Haya Ndio Madhara Ya Uvimbe Wa Fibroid Unaposhindwa Kutibiwa Mapema

Fibroid ni aina ya kawaida ya uvimbe. Takriban 40% hadi 80% ya watu wenye tumbo la uzazi wana uvimbe wa fibroid. Hali hii mara Mara  hutokea kwa watu walio na umri kati ya miaka 30 na 50. 

Mabinti ambao badi hawajavunja ungo, wao hawapatwi na uvimbe wa fibroid. Pia tatizo hili haliwapati wanawake ambao tayari wameshakoma kuingia hedhini.

Je, Maumivu Ya Uvimbe Wa Fibroid Unayahisi Vipi?

Kuna aina mbalimbali za hisia unaweza kupata ikiwa kama una uvimbe wa fibroid. Ikiwa una uvimbe mdogo wa fibroid, unaweza usihisi chochote na hata usitambue kuwa kuna uvimbe. Hata hivyo, uvimbe unapokuwa mkubwa unaweza kupata masumbufu na maumivu.Uvimbe wa Fibroid unaweza kukusababishia kuhisi maumivu ya mgongo, maumivu ya vichomi kwenye tumbo lako na hata maumivu wakati wa kujamiiana.

Je, Uvimbe Wa Fibroid Una Muonekano Gani?

Fibroid kwa kawaida ni uvimbe wa mviringo ambao huonekana kama uvimbe mlaini.

Katika baadhi ya matukio, unaweza kuungana na kikonyo chembamba hivi. Vivimbe vya fibroid vinapokuwa vingi husababisha madhara  kama haya:

  • Mamumivu ambayo sio ya kuvumilika
  • Tumbo kuvimba au maeneo ya nyonga
  • Kutokwa na damu nyingi sana
  • Kupungukiwa damu
  • Kutokushika mimba

Je, Uvimbe Wa Fibroid Unasababisha Kupungukiwa Damu Mwilini?

Upungufu wa damu ni hali inayotokea wakati mwili wako hauna chembechembe nyekundu za damu  zenye afya za kutosha ili kupeleka oksijeni kwenye viungo vyako. Anemia inaweza kutokea kwa watu ambao wana hedhi mara kwa mara au nzito sana. Fibroids inaweza kusababisha hedhi yako kutoka nyingi sana au kipindi cha hedhi kujirudia ndani ya mwezi mmoja. Ongea na mtoa huduma wako wa afya ikiwa unapata dalili za upungufu wa damu wakati una uvimbe wa fibroid.

Je, Uvimbe Wa Fibroid Unaweza Kuzuiwa?

Kwa ujumla, huwezi kuzuia uvimbe wa fibroid. Unaweza kupunguza hatari yako kwa kupunguza uzito wa mwili ili kuufanya uwe na afya na kupata vipimo mara wa mara. Ikiwa una uvimbe mdogo wa fibroid, jitahidi haraka sana kufanya matibabu.

Je, Fibroid Inaweza Kuendelea Kubadilika Tena Na Tena?

Uvimbe wa Fibroid unaweza kweli kupungua au kukua kwa muda mrefu. Unaweza kubadilisha ukubwa ghafla au kwa kasi kwa muda mrefu. Hii inaweza kutokea kwa sababu mbalimbali, lakini katika hali nyingi, mabadiliko haya katika ukubwa wa fibroid yanahusishwa na kiasi cha homoni katika mwili wako. Unapokuwa na viwango vya juu vya homoni mwilini mwako, fibroids inaweza kuwa kubwa zaidi. Hili linaweza kutokea nyakati mahususi maishani mwako, kama vile ujauzito. Uvimbe wa Fibroid pia unaweza kupungua wakati viwango vyako vya homoni vinapopungua. Hii ni kawaida baada ya umri wa hedhi kukoma. Mara nyingi, dalili zake zinaweza pia kuwa bora baada ya kufikia umri wa kukoma hedhi.

Je, Nini Suluhisho Lake?

James herbal Clinic tunazo dawa nzuri mno zenye uwezo mkubwa wa kuondoa uvimbe na matatizo mengine mengi ya uzazi. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu la masomo ya afya ya kila siku.

Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu Sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *