Ugonjwa wa maambukizi kwenye via vya uzazi (PID) ni maambukizi yanayokuwa kwenye tumbo la uzazi la mwanamke (uterus), vifuko vya mayai (ovaries), au mirija ya uzazi.
Je, Nini Visababishi Vyake?
PID ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria. Wakati bakteria kutoka ukeni au mlango wa uzazi wanaposafiri na kuingia kwenye tumbo lako la uzazi, mirija ya uzazi au kwenye vifuko vya mayai (ovaries), wanaweza kusababisha maambukizi.
Mara nyingi, PID husababishwa na bakteria wa pangusa (chlamydia) au kisonono (gonorrhea). Haya ni magonjwa ya zinaa. Kufanya mapenzi bila kinga na mtu ambaye ana magonjwa ya zinaa kunaweza kusababisha PID.
Bakteria wanaopatikana kwenye mlango wa kizazi pia wanaweza kusafiri hadi kwenye tumbo la uzazi na mirija ya uzazi wakati wa taratibu za huduma za matibabu kama vile:
- kujifungua
- kutolewa kinyama kidogo kwenye kizazi kwa ajili ya vipimo
- mimba kuharibika
- utoaji mimba
Maambukizi haya yanazidi kuongezeka kwa kasi sana katika jamii, na haijalishi una umri gani, kijana au mzee.
Unaweza kupata maambukizi haya ikiwa kama:
- una mpezi mwenye maambukizi ya kisonono au pangusa
- una shiriki mapendi na watu wengi tofauti
- uliwahi kuwa na maambukizi ya zinaa hapo awali
- ulikuwa na PID hapo zamani
- ulianza kushiriki tendo la ndoa mapema kabla hujafikisha miaka 20
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili za kawaida za maambukizi kwenye via vya uzazi ni:
- homa
- maumivu kwenye nyonga, tumbo la chini au kwenye kiuno
- kutokwa na uteute ukeni wenye rangi isiyo ya kawaida, na harufu mbaya
Dalili zingine zinazotokana na PID ni pamoja na:
- kutokwa na damu ukeni baada ya kushiriki tendo la ndoa
- kuhisi uchovu sana
- kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- kuhisi kukojoa mara kwa mara
- kuhisi maumivu makali tumboni wakati wa hedhi
- hedhi isiyo ya kawaida au kutokwa na matone tu ya damu
- kutohisi njaa
- kuhisi kichefuchefu na kutapika
- hedhi kuruka au kukosa hedhi
- kuhisi maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa
Unaweza kuwa na PID na usiwe na dalili kali. Kwa mfano, pangusa (chlamydia) inaweza kusababisha PID bila kuonyesha dalili. Wanawake walio na mimba nje ya kizazi au ambao hawawezi kuzaa mara nyingi huwa na PID inayosababishwa na pangusa (chlamydia). Mimba inapotunga nje ya kizazi ni wakati yai linapokua nje ya tumbo la uzazi (uterus). Hali hii inafanya maisha ya mama kuwa kwenye hatari.
Uchunguzi Na Vipimo
Mtoa huduma wako wa afya anaweza kufanya uchunguzi wa fupanyonga ili kutafuta:
- Damu kutoka kwenye mlango wa kizazi. Mlango wa uzazi ni uwazi unaokuwa kwenye tumbo lako la uzazi
- Ute au uchafu unaotoka kwenye mlango wa kizazi
- Maumivu pale mlango wa kizazi unapoguswa
- Uharibifu kwenye tumbo la uzazi, mirija ya uzazi au vifuko vya mayai
Vipimo vingine ni pamoja na:
- Uteute unaotolewa ukeni au kwenye mlango wa uzazi. Sampuli hii itachunguzwa kama kisonono, pangusa, au visababishi vingine vya PID.
- Kipimo cha Ultrasound au CT scan ili kuona ni nini kingine kinachoweza kusababisha dalili zako.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa maambukizi kwenye kizazi. Unaweza pia kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu ili uweze kupata masomo ya afya kila siku.
Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!