Takwimu inatuambia kuwa nyuki wamekuwepo kwa takribani miaka milioni 150 au zaidi. Asali ni nyingi. Imethaminiwa kuwa ni tamu tena ni nzuri mno, kwani ni chakula tena ni dawa.
Asali ni tamu mno. Kwa kuwa imetengenezwa kutokana na viungo mbalimbali vya maua, hivyo, ina mshikamano wa asili na tishu za viungo vya uzazi. Inaweza pia kuponya koo, mafua, kikohozi, vidonda, vichomi, na majeraha. Na pale inapochanganywa pamoja na mimea ya asili (kama unavyoona kwenye bidhaa yetu aina ya REDEEMER) au pale unapoiongeza kwenye bidhaa zetu kama vile FRESH HERB na CARD HERB, asali huifanya dawa iwe na uwezo wa kusafiri na kuingia kwenye tishu kwa kina zaidi na kuweka uponyaji kwenye seli za mwili tena kwa kiwango kikubwa.
Asali mbichi ni dawa, lakini asali iliyopikwa ni sumu inayouwa taratibu. Kwa nini? Katika muonekano wake wa asili, asali ina madini mengi, vitamini, vimeng’enya, amino asidi, na wanga. Lakini joto huondoa ubora wa virutubishi kwenye asali sehemu kubwa mno na kuibadilisha kuwa kitu kisichofaa kabisa. Asali iliyopikwa huunda sumu kwenye seli na inaweza kusababisha mfumo wako wa kinga kushindwa kufanya kazi vizuri. Inaweza pia kuziba mishipa na kusababisha atherosclerosis (unene wa mishipa), kuzuia mtiririko wa damu kwenye viungo muhimu. Kwa hivyo, kama utaratibu ulivyo, asali haipaswi kupikwa kabisa, na hakuna kitu kinachopaswa kupikwa pamoja na asali. Hivyo nakusihi, jifunze kuwa na mazoea ya kuongeza asali mbichi kwenye chai ya moto, uji, dawa au pakaa juu ya mkate.
Siku hizi, asali nyingi inayouzwa kibiashara, mara nyingi inakuwa imepikwa na inapaswa kuepukwa sana. Tafuta maneno ” asali mbichi” hasa kwenye maduka ya vyakula au vituo vya tiba asili (www.jamesherbalclinic.or.tz). Lakini aina safi zaidi ya asali ni mbichi kwa sababu inasaidia kuzuia (au kutuliza) mizio.
Asali, Nisaidie!
Masomo ya afya ya James Herbal Clinic kuhusu magonjwa yamejaa tiba za asili pamoja na asali.
Je, Unaipenda Habari Hii? Basi, Ifuatilie Kwa Makini Mpaka Mwisho.
- Kwa ugonjwa wa kunenepa sana au kitambi, shinikizo la juu la damu, na/au mafuta kujaa mwilini: kunywa kikombe cha maji ya moto na asali kijiko 1 cha chai na matone 5 hadi 10 ya siki ya apple cider mapema asubuhi kila siku. Fanya hivyo kila siku pale unapotumia dozi yetu ya magonjwa ya moyo.
- Ili kuondoa ugonjwa wa baridi yabisi (arthritis au rheumatoid):, chukua vijiko 2 vya asali na unga wa FRESH HERB kijiko 1 cha chai, weka kwenye maji ya moto kikombe 1 cha chai, koroga vizuri kabisa, halafu kunywa kama chai. Fanya hivyo mara 2 kila siku.
- Ili kuponya vidonda mdomoni: pakaa asali kijiko 1 cha chai na unga kidogo wa bizari kwenye vidonda, vidonda kinywani, au kwenye ulimi. Mchanganyiko huu utazalisha mate na kutoa sumu; tema mate ili kuharakisha mchakato wa uponyaji. Kwa vidonda vya tumboni, chukua unga wa CARD HERB kijiko 1 cha chai, weka kwenye maji ya moto kabisa kikombe 1 cha chai, halafu ongeza asali vijiko 2 vya chai. Koroga vizuri halafu kunywa kama chai. Fanya hivyo mara 3 kila siku.
- Ili kuponya jeraha: Pakaa kila siku asali mbichi halafu tafuta kitu kizuri cha kufunika kidonda; ifikapo jioni kiondoe ukitupe.
- Kwa baridi ya kawaida: changanya 1/2 kijiko chai cha unga wa mdalasini na kijiko 1 cha chai cha asali na kula mara mbili au tatu kwa siku.
- Ili kuondoa nya za pua: chukua mchanganyiko wa asali na juisi ya tangawizi, kunywa kijiko 1 mara mbili au tatu kwa siku.
- Kwa ajili ya kichefuchefu, kutapika, au tumbo kutokusaga chakula: changanya sehemu moja ya juisi ya limau na sehemu moja ya asali. Chovya kidole chako cha mwisho kwenye mchanganyiko huu na uilambe polepole mara mbili kila siku.
- Kwa ajili ya mashaka, au mawazo: kunywa kikombe 1 cha juisi ya machungwa na kijiko 1 cha asali mara mbili kwa siku.
- Ili kupunguza hamu ya kuvuta sigara: tafuna vipande vidogo vya mananasi na asali 1/2 kijiko cha chai kabla ya kuvuta sigara.
- Kwa maumivu ya tumbo hasa la hedhi: chukua unga wa FRESH HERB kijiko 1 cha chai, weka maji ya moto kabisa kikombe 1 cha chai, ongeza asali vijiko 2 vya chai, koroga halafu kunywa kama chai. Fanya hivyo asubuhi, mchana na jioni.
- Kwa homa ya muda mrefu: Tengeneza chai kijiko 1 cha chai cha unga wa Kivumbasi (Holy basil), weka kwenye maji ya moto kabisa kikombe 1 cha chai. Ongeza unga wa pilipili manga 1/4 kijiko cha cha chai, na asali kijiko 1 cha chai. Tumia mara 2 au 3 kwa siku.
- Ili kukomesha kwikwi: changanya asali kijiko 1 cha chai kwenye mafuta ya mnyonyo kijiko 1 cha chai, weka kwenye chombo. Tumia kuchovya kwa kidole chako cha mwisho kwenye mchanganyiko huo na uilambe. Rudia kila dakika 10 hadi kwikwi yako iishe.
Je, Utapataje Asali Mbichi?
James Herbal Clinic tunayo asali bora nzuri yenye virubishi mengi mbalimbali. Ni chakula kwako pia ni dawa.
Je, Unahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!