Kuvimba kwa tezi dume kitaalamu wanaita, “Prostatitis”. Tezi dume iko chini ya kibofu chako cha mkojo, mbele ya puru yako. Mrija wako wa mkojo (ambao hubeba mkojo na manii) hupitia katikati ya tezi dume yako.
Ikiwa una mojawapo ya aina tatu za kuvimba kwa tezi dume, tishu ndani na maeneo ya karibu na tezi tume yako huvimba, huuma na kuwashwa.
Maambukizi kwenye ya mkojo (UTI) na maambukizo mengine ya bakteria yanaweza kusababisha aina fulani za kuvimba kwa tezi dume, lakini zingine hazina vyanzo vyake.
Lakini zipo dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kudhibiti dalili zake.
Je, Aina Za Uvimbe Wa Tezi Dume Zinakuwaje?
- Uvimbe Wa Tezi Dume Wa Ghafla Kutokana Na Bakteria: Maambukizi ya bakteria wa papo kwa hapo husababisha tezi dume kuvimba. Dalili ni pamoja na homa na baridi. Unaweza kupata maumivu na kukojoa mara kwa mara au kupata shida ya kukojoa. Kuvimba kwa tezi dume kutokana na bakteria wa papo kwa hapo kunahitaji matibabu ya haraka ili kuondoa bakteria hao.
- Uvimbe Wa Tezi Dume Wa Muda Mrefu Kutokana Na Bakteria: Bakteria pia husababisha aina hii ya kuvimba kwa tezi dume. Dalili zinaweza kutokea hatua kwa hatua, na inaweza kuchukua muda mrefu kutibu ugonjwa huu. Tofauti inayokuwepo kati ya uvimbe wa tezi dume unaosababishwa na bakteria muda mfupi au wa muda mrefu kwa kawaida huwa haisababishi homa wala baridi. Bado utakuwa na dalili kama vile maumivu unapokojoa au kushindwa kukojoa.
- Uvimbe Wa Tezi Dume Usiotokana Na Bakteria: Hali hii husababisha kuvimba kwa tezi dume lakini hakuna dalili. Unaweza kujifunza kuwa una hali hii baada ya kupata vipimo ili kujua sababu ya dalili zingine. Aina hii haihitaji matibabu na sio maambukizi.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili za kuvimba kwa tezi dume hutofautiana kulingana na aina na vyanzo vyake. Ni muhimu kumwona mhudumu wa afya ikiwa unahisi maumivu kwenye fupanyonga au unapata mabadiliko wakati unapokojoa. Watu wenye uvimbe wa tezi dume isiyo sababishwa na bakteria wanaweza wasiwe na dalili zozote. Aina zingine tatu za kuvimba kwa tezi dume huashiria dalili, kama vile:
- maumivu meneo ya tumbo la chini ambayo huenda mpaka kiunoni
- kuhisi kukojoa mara kwa mara
- kuhisi maumivu wakati unapokojoa
- mkojo kuziba tena kutoka
- mkojo kuwa na damu
- damu kwenye manii
- kuhisi maumivu wakati unaposhiriki tendo la ndoa
- kuhisi maumivu pale unapofika kileleni
- kupungukiwa nguvu za kiume
Je, Nini Kinasababisha Tezi Dume Kuvimba?
Aina tofauti za kuvimba kwa tezi dume zina sababu tofauti. Wakati mwingine sababu haijulikani na wakati mwingine ni wazi kwamba sababu ni maambukizi ya bakteria.
Sababu Za Kuvimba Kwa Tezi Dume Kutokana Na Bakteria
Aina za bakteria wanaofanya tezi dume kuvimba hutokea kama matokeo ya maambukizi ya bakteria. Bakteria wanaweza kuingia kwenye kibofu chako kupitia mrija wa mkojo au wakati mkojo unarudi nyuma (vesicoureteral reflux).
Vyanzo vya bacteria wanaosababisha kuvimba kwa tezi dume ni pamoja na:
- maambukizi kwenye kifu cha mkojo au mawe kwenye kibofu
- maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- kutumia mpira wa mkojo baada ya upasuaji
- mkojo kuzuiwa kutoka
- maambukizi katika njia ya mkojo(UTI).
NUKUU: Ili uweze kujua zaidi kuhusu maambukizi ya UTI, bonyeza hapa: Mambo 6 Yanayomfanya Mwanaume Kupata UTI.
Je, Madhara Yake Ni Nini?
Watu wenye uvimbe wa tezi dume kutokana na bakteria wa papo kwa hapo wanaweza kuendeleza bakteria kuzaliana kwa wingi. Huu ni ugonjwa unaotishia maisha yako, unaoenea mwilini mwako. Inahitaji matibabu ya haraka. Madhara mengine yanaweza kuwa ni pamoja na:
- kushindwa kushiriki kabisa tendo la ndoa
- uvimbe ambao huenea kwenye viungo vinavyokuwa karibu na tezi dume
Hivyo msomaji, napenda kukushukuru sana, hivyo naomba niishie hapa nikaribishe kipindi chako cha maswali na maoni yako. Pia unaweza ukatuma namba yako ya WhatsAp tukakuunganisha kwenye darasa letu la mafunzo ya masomo ya afya.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tumekuandalia dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya kuvimba kwa tezi dume, nk. Hivyo unaweza kuwasiliana nasi ili upate huduma kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712 181 626.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya ya kila siku.
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!