Je, unatambua kuwa unaweza ukapatwa na maambukizi na kisha yakampata mtoto wako aliyeko tumboni ambayo yanaweza kusababisha madhara makubwa katika ukuaji wake? Moja ya maambukizi hayo ni kisonono. Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unatokana na bakteria ambao huzaliana na kuenea kwa kasi sana. Ikiwa kama ugonjwa wa kisonono utagundulika mapema wakati wa ujauzito na kisha ukaanza kutibiwa mapema, unaweza ukatibika.
Ijapokuwa kisonono huwa ni ugonjwa usioonyesha dalili mbaya sana, lakini unaweza kuwa ugonjwa mbaya zaidi wenye kutisha ikiwa kama hautatibiwa mapema. Kwahiyo, inafaa sana kuanza vipimo mapema juu ya maambukizi ya kisonono mara unapopata ujauzito.
Je, Kisonono Ni Nini?
Kisonono ni ugonjwa wa zinaa ambao humuathiri mwanamke na mwanaume pia.
- Maambukizi haya huathiri sehemu za siri, koo, pamoja na njia ya haja kubwa
- Mwanamke mjamzito mwenye kisonono anaweza akamwambukiza mwanae pindi anapojifungua mtoto wake.
- Kwa kawaida mtoto anayezaliwa huonyesha dalili za kisonono baada ya siku 2-5 mara baada ya kuzaliwa.
- Kwa mtoto mchanga aliyezaliwa, maambukizi mara nyingi huathiri macho. Ikiwa kama mtoto mchanga atachelewa kutibiwa, hali hii inaweza kusababisha pia upofu wa macho wa kudumu.
- Maambukizi yanaweza kuingia kwenye mfumo wa mzunguko wa damu kwa mtoto mchanga ikiwa kama hautafanyika utaratibu mzuri wa matibabu. Hali hii inaweza kuzidi kusababisha madhara kwenye damu au jointi za mifupa ama homa ya uti wa mgongo.
Je, Nini Kinasababisha Kisonono Wakati Wa Ujauzito?
Hali ya kukua kwa bakteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhea hueneza ugonjwa wa kisonono mwilini. Mtu yeyote anayefanya ngono zembe anaweza akapata maambukizi haya. Maambukizi huwaathiri hasa watu wanapokuwa katika umri wa ujana yaani miaka 20-30.
Je, Dalili Za Kisonono Kwa Mjamzito Zinakuwaje?
Dalili za kisonono zinaweza zikawepo lakini zizsigundulike kwa urahisi kwani zinaweza zikafanana tu na zile zinazojitokeza ukeni. Hata hivyo, kama nilivyoeleza mwanzoni kwamba, yafaa sana mwanamke kupata vipimo mapema juu ya ugonjwa wa kisonono mara anapopata ujauzito. Hapo chini kuna dalili chache za ugonjwa kisonono kwa mama mjamzito, nazo ni:
- Kuhisi maumivu au hali ya kuwaka moto hasa wakati wa kukojoa
- Kutokwa na uchafu mwingi sehemu za uke
- Kutokwa na damu kama vile yuko hedhini.
Ikiwa kama kuna maambukizi sehemu za njia ya haja kubwa, dalili zake huwa ni:
- Kuwashwa sehemu za njia ya haja kubwa
- Kupatwa na vidonda sehemu ya njia ya haja kubwa na pia kutokwa na damu
- Kuhisi maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
Ikiwa kama kuna athari kwenye macho dalili zake huwa ni:
- Macho kuwa mekundu tena yenye kuwasha
- Kutokwa na majimaji ukeni
NUKUU: Unapopatwa na dalili hizi unapaswa ufike hospitali mapema bila kuchelewa. Kwa namna hiyo inaweza kukusaidia ukapata matibabu haraka.
Je, Kuna Madhara Gani Ya Kisonono Kwa Mwanamke Mjamzito?
Ugonjwa wa kisonono usipopimwa na kugundulika na kisha ukashindwa kutibiwa mapema pindi mwanamke anapokuwa mjamzito, basi unaweza kusababisha madhara yafuatayo:
- Mimba kuharibika au kujifungua kabla ya miezi kutimia
- Kusababisha maambukizi kwa mtoto mchanga mara unapojifua.
- Kusababisha upofu wa macho au matatizo ya jointi za mifupa kwa mtoto
- Mtoto kupatwa na madhara makubwa kwenye mzunguko wake wa damu.
TIBA ZAKE
James Herbal Clinic tuna dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili bila kujirudiarudia, nazo ni MULTI-CURE POWDER, NEOTONIC na NEOPOWDER ni dawa zenye uwezo mkubwa mno kuondoa tatizo la kisonono.
Je, unahitaji tiba? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626
Arusha-Mtaa wa Mbauda