Neno “chango” hutumiwa na jamii nyingi nchini Tanzania kuelezea maumivu mbalimbali ya tumbo na mfumo wa uzazi. Katika muktadha wa kitabibu, chango mara nyingi husababishwa na mambo yafuatayo:
Vyanzo vya Chango (Kulingana na Sayansi ya Tiba)
Kitaalamu, kile kinachoitwa “chango” kinaweza kuwa kimesababishwa na:
- Matatizo ya Hedhi (Dysmenorrhea): Maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi yanayosababishwa na kemikali ya prostaglandin kufanya kuta za kizazi kujikaza kupita kiasi.
- Magonjwa ya Uzazi: Hali kama Endometriosis (tishu za kizazi kuota nje ya kizazi), Uvimbe kwenye kizazi (Fibroids), au mirija ya uzazi kuziba.
- Maambukizi ya PID: Maambukizi kwenye viungo vya juu vya uzazi (shingo ya kizazi, mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi, na vifuko ya mayai au ovari). Unaweza pia kubonyeza link hii: Fahamu Madhara 7 Mabaya Ya Ugonjwa Wa PID.
- Matatizo ya Homoni: Mvurugiko wa homoni mwilini unaweza kusababisha mzunguko wa hedhi kutoeleweka na maumivu makali.
Aina za Chango Katika Imani za Asili
- Chango la Uzazi: Husemwa linapowapata wanawake husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa, ugumba, au mimba kuharibika.
- Chango la Ngiri: Huwapata wanaume na mara nyingi huhusishwa na hernia au maumivu ya korodani.
- Chango la Watoto: Hurejelea miungurumo tumboni kwa watoto wachanga, mara nyingi ikiwa ni kukosa choo.
Je, Dalili Zake Za Kawaida Zinakuwaje?
Mtu anayesumbuliwa na tatizo hili mara nyingi hupata:
- Maumivu makali chini ya kitovu.
- Uchovu mwingi na homa anapokaribia kuingia kwenye hedhi.
- Kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa au maumivu wakati wa tendo.
- Hasira kali au jazba kabla ya siku za hedhi.
Kwa ushauri zaidi, ni vyema kupata vipimo vya kitaalamu hospitalini ili kubaini kama chanzo ni maambukizi (PID), uvimbe, au mabadiliko ya kawaida ya homoni badala ya kutegemea tiba pekee.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tuanayo dawa nzuri ya change ambayo inaondoa kwa muda mfupi tu. Unataka huduma wasiliana nasi kwa namba hii: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!