Kutokwa na damu ukeni baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa, kunaweza kuwa na sababu mbalimbali. Magonjwa yanayoathiri uke peke yake yanaweza kusababisha aina hii ya kutokwa na damu. Nayo huwa ni pamoja na haya yafuatayo:
- Kukoma kwa hedhi: Hali hii huambatana na ukuta wa uke kuwa mwembamba, mkavu na kuvimba baada ya kukoma hedhi.
- Kupatwa na ugonjwa wa saratani ukeni: Hali hii huanza ukeni, nayo inaweza isionekane kama saratani lakini baadaye hujulikana kuwa saratani.
- Uke kuvimba: Huu ni uvimbe wa uke ambao unaweza kutokana na maambukizi.
Hali ya kutokwa na damu ukeni baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa pia inaweza kusababishwa na magonjwa ambayo huathiri sehemu ya chini ya mwisho wa tumbo la uzazi, inayoitwa mlango au shingo ya kizazi. Nayo huwa kama haya yafuatayo:
- Saratani ya shingo ya kizazi
- Mlango wa kizazi kutokeza nje
- Shingo ya kizazi kuvimba kutokana na maambukizi.
Magonjwa mengine ambayo yanaweza kusababisha damu kutoka ukeni baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa ni pamoja na:
- Saratani ya kizazi
- Vidonda ukeni kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Ugonjwa wa katika via vya uzazi ambao ni maambukizi kwenye tumbo la uzazi, mirija ya uzazi na vifuko vya mayai(yaani ugonjwa wa PID)
- Saratani ya mashavu ya uke
Damu kutoka ukeni baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa pia inaweza kutokana na sababu ikiwa pamoja na:
- Msuguano wakati wa tendo la ndoa kutokana na kukosa ute ukeni
- Matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango ambayo hubadirisha homoni
- Uvimbe wa fibroid unapoota kwenye ukuta wa tumbo la uzazi
Je, Nini Kinamfanya Mwanamke Kutokwa Na Damu Ukeni Baada Ya Kushiriki Tendo La Ndoa?
Kuna sababu nyingi kwa nini mwanamke anaweza kuvuja damu baada ya kufanya ngono. Jina la ugonjwa huu kitaalamu tunaita “postcoital”.
Kama una wasiwasi kwa sababu unatokwa na damu ukeni baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa, basi tafuta ushauri kutoka kwa daktari wa magonjwa ya uzazi. Watakuuliza kuhusu historia yako ya ugonjwa na kutathmini dalili zake. Kisha wanaweza kukushauri ikiwa matibabu yoyote yanahitajika.
Vyanzo Vya Kutokwa Na Damu Ukeni Baada Ya Kushiriki Tendo La Ndoa
Kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa inaweza kuwa ishara au dalili ya magonjwa haya:
- Maambukizi, kama vile PID, au maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile pangusa,
- Uke kuwa mkavu ambao hutokana na kupungua kwa kutengenezwa kwa uteute baada ya kukoma hedhi.
- Uke kuharibika, kama vile kuchanika kwa maeneo hayo ambako husababishwa na kujifungua mtoto, au ukavu au msuguano wakati unaposhiriki tendo la ndoa,
- Saratani ya mji wa mimba au mlango wa kizazi,
- Kumomonyoka kwa mlango wa kizazi, ambapo kunakuwa na eneo la uvimbe juu ya mlango wa kizazi,
Mara chache sana hali ya kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa inaweza kuwa ishara ya saratani ya shingo ya kizazi au ya uke.
Uchunguzi Na Vipimo
Kulingana na dalili zingine zozote na historia yako ya ugonjwa, daktari anaweza kupendekeza vipimo au uchunguzi, kama vile:
- Kipimo cha ujauzito (kutegemeana na umri wako)
- Kipimo kwenye tumbo la uzazi (ambapo daktari huingiza vidole ukeni mwako ili kuhisi kitu chochote kisicho cha kawaida),
- Kuangalia mlango wa kizazi kwa kutumia kifaa kinachoitwa “speculum”,
Ikiwa kama tatizo linasababishwa na ukavu ukeni, wanaweza kupendekeza kwamba ujaribu kutumia mafuta kulainishia, lakini haifai.
Unaweza pia kuelekezwa kwa daktari wa magonjwa ya uzazi ambaye ni mtaalamu.
Vipimo Vinavyopima Mlango Wa Kizazi
Ni muhimu kwamba wanawake wote wenye umri wa miaka 25 hadi 64 wapate vipimo vya uchunguzi wa mlango wa kizazi mara kwa mara ili kusaidia kuzuia saratani ya shingo ya kizazi.
Je, Suluhisho Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa visababishi vya ugonjwa huu. Unaweza kutuma pia namba yako ya WHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la afya ambalo utapata masomo ya afya kila siku.
Unahitaji huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!