Ni kawaida kabisa mwanamke kupata mzunguko wa hedhi wa siku 23-38, na hata mabinti nao pia hupata mizunguko yenye urefu wa siku kama hizo. Lakini kumbuka kila mwanamke ana utofauti wake, na kila mzunguko wa mtu unaweza kutofautiana kuanzia mwezi mmoja hadi unaofuata.
Katika vipindi vya miezi kadhaa, mzunguko wako unaweza ukadumu kwa muda wa siku nyingi zaidi au chache kuliko ilivyokuwa mwanzo. Wakati mwingine unaweza ukawa na vipindi 2 vya hedhi ndani ya mwezi mmoja. Kama mizunguko yako ya hedhi ni mifupi, basi unaweza ukapata kipindi cha hedhi mwanzoni mwa mwezi au mwishoni mwa mwezi huo pasipokuwa na sababu zozote.
NUKUU: Lakini kama unapata hedhi tofauti kabisa na mzunguko wako wa kawaida na unaona kabisa kuwa unapata hedhi mara 2 kwa mwezi mmoja, kitu cha kwanza cha kufanya ni kutambua kama ni matone ya damu au damu ya hedhi kwa kufanya mambo yafutayo:
- Uonapo damu ya hedhi, unapaswa uchukue pedi uweke ukeni mwako. Damu inaweza kuwa nyeusi, au nyekundu, au ya kahawia au pinki.
- Kama unaona matone ya damu, bila shaka hutatokwa na damu nyingi wala hutaona damu ya hedhi na hutakuwa na haja ya kuweka pedi. Damu yam atone mara nyingi huwa ya kahawia au nyekundu.
NUKUU: Baada ya kutambua kuwa unatokwa na matone ya damu au damu ya hedhi, basi unaweza kuanza kuona nini kinaweza kusababisha muongezeko wa kuvuja kwa damu.
Je, Nini Husababisha Hali Hii?
Muongezeko wa damu kuvuja unaweza kusababishwa na mzunguko mfupi wa hedhi au matatizo ya afya ambayo husababisha uke kutoa damu.
Je, Vyanzo Vya Mzunguko Mfupi Wa Hedhi Vinakuwaje?
Kama mzunguko wako wa hedhi unapokuwa mfupi ghafla tu, basi inaweza kutokana na tatizo lolote kati ya haya yafuatayo:
- Yai kutopevuka
- Kufikia umri wa kukoma hedhi
- Tezi ya thyroid kutokufanya kazi
- Ubarehe
- Uvimbe kwenye kizazi au vifuko vya mayai
- Msongo wa mawazo
- Kuwa na uzito mkubwa au kupungukiwa uzito
- Matumizi ya madawa ya mpango wa uzazi
Je, Nini Kinamfanya Mwanamke Kutokwa Na Damu Nyingi Ya Hedhi?
Kama mara kwa mara una mzunguko wa hedhi usiobadirika, badiriko katika mzunguko wako kama vile kuona vipindi vya hedhi mara 2 ndani ya mwezi mmoja, yaweza kuwa dalili au ishara ambazo sio nzuri. Baadhi ya matatizo ya afya ya mwili wako yanaweza kusababisha kutokwa na damu nayo ni kama haya yafuatayo:
- Ujauzito
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Mimba kuporomoka
Je, Mambo Hatarishi Yanakuwaje?
Kama una historia yoyote juu ya uvimbe kwenye kizazi, vifuko vya mayai au hali ya hedhi kukoma kuanza mapema, basi unaongezeko vihatarishi vya kutokwa na damu ya hedhi mara 2 kwa mwezi mmoja.
Hivyo unapaswa umuone daktari endapo kama utaona mambo yafuatayo:
- Kuhisi maumivu maeneo ya tumbo la chini ambayo hukaa hata kwa siku 2
- Kutokwa na damu nyingi
- Kutokwa na matone ya damu baada ya kipindi cha hedhi kuisha
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kuhisi vichomi kama vile change
- Kuona mabonge ya damu wakati wa hedhi.
Je, Madhara Yake Yanakuwaje?
Moja ya madhara ya afya pale mwanamke anapotokwa na damu nyingi ya hedhi huwa ni kuishiwa damu mwilini, hali ambayo hujitokeza kutokana na kupungukiwa na madini ya chuma kwenye damu. Daktari anaweza kuangalia viwango vya madini ya chuma huku wengine wakiangalia sababu zinazopelekea wewe kutokwa na damu nyingi.
Dalili za kupungukiwa na damu mwili zinaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Uchovu mwilini
- Kichwa kuuma
- Mwili kulegea
- Kuhisi kizunguzungu
- Kushindwa kupumua vizuri
- Mapigo ya moyo kubadirika
Mpendwa msomaji naomba kuishia hapa katika makala hii, tutaonana katika makala nyingine. Nikaribishe kipindi cha maswali, karibuni sana.
James Herbal Clinic pia tunatoa masomo ya afya kila siku katika darasa letu kwa njia ya WHATSAP, hivyo unaweza ukatuma namba yako na ukaunganishwa na darasa au Group letu.
Unahitaji Huduma, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda Maua
Karibuni sana.