Ugonjwa wa maambukizi katika via vyauzazi (PID) ni maambukizi ya mirija ya mayai (fallopian tubes), vifuko vya mayai (ovaries), mfuko wa kizazi (uterus) pamoja na shingo ya kizazi (cervix).
Ugonjwa huu usipotibiwa unaweza kusababisha makovu ama tishu kuotea na ikiwa na mkusanyiko wa ute mchafu kama vile usaha kwenye mirija ya mayai, na hivyo kuharibu viungo vyako vya uzazi.
Miongoni mwa wanawake 8 wenye ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi (PID), mmoja anaweza kupata tatizo la kutoshika ujauzito au kuwa mgumba daima.
Ugonjwa huu kama ilivyo kawaida hutokana na maambukizi katika via vya uzazi. Hali hii hujitokeza pindi bacteria wanapoingia kupitia uke au shingo ya kizazi na kuenea mpaka kwenye mfuko wa kizazi(uterus), mirija ya mayai, au vifuko vya mayai(ovaries). Bakteria hawa hutokana na magonjwa ya zinaa kama vile pangusa (Chlamydia), kisonono (gonorrhea), nk. Bakteria wa magonjwa ya zinaa humpata muhusika ikiwa kama atafanya tendo la ndoa bila kutumia kinga.
Ni mara chache sana ugonjwa wa PID unaweza kumpata mwanamke baada ya kujifungua mtoto, mimba kuharibika, kutoa mimba, ama kuingiziwa chombo kama vile kipimo ukeni.
Mwanamke yuko katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huu ikiwa kama:
- Ana ugonjwa wa maambukizi lakini hajazingatia kuutibu
- Anapoanza tendo la ndoa chini ya umri wa miaka 18
- Ana wapenzi zaidi ya mmoja
- Ana mpenzi mwenye zaidi ya mpenzi mmoja
- Ana mpenzi aliyewahi kupatwa na maambukizi ya PID hapo mwanzo
Katika makala yetu ya mwanzo tuliona dalili za PID anazozipata mwanamke huwa kama ifuatavyo:
- Maumivu ya nyonga, tumbo la chini au kiuno
- Maumivu wakati watendo la ndoa
- Kutokwa na uchafu mwingi ukeni tena wenye harufu mbaya
- Maumivu au kushindwa kukojoa
- Mzunguko wa hedhi wa kubadirikabadirika
- Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi ambayo huwa makali kuliko kawaida
- Kuhisi homa au baridi
- Kuhisi kichefuchefu au kutapika
- Mwili kuchoka
Je, Nini MadharaYa PID Isipotibiwa Mapema?
Ikiwa kama ugonjwa huu hautatibiwa, basi unaweza kusababisha vidonda ama makovu kwenye viungo vyako vya uzazi ambayo yanaweza kusababisha:
- maumivu makali ya nyonga
- mimba kutunga nje ya kizazi
- mirija ya uzazi kuziba
- vivimbe maji kwenye vifuko vya mayai (ovarian cysts)
- ugumba
- usaha kwenye mirija au vifuko vya mayai
NUKUU: Pia fungua link hii: Fahamu Madhara Ya Ugonjwa Wa PID
Madhara ya maambukizi haya yanaweza pia kuenea mpaka kwenye mzunguko wa damu au katika sehemu zingine za mwili wako. Yafaa sana kumuona daktari mapema ikiwa kama unahisi una tatizo hili la PID. Dawa zetu za asili zitakusaidia sana katika kuondoa tatizo hili na kuzuia kabisa madhara katika mfumo wako wa uzazi.
Je, Unawezaje Kujikinga Na UgonjwaWa PID?
Unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kinga na kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu.
Je, Unawezaje KupataVipimo?
-
Kupiga bomba: Usipende kupiga bomba, kwani kwa kutumia njia hii unaweza kusababisha kuharibu uwiano wa bacteria katika uke wako.
-
Kupima magonjwa ya zinaa: Unapopima magonjwa ya zinaa na kuanza kuyatibu mapema, kunaweza kukusaidia usipatwe na matatizo ya PID.
-
Kuwamsafi: Unapokuwa ukitawaza au kusafisha uke wako, hakikisha unafuta uke wako kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kujisaidia haja kubwa ili kuzuia kuenea kwa bacteria walioko sehemu ya njia ya haja kubwa wasiingie katika eneo la uke.
NUKUU: Madaktari hupima ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi (PID), kwa kuangalia dalili zilizopo, kama vile kupima mkojo, uchafu unaotoka ukeni, kupiga picha kwenye nyonga, nk.
Wakati wa kupiga picha kwenye nyonga, daktari wako ataanza kwanza kuchunguza nyonga zako kwa kuangalia dalili au isharaza PID. Daktari wako hatimaye anaweza kutumia pamba ili kuchukua kielelezo kutoka kwenye uke wako ama shingo ya kizazi chako. Kielelezo hicho kitapimwa ndani ya maabara ili kubaini vimelea waliosababisha maambukizi hayo.
Ili kuhakikishakipimo au kubaini maambukizi haya yameenea kwa ukubwa gani, basi daktari wako anapaswa apendekeze vipimo vingine tena kama vile:
- Vipimo vya damu na mkojo. Vipimo hivi vitapima kiwango cha chembe zako nyeupe za damu, ambavyo vitaonyesha maambukizi, na kutia alama inayoonyesha uvimbe. Daktari wako pia sharti apendekeze vipimo vya HIV pamoja na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo wakati mwingine huchangamana na PID.
- Vipimo vya Ultrasound: Kipimo hiki hutumia sauti ya mawimbi ili kutengeneza umbo la viungovyako vya uzazi.
- Laparoscopy: Wakati unapofanyika utaratibu huu, daktari wako huingiza kifaa chembamba chenye incha kali kwenye tumbo lako la chini ili kuangalia viungo vya nyonga yako.
Je, MatibabuYake Yanafanyikaje?
Matibabu ya maambukizi katika via vya uzazi(PID) yanatakiwa yafanyike kama ifuatavyo:
- Matibabu Kwa Mwenzi Wako: Ili kuzuia ugonjwa usiendelee, yafaa pia mwenzi wako apate vipimo na aanze tiba. Wapenzi wenye maambukizi haya wakati mwingine wanaweza wasionyeshe dalili zao.
- Kujizuia Kwa Muda: Jizue kufanya tendo la ndoa mpaka pale matibabu ya PID yatakapokamilika, vipimo vitakapodhihirisha kuwa maambukizi yametoweka kabisa kwa wapenzi wote wawili, ikiwa kama ni mume na mke au mtu na mpenzi wake. James & Ferdinand Herbal Clinic tunapenda sana kuwashauri ndugu wapendwa kwasababu tatizo hili linazidi kukithiri katika jamii kutokana na kutozingatia masharti ya matibabu.
Wanawake wengi wenye ugonjwa huu wanahitaji matibabu ya nje. Ili kuondoa na kuzuia madhara ya uvimbe ndani ya kizazi kama vile kuvimba kwa mlango wa uzazi (Cervitis), basi unapaswa kutumia dawa zetu za asili zenye uwezo wa kuondoa vyanzo na madhara ya ugonjwa wa PID.
NUKUU: Pia bonyeza hapa: Fahamu Mambo Yanayopelekea Mlango Wa Kizazi Kuvimba
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tuna dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo na madhara ya ugonjwa wa PID. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Unahitaji Huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Asante Sana!