FAHAMU VYANZO VYA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB), DALILI ZAKE, MADHARA YAKE NA TIBA YAKE.

Kifua kikuu(TB) ni ugonjwa unaweza kuwa mbaya kabisa ambao huathiri sana mapafu. Bakteria wanaosababisha ugonjwa wa kifua kikuu(TB) husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia matone madogo ya mate yanayotolewa baada ya kupiga chafya au kukohoa.

Mara chache katika nchi zilizoendelea, maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu yalianza kuongezeka mnamo mwaka 1985, kwasababu ya kuibuka kwa Virusi Vya Ukimwi(VVU), kirusi kilichosababisha upungufu wa kinga mwilini(AIDS).  Virusi vya ukimwi hudhoofisha mfumo kinga wa mwili wa mwanadamu, kwahiyo hauwezi kushambulia vimelea wa ugonjwa wa kifua kikuu(TB).

1,876 Tuberculosis Patient Stock Photos, Pictures & Royalty ...

NUKUU: Magonjwa mengi ya kifua kikuu hupinga dawa zinazotumiwa ili kutibu ugonjwa huo. Watu wenye ugonjwa sugu wa kifua kikuu sharti watumie aina mbalimbali za madawa kwa miezi kadhaa ili kuepukana na maambukizi na kuondokana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Ingawa mwili wako unaweza kubeba bakteria wanaosababisha kifua kikuu(TB), mfumo kinga wa mwili wako mara nyingi unaweza kuzuia wewe usiwe mgonjwa. Kwasababu hiyo, daktari hufanya tofauti kati ya:

  1. Ugonjwa Wa Kifua Kikuu Uliojificha

Una mambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu, lakini bakteria mwilini mwako sio hai na hawasababishi dalili. Ugonjwa wa kifua kikuu, pia unaitwa kifua kikuu kisicho hai au maambukizi ya kifua kikuu, sio ya kuambukiza. Ugonjwa wa kifua kikuu uliojificha unaweza kubadirika ukawa hai, kwahiyo matibabu ni ya muhimu sana.

  1. Ugonjwa Wa Kifua Kikuu Ulio Hai

Pia unaitwa ugonjwa wa kifua kikuu, hali hii hukufanya wewe uwe mgonjwa na wakati mwingine unaweza kuenea kwa wengine. Unaweza kutokea kwa muda wa majuma kadhaa au miaka baada ya kuambukiwa na bakteria wa kifua kikuu.

Ishara na dalili zake huwa kama hivi ifuatavyo:

  • Kukohoa kwa muda wa wiki tatu au zaidi
  • Kukohoa makohozi yenye damu
  • Maumivu ya kifua, au maumivu kifuani unapopumua au kukohoa
  • Mwili kupungua
  • Mwili kuchoka
  • Kuhisi homa
  • Kutokwa na jasho usiku
  • Kuhisi baridi
  • Kukosa hamu ya kula

Renal tuberculosis | Radiology Reference Article | Radiopaedia.org

NUKUU: Kifua kikuu pia kinaweza kuathiri maeneo mengine ya mwili wako, ikiwa pamoja na figo, uti wa mgongo na ubongo. Ugonjwa wa kifua kikuu unapojitokeza nje ya mapafu yako, dalili hutofautiana kulingana na viungo vilivyohusika. Kwa mfano, maambukiz ya kifua kikuu kwenye uti wa mgogo lazima isababishe maumivu ya mgongo, na maambuki ya kifua kikuu kwenye figo lazima yasababishe damu kwenye mkojo wako.

Je, Lini Unapaswa Umuone Daktari?

Fika hospitali umuone daktari ikiwa kama una hisi homa, uzito wa mwili kupungua, kutokwa na jasho jingi usiku au kukohoa bila kukoma. Hizi mara nyingi huwa ni ishara za ugonjwa wa kifua kikuu lakini inaweza kutokana na magonjwa mengine. Pia, muone daktari ikiwa kama unafikiri uliwahi kuwa karibu na mtu mwenye ugonjwa wa kifua kikuu.

Vituo vya afya vinapendekeza kwamba watu wenye vihatarishi vikubwa vya ugonjwa wa kifua kikuu wanapaswa wapate vipimo ili kubaini maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu uliojificha. Mapendekezo haya yanajumuisha watu ambao:

  • Wana Virusi Vya Ukimwi(VVU)
  • Wanaotumia vidonge vya ukimwi
  • Wana mahusiano na watu walioambukizwa
  • Wanatoka katika nchi ambapo ugonjwa wa kifua kikuu ni wa kawaida
  • Wanaishi au wanafanyakazi kwenye maeneo ambapo kifua kikuu ni kawaida kama vile magerezani, nk.
  • Wanafanya kazi hospitalini na wanatibu wagonjwa wenye vihatarishi vya kifua kikuu.

Je, Nini Husababisha Kifua Kikuu?

Ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na bakteria ambao husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia matone madogo madogo ya mate. Hii inaweza kutokea pale mtu mwenye ugonjwa huo ambao haujatibiwa, kikohozi kilicho hai, au anapozungumza na kutoa matone ya mate, au anapopiga chafya, au anapotema mate, au anapocheka au kuimba.

Ingawa ugonjwa kifua kikuu unaambukiza, sio rahisi kuupata. Una uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kifua kikuu kutoka kwa mtu unayeishi naye au unayefanya kazi naye kuliko kutoka kwa mgeni. Watu wengi walio na kifua kikuu hai ambao wamekuwa na matibabu sahihi kwa angalau wiki mbili hawawezi kuambukiza tena.

Je, Vipi Kuhusu Upungufu Wa Kinga Mwilini Na Kifua Kikuu?

Tangu mwaka 1980, ugonjwa wa kifua kikuu umeongezeka kwa kasi sana kwasababu ya kuenea kwa upungufu wa kinga mwilini, visrui ambavyo vilisababisha AIDS. HIV hugandamiza mfumo kinga wa mwili, hivyo huufanya mwili kushindwa kuthibiti bakteria wa kifua kikuu. Kama yalivyo matokeo, watu wenye HIV wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu na kutokana na maambukizi ya kifua kikuu yaliyojificha na kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu ulio hai kuliko watu ambao hawana maambukizi ya HIV.

Je, Vipi Kuhusu Madawa Ya Vidonge Kwa Ajili Ya Kudhibiti Kifua Kikuu?

Ugonjwa wa kifua kikuu pia bado ni muuaji mkuu kwasababu ya ongezeko la aina nyingi za madawa anayotumia mgonjwa. Baada ya muda, baadhi ya vimelea wa ugonjwa wa kifua kikuu, wamekuwa na uwezo mkubwa wa kuishi licha ya kutumia madawa. Hii ni kwasababu watu watu hawatumii madawa kama walivyoelekezwa au hawamalizi kozi ya matibabu.

Aina za madawa ya kuthibiti ugonjwa wa kifua kikuu hujitokeza pale antibiotic zinaposhindwa kuua bakteria zote kwa malengo. Bakteria wanaoishi huwa sugu kwa madawa hayo na mara nyingi hata madawa mengine pia. Baadhi ya bakteria wa kifua kikuu huendelea kuwa sugu dhidi ya madawa ya kawaida kama vile isoniazid, pamoja na rifampin(Rifadin, Rimactane).

Baadhi ya aina za ugonjwa wa kifua kikuu zimekuwa zikikuza upinzani dhidi ya madawa ambayo hayatumiki sana katika kutibu ugonjwa wa kifua kikuu, kama vile madawa yajulikanayo kama fluoroquinolones, na injectable pamoja na amikacin na capreomycin(Capastat). Madawa haya mara nyingi hutumiwa kutibu maambukizi ambayo ni sugu kwa madawa yanayotumiwa zaidi.

Vihatarishi

Mtu yoyote anaweza kupata kifua kikuu, lakini mambo fulani yanaweza kuongeza vihatarishi vyako, ikiwa pamoja na:

Mfumo Kinga Uliodhoofika

Mfumo kinga wenye afya mara nyingi hudhibiti bakteria wa kifua kikuu kwa uhakika kabisa. Hata hivyo hivyo, magonjwa na madawa mbalimbali yanaweza kudhoofisha mfumo kinga wako wa mwili, kama vile;

  • Kisukari
  • Magonjwa mabaya ya figo
  • Magonjwa ya saratani
  • Matibabu ya saratani kama vile kupigwa mionzi
  • Madawa yanayotumika kutibu ugonjwa wa baridi yabisi, nk
  • Utapia mlo
  • HIV au AID

Je, Madhara Ya Ugonjwa Wa Kifua Kikuu Ni Nini?

Bila matibabu, ugonjwa wa kifua kikuu unaweza kuwa hatari. Ugonjwa wa kifua kikuu usiotibiwa kwa kawaida huathiri mapafu, lakini unaweza kuathiri sehemu zingine za mwili wako pia.

Madhara ya ugonjwa wa kifua kikuu ni pamoja na:

  • Maumivu ya uti wa mgongo
  • Kuharibika kwa viunganishi vya mifupa(joints)
  • Kuvimba kwa membrane zinazofunika ubongo wako
  • Matatizo ya figo au ini
  • Magonjwa ya moyo

Jinsi Ya Kudhibiti

Kama ukipima maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu uliojificha, basi daktari wako lazima akushauri kutumia madawa ili kupunguza vihatarishi vyako vya kuendeleza kifua kikuu kilicho hai. Mara nyingi ugonjwa wa kifua kikuu ulio hai huambukiza.

Je, Unawezaje Kulinda Familia Yako Na Marafiki Zako?

Kama una ugonjwa wa kifua kikuu ulio hai, kwa kawaida huchukua wiki chache kwa matibabu ya kifua kikuu kabla hujaambukiza kabisa. Fuata hatua hizi ili kusaidia rafiki zako wasiweze kupata maambukizi hayo:

  1. Kaa nyumba

Usiende kazini au shuleni au kulala chumbani na watu wengine wiki chahche  wakati unapotumia tiba.

  1. Fungua Chumba

Vimelea wa ugonjwa wa kifua kikuu husambaa kwa urahisi kwenye eneo dogo tu lililofungwa ambapo hewa haitoki. Ikiwa nje sio baridi sana, fungua madirisha na utumie feni kupuliza hewa ya ndani itoke nje.

  1. Funika Kinywa Chako

Tumia tishu kufunika mdomo wako muda wowote unapocheka, au kupiga chafya au kukohoa. Hakikisha unaweza tishu chafu kwenye begi, ikunje na uitupe.

  1. Vaa Barakoa

Kuvaa barakoa unapokuwa karibu na watu wakati wa wiki tatu za mwanzo za matibabu inaweza kusaidia kupunguza vihatarishi vya maambukizi.

Kamilisha Matibabu Yako

Hii ni hatua muhimu sana unayoweza kuichukua ili kujilinda mwenyewe na wengine wasiweze kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu. Unapoacha matibabu mapema au kuruka dozi, bakteria wa kifua kikuu wana nafasi ya kukuza mabadiriko ambayo huwaruhusu kustahimili dawa za kifua kikuu zenye nguvu zaidi.

Ugonjwa huu huwa hatari na hivyo madawa ya vidonge yanayotumika kudhibiti na kuutibu hushindwa kabisa kufanya kazi.

Ndugu msomaji makala yetu inaishia hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana!

Je, Unahitaji Huduma Ya Tiba Asili Ili Kuondoa Tatizo Hili?

Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuunganishwa na GROUP letu uweze kupata ushauri na maelekezo zaidi juu ya masuala ya afya.

Karibu sana!

Arusha Mbauda-Maua