JE, KUNA UHUSIANO GANI KATI YA UGONJWA WA KISUKARI(DIABETES) NA KIHARUSI(STROKE)?

Je, kuna uhusiano gani kati ya kisukari na kiharusi? Kisukari kinaweza kuongeza vihatarishi vingi vya magonjwa katika afya yako, ikiwa pamoja na ugonjwa wa kiharusi. Kwa ujumla watu wenye ugonjwa wa kisukari huelekea kupata ugonjwa wa kiharusi kwa urahisi sana kuliko watu wasiokuwa na kisukari.

13,948 Stroke Patient Stock Photos and Images - 123RF

NUKUU: Ugonjwa wa kisukari huathiri uwezo wa mwili kushindwa  kutengeneza homoni ya insulin au kutukuitumia kwa ufasaha. Kwakuwa homoni ya insulin ina jukumu kubwa la kuingiza glukozi ndani ya seli za mfumo wa damu, basi watu wenye ugonjwa wa kisukari mara nyingi huachwa wakiwa na sukari nyingi kwenye damu zao. Baada ya muda, sukari hii nyingi inaweza kuchangia kujenga mabonge ya damu au mafuta ndani ya mishipa ya damu inayopeleka damu maeneo ya shingo na ubongoni. Mchakato huu unafahamika kama atherosclerosis.

Kama matabaka haya yakizidi kuongezeka, basi yanaweza kusababisha kuta za mishipa ya damu kuwa finyu au kuziba kabisa. Damu inapokoma kububujika kwenye ubongo wako kwa sababu yoyote ile, basi utaona tatizo la kiharusi linajitokeza.

Je, Kiharusi Ni Nini?

Kiharusi ni ugonjwa ambao mishipa ya damu kwenye ubongo huharibika. Ugonjwa wa kiharusi una sifa ya mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na ukubwa wa mishipa ya damu iliyoharibika, ambapo mishipa ya damu ya  ubongo imeharibiwa, na ni tukio gani lililosababisha uharibifu huo.

Aina kuu ya kiharusi ni kuziba kwa mishipa ya damu, kupasuka kwa mishipa ya damu, na kuziba kwa muda kwa mishipa ya damu.

  1. Kuziba Kwa Mishipa Ya Damu(Ischemic)

Hali ya kuziba kwa mishipa ya damu ni aina ya kawaida ya ugonjwa wa kiharusi. Hali hii hutokea pale mishipa ya ateri inayosambaza damu yenye hewa ya oksijeni kwenye ubongo  inapoziba, kutokana na damu kuganda. Tatizo la kiharusi kutokana na mishipa ya damu kuziba limekuwa likiongezeka kwa kasi sana.

  1. Damu Kuvuja Kwenye Ubongo(Hemorrhagic Stroke)

Damu kuvuja kwenye ubongo hutokea pale mishipa ya damu inapopasuka. Inaonekana asilimia 15% ya ugonjwa wa kiharusi huwa ni kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo. Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi na asilimia 40% ya watu wenye ugonjwa huu hupoteza maisha yao.

  1. Damu Kuziba Kwa Muda Mfupi(Transient Ischemic Attack Au TIA)

Damu kushindwa kusafiri, wakati mwingine tunaita, “ministroke” kwasababu mtiririko wa damu kwenye ubongo huzibwa kwa muda mfupi kidogo na huwa haionekani kuwa ni tatizo la kudumu. Tatizo hili linaweza kukaa kwa dakika chache mpaka masaa kadhaa hivi, mpaka pale mishipa iliyoziba inapofunguka tena yenyewe. Hupaswi kupuuza, na unapaswa kuzingatia kabisa kuwa hilo ni onyo kwako.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Kutambua ishara na dalili za kiharusi ni hatua muhimu ya kwanza ya kupata msaada wa mtu kabla ya kuchelewa. Katika juhudi ya kusaidia watu kumbuka jinsi ya kutambua ugonjwa wa kiharusi, ambao inasimama kwa:

  • Mdomo kupinda
  • Mkono kushuka
  • Kushindwa kuongea

Dalili zingine ambazo zinaweza kuonyesha ishara za kiharusi ni pamoja na hizi zifuatazo, naomba usifuatilie vizuri kabisa:

  • Uso kufa ganzi
  • Mkono na mguu kufa ganzi hasa ikiwa ni upande mmoja
  • Kushindwa kushindwa kuelewa maneno wakati wa kuongea
  • Kushindwa kuona upande wa jicho moja au yote mawili
  • Kuhisi kizunguzungu
  • Kushindwa kutembea
  • Kichwa kugonga sana bila sababu yoyote

Je, Ni Sababu Gani Za Hatari Za Kiharusi?

Tatizo hili wengi hushindwa kulifahamu mapema, lakini yapo magonjwa ambayo mtu anaweza kuishi nayo na baadaye yakasababisha kiharusi, nayo ni:

  • Ugonjwa wa kisukari
  • Shinikizo la juu la damu(high blood pressure)
  • Matatizo ya kuganda kwa damu
  • Mafuta mengi kwenye damu
  • Ugonjwa wa siko seli
  • Matatizo ya mzunguko wa damu
  • Matatizo ya mishipa ya damu

 

Risk Factors for Stroke | Johns Hopkins Medicine

NUKUU: Uwezo wa kupata ugonjwa wa kiharusi ni mkubwa mno ikiwa kama una ugonjwa mmoja kati ya hayo au zaidi. Lakini mitindo mibaya ya maisha nayo inachangia kuwa na ugonjwa wa kiharusi, kama vile:

  • Lishe duni
  • Vyakula visivyokuwa na virutubishi
  • Uvutaji sigara au tumbaku
  • Kutokufanya mazoezi ya mwili
  • Ulevi wa pombe sana

Tatizo la kiharusi huongezeka kulingana na umri, hasa unapofikisha umri wa miaka 55. Wanaume wanaonekana kupatwa na ugonjwa wa kiharusi zaidi kuliko wanawake. Pia unapokuwa na ugonjwa wa shambulio la moyo, inaweza kukusababisha ukapatwa na ugonjwa mwingine wa kiharusi.

Je, Unawezaje Kupunguza Hatari Ya Ugonjwa Wa Kiharusi?

Unaweza kujiepuesha na ugonjwa wa kiharusi kwa kurekebisha mitindo yako ya ulaji. Zingatia sana mitindo yako ya maisha pamoja na tiba za asili na ujiulize mwenyewe nini unaweza kufanya ili kuepukana na ugonjwa wa kiharusi.

Je, Inakufaa Ubadiri Milo Yako?

Shinikizo la juu la damu(high blood pressure) pamoja na mafuta mengi kwenye damu inaweza kuongeza hatari ya ugonjwa wa kiharusi. Unaweza kupunguza shinikizo la damu na viwango vya kolestero kwa kufanya mabadiriko kwenye lishe. Jaribu utaraibu huo hapo chini wa lishe:

  • Punguza matumizi ya chumvi na mafuta
  • Kula vyakula samaki kwa wingi badala ya nyama
  • Kula zaidi vyakula vyenye sukari kidogo
  • Kula vyakula vingi vya mboga za majani, maharage na karanga
  • Tumia mkate uliotengenezwa kwa nafaka (brown bread) badala ya mkate mweupe
  1. Fanya Mazoezi

Kufanya mazoezi mara 5 kwa wiki kunaweza kukusaidia kupunguza hatari ya kupatwa na kiharusi. Zoezi lolote linalofanya mwili wako uweze kutembea ni zuri mno. Tabia ya kuwa unafanya mazoezi ya kutembea kwa mwendo kasi nayo husaidia mtu kuepuka ugonjwa wa kiharusi na huboresha mwili wako kwa ujumla.

  1. Usivute Sigara

Kama unavuta sigara, basi ongea na daktari wako vizuri juu ya mazoea yako ya kuvuta sigara ili akupe msaada wa kuacha kuvuata sigara. Hatari ya kiharusi huwa ni mara mbili zaidi kwa mtu anayevuta sigara.

Bearded Man Smoking A Marijuana Joint Stock Photo - Download Image Now -  Smoking - Activity, Marijuana - Herbal Cannabis, Smoke - Physical Structure  - iStock

NUKUU: Njia bora ya kuacha kuvuta sigara ni kujizuia kabisa. Kama hilo sio kwa ajili yako, zingatia sana kumuuliza daktari wako kuhusu misaada mbalimbali inayopatikana ili kukusaidia uachane na tabia ya uvutaji sigara.

Je, Mtizamo Unakuwaje?

Ingawa hutakuwa tiyari kuondoa vihatarishi vyote vya ugonjwa wa kiharusi, kuna mambo unaweza kufanya ili kupunguza hatari ya ugonjwa wa kiharusi na kuongeza nafasi yaw ewe kuishi muda mrefu.

Hapa kuna baadhi ya mambo unayopaswa kuyashikilia na kuzingatia:

  • Hakikisha unakuwa karibu na daktari wako ili akusaidie tatizo la kisukari
  • Jizuie kutumia pombe
  • Kama unavuta sigara, acha
  • Tengeneza mlo mzuri wenye afya
  • Fanya mazoezi mara kwa mara

 

Nikushukuru sana ndugu msomaji, naomba niishie hapa katika makala hii, tutaonana katika makala nyingine ijayo. Nikaribishe kipindi cha maswali na maoni.

Unahitaji huduma na ushauri? Wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252/0712181626.

Pia James Herbal Clinic tuna darasa letu endelevu katika Group la WHATSAP, hivyo unaweza kutuma namba yako ukaunganishwa na darasa letu.

Karibuni sana!