FAHAMU MATATIZO YA NYAMA ZA PUA NA UGONJWA WA PUMU

Watu wengi wenye ugonjwa wa pumu pia wana matatizo sugu ya muda mrefu ya pua na njia ya hewa. Matatizo haya yanaweza kuwa ni:

  • Kuvimba kwa tishu puani(rhinitis)
  • Kuvimba kwa tishu kwenye njia ya hewa ndani ya mifupa usoni mwako(sinusitis)
  • Kuvimba kwa njia ya hewa pamoja na tishu za puani. Hapa unaweza kuwa na matatizo yote kwa pamoja au unaweza kuwa na tatizo la kuvimba kwa tishu katika njia ya hewa tu peke yake.

Je, Nini Visababishi Vyake?

Watu wengi huhangaika sana juu ya matatizo haya. Lakini magonjwa haya yanaweza kuwa na visababishi vingi sana. Visababishi hivi vina vyanzo vingi mno na vinaweza kuwa:

  • Virusi
  • Bakteria
  • Fangasi
  • Aleji

Aleji ile ile inaweza kusababisha kuota nyama za pua, kuvimba kwa nyama katika njia za hewa, pamoja na dalili za pumu. Unapotibu tatizo la aleji kutakusaidia kudhibiti ugonjwa wa pumu na dalili za kuota nyama puani. Pia unapaswa kukaa mbali na vitu vinavyosababisha dalili kwako.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili za sugu za kuvimba nyama puani, kuvimba kwa tishu katika njia ya hewa au kuwa na matatizo yote mawili kwa pamoja ni pamoja na:

  • Kupiga chafya
  • Makamasi mepesi
  • Mafua yasiyokoma
  • Makohozi kooni
  • Vidonda kooni
  • Miwasho puani
  • Kichwa kugonga
  • Kuhisi maumivu usoni na mara nyingi nyuma ya mashavu
  • Kuhisi uchovu
  • Kushindwa kuhisi harufu ya kitu
  • Kutoa harufu mbaya puani
  • Maumivu kwenye meno

Brain & Spine Foundation | Face pain

NUKUU: Dalili hizi zinaweza kulifanya tatizo lako la pumu kuwa baya zaidi. Dalili hizi zinaweza kumaanisha kwamba una uvimbe kwenye mapafu katika njia za hewa. Lakini BEST GREEN ndio mwisho wa matatizo yote hayo.

Ikiwa kama una dalili zozote hizi, basi fika hospitali kafanye uchunguzi na vipimo. Au muone daktari wa masikio, pua na koo. Katika kudhibiti dalili hizo kutakusaidia kudhibiti ugonjwa wa pumu.

Nipende kuishia hapa ndugu msomaji katika makala hii, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana.

 

Je, Unahitaji Huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na Darasa letu ukazidi kupata mafunzo juu ya magonjwa mbalimbali. Mungu akubariki!

 

Karibu sana!

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *