Fahamu Madhara 6 Ya Ugonjwa Wa Pangusa (Chlamydia) Kwa Mwanamke.

Pangusa  ni ugonjwa  wa zinaa wa kawaida  kabisa, nayo huwa ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria aina ya pathogen ambao wanaweza kuharibu mlango wa kizazi ama shingo ya kizazi (cervix) ya mwanamke, mrija wa mkojo pamoja na njia ya haja kubwa pande zote mbili, kwa wanawake na wanaume pia.

Kwa kawaida sehemu zingine za mwili hasa sehemu za kope za macho, koo na njia ya haja kubwa zinaweza kuathiriwa na ugonjwa huu. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha PID, kwani unazidi kusumbua wengi sana katika jamii.

Je, Ugonjwa Huu Huambukizwaje?

Kwa kawaida ugonjwa wa pangusa huambukizwa kupitia njia ya kujamiiana. Zifuatazo ni njia za kawaida kabisa;

  • Kufanya mapenzi bila kutumia kinga
  • Bakteria wanaweza kusafiri kutoka ukeni na kuingia katika njia ya haja kubwa ya mwanamke hasa wakati anapojisafisha kwa kutumia toilet paper.
  • Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto mchanga wakati wa kujifungua.
  • Maambukizi haya pia  yanaweza kupatikana kupitia vidole vya mikono hasa unaposhika sehemu za uke kwa kuzichezea, hivyo yawezekana mwanaume ukapatwa na maambukizi haya kupitia vidole hata kama hujajamiiana na mwanamke, kwa mfano ugonjwa wa pangusa unaweza ukaonekana katika kope za macho.
  • Sehemu za uke, mlango wa kizazi, uume au kinywa ikiwa kama kitaingia katika maeneo hayo, nikimaanisha kwamba ugonjwa huu pia unaweza kukupata hata kama uume au ulimi haujaingia sehemu za uke.

Unaweza ukashikashika sehemu za uke za mpenzi wako ambaye tayari ana maambukizi hayo, halafu ukamuacha bila kujamiiana naye, lakini ukasahau kusafisha mikono yako na baadaye ukashika sehemu zako za macho, hivyo bakteria hao, watahamia machoni na kusababisha  maambukizi katika kope za macho.

Je, Dalili Za Ugonjwa Wa Pangusa(Chlamydia) Zinakuwaje?

Kwa kawaida dalili za ugonjwa huu huwa ni nyingi lakini baadhi ya wanawake huwa hawazifahamu, nazo zipo kama ifuatavyo:

  • Kutokwa na uchafu ukeni, wakati mwingine waweza kuwa wenye rangi ya njano na wenye harufu mbaya.
  • Kuhisi Maumivu  na kukojoa mara kwa mara.
  • Kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja ama kabla ya wakati wake, au kupata hedhi yenye damu nyingi kwa muda mrefu(yawezekana kuwa siku 7 hadi zaidi. Hiyo ni hatari)
  • Kuhisi Maumivu wakati wa kujamiiana au kutokwa na damu baada ya kujamiiana.
  • Kuhisi Maumivu chini ya kitovu na wakati mwingine kuambatana na kichefuchefu na homa kwa mbali.
  • Kuvimba kwa ngozi laini ya ndani ya uke ama inayoyozunguka ndani ya njia ya haja kubwa.

Je, Nini Madhara Ya Klamidia(Pangusa)?

Ugonjwa huu usipotibiwa mapema husababisha maambukizo katika via vya uzazi au PID (Pelvic Inflammatory Disease) na hivyo kusababisha madhara yafuatayo:

  1. Kubeba mimba nje ya kizazi (ectopic pregnancy)
  2. Maumivu ya nyonga  kwa muda mrefu.
  3. Kuporosha mimba ama kuza mtoto kabla ya miezi tisa kutimia.
  4. Uvimbe katika kibofu cha mkojo (Cystitis)
  5. Kuziba kwa mirija ya mayai(mirija inayobeba mbegu kutoka kwenye ovary na kupeleka kwenye mji wa uzazi), ambayo inaweza kusababisha mwanamke awe na usumbufu wa kubeba ujauzito ama kuwa mgumba daima.
  6. Uvimbe katika mlango wa kizazi na kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano pamoja na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Premium Photo | Pregnant Black Female Suffering From Pain Having Painful Spasm Indoors

NUKUU: Unaweza pia kupata habari ya maambukizi ya PID katika link hiyo hapo chini:

  1. Fahamu Madhara Ya Ugonjwa Wa PID

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye mchanganyiko wa vyakula na mimea ya asili, nazo zina uwezo mkubwa wa kuondoa ugonjwa huu.

Hivyo, unahitaji huduma wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Au unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya.

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

2 thoughts on “Fahamu Madhara 6 Ya Ugonjwa Wa Pangusa (Chlamydia) Kwa Mwanamke.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *