Je, Ujauzito Ni Nini?
Ujauzito ni kipindi ambacho wakati huo kiumbe kimoja au zaidi kinaanza kuumbika tumboni mwa mwanamke. Ujauzito unaweza kujitokeza kwa kujamiiana au njia nyingine ya kitaalamu kama vile kupandikiza. Hali ya kujifungua kwa kawaida hutokea baada ya wiki 40.
Je, unahisi kuwa una ujauzito? Uhakika uko katika kipimo cha ujauzito. Lakini kabla hujaona hedhi, unaweza ukahisi au kuwa na tumaini kwamba uko na ujauzito. Sasa leo James Herbal Clinic tunapenda kukufahamisha dalili za ujauzito na kwanini huwa zinatokea.
Je, Dalili Za Ujauzito Zinakuwaje?
Kwa kawaida dalili za awali za ujauzito huwa kama ifuatavyo:
- Kukosa Hedhi
Ikiwa kama uko katika umri wa kuzaa na huenda wiki moja imepita au zaidi bila kuona dalili zozote za hedhi, basi tambua kuwa uko na ujauzito. Hata hivyo dalili hizi zinaweza kuvurugika ikiwa kama una mzunguko wa hedhi wenye kubadirik badirika.
- Matiti Kuvimba Na Kuuma
Mabadiriko ya awali ya vichochezi au homoni katika ujauzito yanaweza kusababisha matiti yako kuuma. Hali hii itaanza kupungua baada ya wiki chache kadiri mwili wako unavyozidi kubadiri homoni zake.
- Kuhisi Kichefuchefu Bila Kutapika Au Na Kutapika
Kichefuchefu cha mjamzito asubuhi ambacho kinaweza kutokea muda wowote wa asubuhi au usiku, mara nyingi huanza mwezi mmoja baada ya kupata ujauzito. Hata hivyo, baadhi ya wanawake huanza kuhisi kichefuchefu mapema na wengi hushindwa kuona hali kama hii. Ikiwa kama chanzo cha kichefuchefu wakati wa ujauzito kitasumbua sana, basi mfumo wa homoni hushughulika kurekebisha hali hiyo.
- Kuongezeka Hali Ya Kukojoa
Unaweza ukijitambua tu mara tu utakapokuwa unaenda kukojoa mara kwa mara kuliko kawaida. Kiwango cha damu mwilini mwako huongezeka wakati wa ujauzito, na kusababisha mapafu yako kuanza kutengeneza majimaji ambayo husafirishwa mpaka kwenye kibofu cha mkojo.
- Uchovu
Uchovu pia huzidi kuwa mkubwa ukiambatana na dalili za awali za ujauzito. Wakati wa ujauzito wa awali, kiwango cha homoni ya progesterone hupanda sana ambacho ndicho humfanya mjamzito kupata usingizi mara kwa mara.
Je, Dalili Zingine Za Ujauzito Zinakuwaje?
Dalili zingine unazoweza kuzipata wakati wa kipindi cha awali cha ujauzito huwa kama ifuatavyo:
- Hasira
Mbubujiko wa vichochezi au homoni mwilini mwako wakati wa kipindi cha awali cha ujauzito, unaweza kukufanya kuwa mwenye hasira na mwepesi kutoa machozi.
- Tumbo Kujaa Gesi
Kubadirika kwa homoni wakati wa awali wa ujauzito kunaweza kusababisha ujisikie tumbo kujaa gesi, vile vile kama unavyojisikia wakati kipindi cha hedhi kinapokaribia.
- Kutokwa Na Matone Ya Damu
Wakati mwingine unapoona kiwango kidogo cha matone ya damu kinatoka, yaweza kuwa ni ujauzito. Hujulikana kama kuvuja damu wakati wa upandikizaji, nayo ni hali ambayo hujitokeza wakati yai lililorutubishwa lipojipachika kwenye ukuta wa kifuko cha kizazi kwa muda siku 10-14 baada ya utungishaji wa mimba. Hali ya kuvuja damu wakati upandikizaji hutokea wakati wa kipindi cha hedhi. Hata hivyo, sio kwamba wanawake wote huwa wana hali hii.
- Vichomi: Baadhi ya wanawake hupatwa na hali ya vichomi wakati wa hali ya mwanzo ya
- Kukosa Choo: Kubadirika kwa homoni husababisha mfumo wako wa umeng’enyaji kufanya kazi taratibu mno, hali ambayo inaweza kusababisha kukosa choo.
- Kuchukia Chakula
Kwa kawaida unapokuwa mjamzito, lazima uchukie harufu au ladha za vyakula fulani. Kama ilivyo dalili zingine za ujauzito, vyakula hivi vinaweza kuchukiwa kutokana na kubadirika kwa homoni.
Je, Una Ujauzito Kweli?
NUKUU: Kwa bahati mbaya, dalili nyingi za ujauzito huwa zinatofautiana. Zingine zinawe kuonyesha kwamba wewe ni mgonjwa au kwamba kipindi chako cha hedhi kinakaribia kuanza. Vile vile unaweza kuwa mjamzito bila kuona dalili nyingi kama nilizo taja hapo juu.
Na bado, ikiwa kama ukishindwa kuona hedhi na kutambua dalili kama nilizotaja hapo juu, basi unaweza ukachukua kipimo cha ujauzito hata kama ni nyumbani, pima mkojo wako ili kuhakiki. Kama kipimo chako cha nyumbani kitaonyesha kuwa una ujauzito, basi jaribu kufika hospitali ili kumuona daktari. Kitendo cha kuhakiki mimba yako mapema kitakusaidia pia kuanza kuanza kliniki mapema.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana.