Fahamu Mambo 7 Yanayosababisha Kuondolewa Kizazi

Kuondolewa kizazi ni utaratibu wa kawaida wa upasuaji ambao wanawake wengi hupitia ili kutibu hali mbalimbali za afya kiafya katika mfumo wa uzazi wa mwanamke ili kuondoa mfuko wa uazi.

Kuna tofauti za utaratibu unaojumuisha sehemu mbalimbali za mfumo wa uzazi kulingana na hali hiyo kwa uhalisia.

Sababu Za Kuondolewa Kwa Kizazi

  1. Fibroid

Uvimbe wa Fibroid kwenye kizazi huwa ni uvimbe usio na saratani kwenye ukuta wa tumbo la uzazi. Uvimbe wa fibroid unaweza kukua sana na kuweka shinikizo au kukandamiza viungo vingine kwenye nyonga. Wanawake walio na uvimbe kwenye kizazi wanaweza kutokwa na damu nyingi sana au kuhisi maumivu makali kwenye nyonga.

  1. Kizazi Kulegea

Kizazi kulegea ni hali ambayo mfuko wa uzazi huhama na kushukia ndani ya ukeni. Kulegea kwa kizazi mara nyingi ni hali ambayo hujitokeza kwa wanawake ambao wamejifungua mara nyingi na pia linaweza kuwa tatizo kwa wanawake wanene na wanawake waliokoma hedhi. Hali hiyo inaweza kusababisha matatizo ya kukojoa mara kwa mara, kuhisi kwenda choo mara kwa mara, na kuhisi maumivu makali nkwenye nyonga au shinikizo.

  1. Kutokwa Na Damu Nyingi Ukeni

Kutokwa na damu nyingi au kwa muda mrefu kunakosababishwa na maambukizi, saratani, mvurugiko wa homoni (hormonal imbalance), au uvimbe wa fibroid kunaweza kuwa hatari. Wakati matibabu mengine yanaposhindikana, basi inaweza kupendekezwa kizazi kiondolewe.

4. Endometriosis

Endometriosis ni hali ambapo tishu zinazokuwa zimetanda kwenye ukuta wa ndani ya mfuko wa uzazi hugeuka na kuota nje ya kizazi (yaani kwenye uwazi wa nyonga, vifuko vya mayai au ovaries, mirija ya uzazi, na sehemu ya nje mfuko wa uzazi). Tishu zinazoota kama uvimbe husababisha kutokwa na damu kabla ya hedhi, pia maumivu ambayo yanaweza kuwa makali sana na kusababisha kushindwa kufanya shughuli za kila siku. Ugonjwa huu unapokuwa wa muda mrefu huwa mbaya mno na hivyo hupendekezwa kizazi kuodolewa.

5. Kizazi Kuwa Kinene (Endometrial Hyperplasia)

Endometrial Hyperplasia inahusu mfuko wa uzazi kuwa mnene. Mara nyingi husababishwa na kuwepo kwa homoni ya estrojeni bila progesterone kwa muda mrefu, ambayo inaweza kutokea wakati ambapo viwango vya homoni vinabadilika, kama vile wakati wa kukoma hedhi. Mara nyingi hali hii inapojitokeza huashiria saratani ya awali ya kizazi, na ndio maana hali hii inapojulikana hupendekezwa kizazi kiondolewe.

6. Tishu Kuota Ndani Ya Msuli Wa Mfuko Wa Uzazi(Adenomyosis)

Adenomyosis ni hali sawa na endometriosis kwa kuwa inahusisha kukua kwa ukuta wa mfuko wa uzazi ambapo haipaswi kukua. Hata hivyo, kama inavyokuwa endometriosis, tishu hukua ndani ya kuta za mfuko wa uzazi mahali ambapo hazipaswi kuwa zinaweza kusababisha kutokwa na damu na kuhisi maumivu.

7. Maambukizi Katika Via Vya Uzazi(PID)

Ugonjwa wa PID ni maambukizi ya bakteria kwenye eneo la viungo vya uzazi ambayo yanaweza kusababisha maumivu makali ya kwenye nyonga. Inapougundua mapema, PID inaweza kutibiwa kwa haraka tu na dawa za asili. Hata hivyo, ikiwa maambukizi hayatatibiwa na kuenea, yanaweza kuharibu mfuko wa uzazi, na hata kupelekea kizazi baadaye kuondolewa.

Je, Nini Madhara Yake?

Kwa wanawake ambao hawajafikia mwisho wa hedhi, hedhi haitatokea tena, wala mimba haitapatikana tena pale kizazi kinapoondolewa.

Kuondolewa kizazi, kama ilivyo taratibu zote za upasuaji, vivyo hivyo kuodolewa kizazi husababisha hatari fulani. Madaktari wa upasuaji katika magonjwa ya uzazi huchukua tahadhari kubwa ili kupunguza hatari iwezekanavyo.

Hatari za muda mfupi za kuondolewa kizazi, mara nyingi huwa za kawaida, na hutokea katika siku 30 za mwanzo baada ya upasuaji. Hatari hizi zinaweza kuwa pamoja na:

  • Damu kuganda kwenye miguu au kwenye mapafu
  • Maambukizi
  • Kupungukiwa na damu mwilini na hatari ya kuongezewa damu
  • Shinikizo la juu la damu,
  • Uharibifu katika maeneo yanayozunguka, kama vile kibofu cha mkojo, mrija wa mkojo, mishipa ya damu na neva za fahamu, nk.

Je, Nini Suluhisho La Vyanzo Vya Kuondolewa Kizazi?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa visababishi vya kuondolewa kizazi.

Unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili uweze kuungana na darasa letu la mafunzo ya afya. Kama unahitaji huduma, basi mawasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712 181 626,

Arusha- Mbauda,

Karibu sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *