Fahamu Mambo Yanayosababisha Mkusanyiko Wa Majmajii Mwilini

Hali ya mkusanyiko wa majimaji mwilini kitaalamu tunaita “Edema.” Majimaji haya hukusanyikana kwa wingi kwenye tishu za misuli ya mwili. Mkusanyiko wa majimaji(Edema) unaweza kuathiri sehemu yoyote ya mwili. Lakini kuna uwezekano mkubwa wa hali hii kuonekana kwenye miguu.

1+ Thousand Ankle Edema Royalty-Free Images, Stock Photos & Pictures | Shutterstock

Madawa na mimba vinaweza kusababisha majimaji kukusanyikana mwilini (edema). Hali hii inaweza pia kuwa matokeo ya ugonjwa, kama vile moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa figo, upungufu wa oksijeni kwenye damu au ini kusinyaa au kuharibika.

Wakati ugonjwa unaposababisha mkusanyiko wa majimaji mwilini, ndipo unahitaji matibabu haraka pia.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kwa kawaida tatizo hili linapotokea, dalili zake huwa kama hivi ifuatavyo:

  • Kuvimba kwa tishu hasa miguuni au mikononi
  • Ngozi kuwasha au kung’aa
  • Ngozi kubonyea na kuacha kishimo pale inapobonyezwa
  • Tumbo kujaa na kuwa kubwa
  • Miguu kuwa mizito

Je, Muda Gani Sasa Unapaswa Kufika Hospitali?

Fika hospitali kuonana na daktari ili upate vipimo au ushauri pale unapoona dalili za:

  • Kushindwa kupumua vizuri
  • Mapigo ya moyo kubadirika
  • Maumivu ya kifua

Hizi zinaweza kuwa ishara za kuongezeka kwa majimaji kwenye mapafu, ambayo pia hujulikana kama mkusanyiko wa majimaji kwenye mapafu. Inaweza kuhatarisha maisha na inahitaji matibabu ya haraka sana bila kuchelewa.

Je, Nini Vyanzo Vyake?

Edema hutokea wakati mishipa midogo ya damu mwilini, inayojulikana pia kama kapilari, inapovuja maji. Majimaji haya hulundikana kwenye tishu zilizo karibu. Kuvuja husababisha uvimbe.

Vyanzo vya matukio madogomadogo edema(kujaa majimaji) ni pamoja na:

  • Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu
  • Kula vyakula vyenye chumvi nyingi
  • Kukoma hedhi kabla ya muda wake
  • Kuwa mjamzito

Mkusanyiko wa majimaji (Edema) pia inaweza kuwa athari ya dawa fulani. Hizi ni pamoja na:

  • Madawa ya presha ya kupanda/shinikizo la juu la damu
  • Madawa ya vidonge ya kutibu uvimbe (steroid medicines)
  • Madawa ya homoni ya estrogen
  • Madawa fulani ya kisukari yanayoitwa
  • Madawa yanayotumiwa kutibu maumivu ya neva

Wakati mwingine mkusanyiko wa majimaji mwilini (edema) unaweza kuwa ishara ya hali mbaya zaidi. Magonjwa ambayo yanaweza kusababisha mkusanyiko wa majimaji mwilini (edema) ni pamoja na:

  • Moyo Kushindwa Kufanya Kazi:Kushindwa kwa moyo kufanya kazi ni pale chumba kimoja cha chini cha moyo au vyote viwili vinaposhindwa kusukuma damu vizuri. Kama matokeo, basi damu inaweza kurudi miguuni, vifundo vya miguu na kusababisha edema.

Kushindwa kwa moyo kusukuma damu kunaweza pia kusababisha tumbo kuvimba. Hali hii pia inaweza kusababisha majimaji kulundikana  kwenye mapafu. Inajulikana kama “Pulmonary edema” hali ambayo inaweza kusababisha kutokuwa na uwezo wa kupumua.

  • Kuharibika Kwa Ini:Uharibifu huu wa ini kutokana na michubuko ya ini (cirrhosis) kunaweza kusababisha majimaji kulundikana tumboni  na kwenye miguu. Mkusanyiko wa majimaji katika eneo la tumbo huitwa ascites.
  • Ugonjwa Wa Figo:Ugonjwa wa figo unaweza kusababisha majimaji na chumvi kukusanyikana kwenye damu. Mkusanyiko wa majimaji (Edema) unaohusishwa na ugonjwa wa figo kawaida hutokea kwenye miguu na usoni hasa kwenye macho.
  • Uharibifu Wa Figo:Uharibifu wa mishipa midogo ya kuchuja damu kwenye figo inaweza kusababisha kuvujisha protini nyingi na kuingi kwenye mkojo, ugonjwa ambao kitaalamu tunaita “nephrotic”. Katika ugonjwa wa nephrotic, kupungua kwa viwango vya protini kwenye damu kunaweza kusababisha mkusanyiko wa majiamji mwilini (edema).

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Ikiwa ugonjwa wa majimaji(edema) kujaa mwilini haujatibiwa, basi unaweza kusababisha:

  • Uvimbe ambao husababisha maumivu makali
  • Matatizo ya kutembea
  • Ngozi kutanuka
  • Kuongezeka kwa madhara kwenye maeneo yaliyovimba
  • Damu kububujika kidogo sana
  • Uwezo mdogo wa kutanuka kwa mishipa ya ateri na vena, jointi na misuli
  • Kuongezeka kwa hatari ya vidonda vya ngozi

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya kujaa majimaji mwilini.

Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Pia unataka ushauri, basi ungana nasi kwenye darasa letu la WHATSAP kwa kubonyeza: wa.me/255768559670

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!