana, homoni ya estrogen ndio hutengeneza tabia za mwanamke. Huyafanya matiti yaweze kuota kwa kuongeza idadi ya seli za matiti. Pia ndio inayofanya kuamsha viungo vya uzazi vya mwanamke.

Je, Homoni Ya Estrogen Yaweza Kupunguza Kazi Za Homoni Ya Thyroid?

Homoni ya estrogen ndio huongeza uzarishaji wa protini inayoitwa thyroid. Protin hii huifunga homoni ya thyroid na kuifanya isiwe na uwezo kabisa. Hivyo basi, hupunguza uyeyushaji mafuta na kuongeza utoaji mafuta. Mwili wako huhifadhi mafuta ili kuweze kuwepo na nguvu au nishati ya kutosha kwa ajili ya kutengeneza kiumbe katika tumbo la mwanamke ikiwa kama hali ya ujauzito itaendelea.

Homoni ya estrogen huathiri ubongo. Madhara yake katika ubongo huwa ni makubwa mno. Katika kiwango cha kawaida tu homoni ya estrogen huzuia hali ya wasiwasi au kukosa usingizi, huongeza hali hisia au nyege, na hutengeneza kiwango cha kawaida katika tendo la ndoa.

NUKUU: Ikiwa kama kiwango cha homoni ya estrogen kitapanda na kuwa juu sana au kushuka na kuwa chini sana, basi mwanamke hupatwa na hali ya msongo wa mawazo, hofu, kukosa usingizi, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa, na hata kama akiingiliwa na mumewe au mpenzi wake, yeye hukosa raha katika tendo la ndoa.

Je, Homoni Ya Progesterone Ina Kazi Gani Katika Mwili Wa Mwanamke?

Homoni ya progesterone pia hubeba taarifa katika viungo vingine. Taarifa hizi huelekezwa katika viungo vilevile vya mwili pamoja na mfumo kama ifanyavyo homoni ya estrogen lakini taarifa hizi hutofautiana kama ifuatavyo:

  1. Kwanza kabisa, homoni ya progesterone huzarishwa na ovary baada ya upevusahaji kufanyika. Homoni hii ndio huamuru utando au ute unaokuwa kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus) usimame usizidi kuongezeka ili kwamba uweze kukomaa kwa ajili ya maandalizi ya ujauzito
  2. Homoni ya progesterone huzarishwa kwa muda wa siku 14 baada ya upevushaji kumalizika. Ikiwa kama hakuna ujauzito, homoni ya progesterone hupungua na huonyesha ishara za kuanza kwa hedhi.

NUKUU: Homoni ya progesterone hupunguza uwezo wa viungo vya mwili vinavyohusiana na homoni ya estrogen kwa kupunguza idadi ya viungo vinavyopokea homoni ya estrogen. Vipokezi hivi ni molecules kwenye seli zinazotambua homoni maalum na kuziruhusu kubeba taarifa zake na kuzipeleka kwenye seli.

Homoni ya progesterone pia hupunguza ukuaji wa seli ya matiti. Homoni hii pia inahusika katika kukuza seli za matiti na kupunguza kiwango cha uwezo wa kufanya kazi kwa matiti. Homoni ya progesterone pia huchangia katika kuzuia seli za kawaida za matiti kutokufa kwenye matiti ambazo ni muhimu sana katika kuzuia salatani ya matiti.

Wakati homoni ya estrogen inapopunguza kiwango cha mifupa kuishiwa nguvu, basi homoni ya progesterone huamsha nguvu ya mifupa kutovunjika. Nguvu hii husaidia kuijenga mifupa kuwa mipya isizeheke.

Kwa kupunguza nguvu ya tezi ya thyroid, homoni progesterone huongeza uwezo wa homoni ya thyroid. Homoni ya thyroid huongeza utendaji kazi wa uyeyushaji wa mafuta mwilini, na huyatumia mafuta yaliyohifadhiwa chini ya homoni ya estrogen ili yaweze kuwa nishati ya mwili wako. Viwango cha kawaida cha homoni ya progesterone huwa muhimu sana kwa ajili ya kazi za kawaida za mwili. Viwango vya chini vya homoni ya progesterone vinaweza kusababisha mwili kuwa na uzito mkubwa au unene.

NUKUU: Progesterone huamsha utendaji kazi wa kawaida wa tendo la ndoa kwasababu inaweza kubadilishwa na kuwa homoni ya testosterone ambayo huhusika kwa mfumo wa uzazi wa mwanaume na mwanamke pia.

Progesterone hupunguza uwezo wa misuli ya mkojo kusinyaa ambayo husababisha chango la uzazi kwa kuifanya misuli ya mirija ya mkojo iweze kusinyaa.

Ndani ya ubongo, homoni ya progesterone  hujenga kitu kama asidi fulani hivi ambayo hupunguza hali ya waiswasi, kukosa usingizi pamoja na msongo wa mawazo.

Je, Dalili Za Homoni Ya Estroge Inapopungua Zinakuwaje?

Ili kutambua kuwa homoni ya estrogen imepungua au imekosekana, utaona dalili zifuatazo:

  • Kukosa amani na hivyo kuwa na mashaka mashaka
  • Uzito wa mwili kuongezeka au kunenepeana
  • Msongo wa mawazo
  • Kipanda uso
  • Kuwa na hamu na vitu vya kula kama vile udongo(pemba) au mkaa
  • Kupata hedhi ya kubadirika badirika
  • Chango la tumbo
  • Maumivu wakati wa hedhi
  • Kukosa usingizi
  • Kukosa hedhi
  • Matiti kuuma au kujaa
  • Kupatwa na uvimbe katika tumbo la uzazi
  • Kukosa hamu ya tendo la ndoa
  • Uke kuwa mkavu
  • Kupatwa na salatani ya matiti

Je, Wawezaje Kuliondoa Tatizo Hili?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri zenye mchanganyiko wa mimea ya asili, nazo zina uwezo mkubwa wa kujenga mfumo wa homoni na kurekebisha kizazi chako.

Nipende kuishia hapa mpendwa msomaji, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp tukakuunganisha na darasa letu ili upate mafunzo ya afya.

Je, Unahitaji Huduma? Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *