Fahamu Jinsi Uvimbe Wa Fibroid Unavyoweza Kuchangia Kutokwa Na Damu Nyingi Wakati Wa Hedhi.

Damu nyingi wakati wa hedhi kwa kawaida hufafanuliwa kama kipindi cha hedhi ambacho hukaa kwa muda zaidi ya siku 8 na huhitaji kubadiri pedi mara kwa mara. Wakati hakuna sababu moja kuwa uvimbe wa fibroid kuwa husababisha hedhi ya muda mrefu, kuna nadharia chache:

  • Uvimbe unaweza kukandamiza kizazi na kusababisha kutokwa damu nyingi
  • Uvimbe unaweza usisinyae vizuri, ikimaanisha hauwezi kukoma kuvuja damu
  • Uvimbe unaweza kuchochea ukuaji wa mishipa ya damu ambayo huchangia kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu au vipindi vya hedhi kubadirika na kutokwa na matone ya damu hata kipindi cha hedhi kimeisha.
  • Viwango vya juu sana vya homoni inayoitwa prostaglandins vinaweza pia kuchangia kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu.

What Exactly Is a Heavy Period & How to Tell If You Have Them – SheKnows

NUKUU: Damu ya hedhi kwa muda mrefu kutokana na uvimbe wa fibroid kwa kawaida hutegemeana na mahari uvimbe ulipo, kukaza kwa misuli ya tumbo la uzazi, kuwepo kwa matatizo ya homoni ya prostaglandins, au mvurugiko wowote kwenye ukuta wa tumbo la uzazi.

Kuthibitisha Upimaji Wa Uvimbe Wa Fibroid

Kama unapatwa na hedhi ya muda mrefu, ni vyema kufika hospitali ukaonana na mtaalamu. Uvimbe wa fibroid unapokuwa wa kawaida, basi inaonyesha karibia nusu ya wanawake huwa haoni dalili zozote za kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi.

Kwahiyo, ni vyema kuchunguza na kuona chanzo cha kutokwa na damu nya hedhi nyingi kwa muda mrefu, kama ni uvimbe wa fibroid au kitu kingine zaidi. Hali ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi inaweza kusababishwa na mambo mengi, ikiwa pamoja na:

  • Vipindi vya mayai kupevuka hubadirika
  • Damu kuwa ya mabonge
  • Mlango wa kizazi kuvimba
  • Kizazi kulegea
  • Saratani ya shingo ya kizazi
  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID
  • Mimba Kutunga nje ya kizazi
  • Mimba kuharibika
  • Ugonjwa tezi ya thyroid
  • Ugonjwa wa ini
  • Ugonjwa wa figo

Ili kubaini kama dalili zako zinatokana na uvimbe wa fibroid, basi daktari wako ataweza kufanya vipimo kwenye nyonga ili kubaini mabadiriko ya ukubwa au umbo la tumbo la uzazi au mji wa mimba, ambao unaweza kuashiria uwezo wa uvimbe wa fibroid. Vipimo vingine kama vile ultrasound au MRI, vinaweza kuhitajika ili kuthibitisha vipimo.

Unapaswa utafute daktari anachunguza kila kitu: historia yako ya matibabu, historia ya familia, pia na kuzamisha kipimo ndani ya uke na kupima damu.

Ndugu msomaji naomba niishie hapa katika makala yetu, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu!

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATsAP tukakuunganisha na darasa letu ili uzidi kujifunza zaidi juu ya mambo ya afya.

Je, Unahitaji Huduma?

Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!