Je, Upendo Ni Nini?
Upendo wa kweli sio hisia; ni uamuzi wa kujitoa na kukidhi mahitaji ya mtu na usitarajie chochote. Upendo wa kweli hauna sababu, matarajio, au masharti. Huu ndio upendo wa dhati.
Ni chaguo la mtu kubaki kuwa umejitoa kabisa kwake bila kujali anachofanya au kutofanya. Na wengi leo wanakwama hapa sana hasa wanawake. Wengi wamekuwa wakitegemea wanapompenda mwanaume, matarajio yao ni kwamba huenda watafanyiwa kitu au mambo Fulani mazuri sana kama mrejesho wa kumpenda. Kwa mfano; anaweza kutarajia kupewa pesa, au kuletewa zawadi Fulani kila mara, na vitu vingine vingi tu. Huo sio upendo hata kidogo, na wala haujengi mahusiano ya ndoa kabisa, bali hiyo huwa ni tamaa.
Je, Ndoa Ni Nini?
Ndoa ni taasisi iliyowekwa na Mungu, uhusiano wa kudumu kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja. Ndoa ni mchakato, muunganiko wa vitu viwili tofauti na kuwa kitu moja—na hivyo kuwa katika upendo unaopendeza kabisa, uaminifu, na kujitoa kwa nadhiri ambayo hung’aa vyema katika maisha mafupi mazuri ya ulimwengu huu.
Mungu alianzisha ndoa; ni mali yake, si yetu. Ndoa ni watu wawili wasio wakamilifu wanaojitoa kwenye taasisi kamilifu, kwa kuweka nadhiri kamilifu kutoka katika midomo isiyokamili mbele za Mungu mkamilifu.
Kukosea kuoa au kuolewa ni kujenga muunganiko usio imara. Hapa kuna sababu 10 sahihi kwa nini unapaswa kuoa au kuolewa. Nazo ni hizi hasa:
- kwasababu ni mapenzi ya Mungu
- kuonyesha upendo wa Mungu kwa mtu mwingine
- kuonyesha upendo wako binafsi kwa mtu mwingine
- kutimiza mahitaji ya tendo la ndoa kwa njia ya ki Mungu
- tamanio la kuanza familia kwa muda wake sahihi
- ushirikiano
- kushiriki vitu vyote pamoja na mwenzako
- kufanya kazi pamoja ili kutimiza mahitaji ya kila mmoja.
- kuongeza uwezo wa kila mmoja
- kuimarishwa ukuaji wa kiroho
Misingi 10 ya Ndoa yenye Mafanikio
- Upendo
- Ukweli
- Kuamiana
- Kujitoa
- Heshima
- Unyenyekevu
- Maarifa
- Imani
- Uvumilivu
- Uimara kifedha
Jinsi Ya Kuchagua Mke/Mume
Katika kuchagua (mchumba) mwenzi, lazima uwe na mbinu hizi 8 katika kumchunguza na kumtambua. Mbinu hizi zitaongeza nafasi ya nyie wawili kuweza kuishi kwa mafanikio.
- Mabadiliko
Tambua kuwa huku ni kubadilika, si kufanana. Kubadilika ni sifa yenye nguvu katika mahusiano ambayo yatafanya kazi kuliko kufanana. Kufanana hulenga vitu vingapi ulivyonavyo ambavyo vinafanana. Ni muhimu lakini bado kutakuwa na tofauti kati yenu.
Kubadilika kwa upande mwingine ni uwezo wenu wa kuzoeana bila kujali tofauti zenu.
2. Uwezo Wa Kuhisi
Uwezo wa kuhisi ni usikivu kwa ajili ya mahitaji, maumivu, na matamanio ya wengine—uwezo wa kuhisi pamoja nao na kuupata ulimwengu kutoka katika mitazamo yao.
Upendo na ndoa ni mahusiano ya kukutanisha mahitaji ya mwingine. Ikiwa mmoja wenu au nyote wawili hamuhisi na kujali mahitaji ya mtu mwingine, basi kutakuwa na kutoridhika sana katika muunganiko wenu.
3. Uwezo Wa Kufanya Kazi Kupitia Matatizo
Kudai kuwa na uwezo wa kutatua kila shida ni uwongo. Lakini ndoa yenye mafanikio hutengenezwa na wanandoa ambao wameamua na kubaki kuwa watu wa kujitolea kutatua matatizo mengi kwa pamoja kadiri wawezavyo na kutafuta njia ya kukabiliana na yale wasiyoyaweza. Lakini kamwe usijifanye kuwa matatizo hayapo au ukayapuuza.
4. Uwezo Wa Kutoa Na Kupokea Upendo
Hii ni jambo la muhimu hasa kwa wanaume. Wanawake wengi hawana matatizo ya kutoa na kupokea upendo. Lakini wanaume wanashinikizwa na jamii kuamini kwamba lazima wabaki wagumu na kuficha mahitaji yao ya kihisia. Kwa mfano; mwanaume anaweza kuugua ugonjwa Fulani kama vile PID au UTI, lakini akawa mgumu kutibu ugonjwa huo.
Kwakuwa ninyi nyote lazima mpeane upendo, lazima pia mpate upendo kutoka kwa kila mmoja wenu. Kwahiyo lazima kila mmoja ampende mwenzake.
5. Utulivu Wa Kihisia
Hii ina maana kuwa na uwezo wa kudhibiti hisia zako na si kuziacha zikukimbie. Inamaanisha kudhibiti hasira yako na kutotoa visingizio vya milipuko ya hisia isiyokomaa.
Haya ni matokeo ya mapenzi zaidi kuliko akili. Kila mtu ana nguvu juu ya hisia zake ikiwa yuko tayari kuzidhibiti. Chunga ulinzi wa kudhibiti hisia zako.
6. Uwezo Wa Mawasiliano
Mawasiliano yanaweza kuharibu au kuimarisha uhusiano wowote. Urafiki na mapatano ni bidhaa bora za mawasiliano. Kwa hiyo ni lazima mume na mke wajue kuonyesha nia na hisia zao kwa upande mwingine kwa njia ambayo wangeelewa kikamilifu. Ni lazima pia wajue kwamba wanaume na wanawake wanawasiliana katika viwango tofautitofauti.
7. Kufanana Kati Ya Wanandoa Wawili
Kila ndoa inahusisha muunganiko wa watu wawili tofauti, lakini kunapaswa pia kuwa na baadhi mifanano tofauti: shauku ya kawaida, mapenzi ya kawaida, imani ya kawaida, au maoni sawa ya kiimani kwa mfano.
8. Malezi Ya Familia Yenye Kufanana
Sasa, watu wenye malezi tofauti wanaweza kuwa na ndoa zenye mafanikio lakini sifa hizi zinalenga kuongeza nafasi. Watu walio na malezi sawa ya familia watapata urahisi wa kuelewana kwa sababu kutakuwa na mambo machache ya kuzoea.
Zijue Aina 4 Za Upendo
- Upendo Vuguvugu
Upendo vuguvugu ni wa kiwango cha urafiki wa kawaida, yaani mapenzi unayokuwa nayo kwa mtu unayemfahamu na uliyemzoea. Kwa kawaida unaweza kuvutiwa na mtu mwingine anayeshiriki katika mambo yako sana au ambaye yuko katika ukoo lakini yupo karibu sana na wewe. Urafiki wa kweli ni kiungo cha maisha.
Rafiki ni mtu ambaye unaweza kushiriki naye mawazo yako ya ndani na utu wako wa ndani. Sababu moja ya urafiki kusitawishwa ni kwa sababu mtu unayehusika naye anahisi kwamba anapatana na wewe kwa kadiri fulani au nyingine.
Hii ni sawa kwa urafiki wa kawaida lakini sio vigezo vizuri vya kuchagua mwenzi au mchumba.
Mahusiano yenye mafanikio zaidi kwa kawaida huhusisha watu wawili ambao ni wapo tofauti au angalau tofauti sana kutoka kwa kila mmoja. Kwa sababu ya tofauti zao, wanasawazisha wao kwa wao, wakikamilishana na kuongezana badala ya kushindana jambo ambalo ni la kawaida miongoni mwa watu wenye tabia zinazofanana.
- Upendo Mwororo
Upendo mwororo ni upendo wa wazazi kuelekea kwa watoto wao na ule wa watoto kuelekea kwa wazazi wao. Ingawa upendo wetu kwa wazazi wetu na ndugu zetu ni wa kweli, bado kuna hisia ya msingi kwamba tunawapenda kwa sababu tunapaswa kuwapenda.
Wakati wowote hisia isiyo na upendo inapotokea ndani yako kuelekea kwa mshiriki yeyote wa familia, kwa kawaida hisia ya hatia itatokea. Hujisikii kupenda, lakini wakati huo huo, unahisi kwamba unapaswa kupenda.
Kwa mtazamo huu, basi, upendo mwororo ni sawa na upendo vuguvugu kwa kuwa unaweza kukuza hisia ya kushurutisha au kuwajibika na mambo mengine tu ukashindwa kumpenda mwenzako. Na huu upendo upo sana kwa wanawake wanaochumbiwa au kuolewa lakini akili na fahamu zao bado wameelekeza nyumbani wanakotoka. Atafunga harusi na kuingia nyumbani kwake lakini baada ya miezi michache ataomba kwenda kusalimia nyumbani kwao. Au wakati mwingine watu kama hawa wanapoolewa hawatapenda sana kwenda kuishi mbali na nyumbani kwao, hivyo anaweza kumshauri mchumba au mwenza wake wakajenge maeneo ya karibu na kwao. Unapenda, si kwa sababu unataka kupenda, bali kwa sababu inakupasa upende. Maana ni mpango wa Mungu.
3. Upendo Wa Kimapenzi
Upendo wa kimapenzi unakumbatia hamu ya ngono, tamaa, na mapenzi bila heshima katika utakatifu; furaha ya mwili ambayo inaacha kiasi na uwiano nyuma sana. Tofauti na upendo wa kweli, upendo wa kimapenzi huwa ni wa hisia kabisa.
Umejikita sana kwenye msisimko wa mwili katika hisia tano, yaani kuona, kunusa, kusikia, kuonja, na kugusa—na tamaa pamoja na vivutio vinavyoamsha hisi hizo. Ni kupe tu mfano; kijana wa kiume anaweza kuona umbo la mwanamke tu kama vile makalio, matiti, nywele, sura, au akasikia sauti nzuri inayompendeza yeye, au akahisi harufu ya marashi au manukato tu, basi mwili wake unaweza kuwaka na kumtamani mwanamke. Kadhalika hata kwa mwanamke.
Kwa sababu ni wa kimwili, hivyo upendo wa kimapenzi unadhibitiwa na athari za kemikali na mwingiliano ndani ya mwili. Mahusiano yaliyojengwa kwa upendo wa kimapenzi hudumu kwakuwa tu mvuto wa kimwili na tamaa ambayo viliwaunganisha watu kama wapenzi kuwa pamoja hapo awali.
4. Upendo Wa Kweli
Upendo wa kweli ni upendo wa dhati ambao unamaanisha upendo wa kimungu, upendo ambao Mungu anao kwa watu wake pamoja na upendo ambao watu wake wanamrudishia Yeye. Tofauti na upendo vuguvugu, upendo mwororo, basi upendo wa kweli haubebi wajibu wowote, hauna matarajio yoyote, na hautoi masharti yoyote.
Upendo wa kweli ni upendo usio na masharti maana ni upendo wa kimungu yaani agape. Upendo wa kweli ni kujitoa kabisa kwa ajili ya mtu. Kama vile Kristo alivyojitoa kwa ajili ya ulimwengu, vile vile yule mwenye upendo wa kweli ambao ni upendo wa agape kwa tafsiri nyingine, anapaswa kuwa mtu wa kujitoa kabisa kwa ajili ya mwenzake. Hatimaye, upendo wa dhati ni chaguo. Haitegemei hisia, bali uamuzi wa makusudi. Biblia inasema waziwazi kwamba Mungu anatupenda lakini haituambii kamwe kwa nini anatupenda. Hakuna “kwa nini.”
Kwa sababu ni uamuzi—chaguo la makusudi—basi upendo wa kweli ni wa kudumu. Tofauti na “upendo” unaotegemea hisia, hivyo upendo wa kweli haubadiliki kamwe. Mlivyoanza kama wachumba ndivyo mtakavyokuwa mpaka wazee wanandoa. Sema aminaa.
Hapa hakuna tena kwamba eti ili upendo uwepo, sharti ununuliwe simu smart phone, au ukapelekwe saluni kusuka nywele za bei, au ukanunuliwe nguo za thamani, nk. Hapa anakaa Mungu, sio mwanadamu tena na ndio maana ukaitwa upendo wa kweli. Ikosekane simu smart phone, haina shida kwa mwenye upendo wa kweli, ikosekane suti, hakuna shida kwa mwenye upendoa wa agape, mana yupo Mungu mwenyewe.
Hitimisho
Hakuna ndoa yenye mafanikio inayotokea tu—eti watu wawili wameanza kama wapenzi tu chuoni, au mtandaoni wa facebook, Instagram, whatsap, au barabarani, kwenye haisi, au sokoni, nk. Na ubora wa kila ndoa unategemea ubora wa wachumba ndani yao. Pande zote mbili lazima zifungue maarifa na zijitolee kabisa kwa ajili ya ndoa iliyo Zaidi ya kujitolea kwao wenyewe.
Hivyo basi, usiinuse ndoa tu kwa kuanza na mpenzi au wapenzi, maana kwa mazoea ya tabia hii, kwa kukosa utii kwa Mungu kwa kuvunja amri zake na kuyaacha maagizo yake, ndipo adhabu na mateso huturudia sisi katika jamii. Magonjwa mengi katika jamii kama vile maambukizi ya magonjwa ya zinaa au PID, saratani ya matiti au ya kizazi, ugumba au kushindwa kupata ujauzito, nk, yanatokana na maovu tunayoyafanya kwa kuvunja amri za Mungu na kuacha maagizo yake.
Ikiwa kama tunapenda kuepukana na mateso haya, basi inatupasa kumugeukia Yeye maana maandiko yanasema hivi:
Hebu sema, amina! Suluhisho lipo na kwamba, tukiyashika maagizo ya Mungu, Yeye hatatia ugonjwa wowote juu yako, iwe fangasi, PID, saratani ya kizazi wala ugumba juu yako.
Nipende kuwashauri ndugu watu wa Mungu kwamba, wewe kama ni mwanandoa kweli hebu jaribu kujitafakari tu vizuri, je huo upendo ulioubeba ni upendo wa dhati kweli au ni upendo wa vuguvugu au mwororo au wa kimapenzi tu? Jitafakari! Na kama sio wa dhati, basi piga hatua muombe Mungu akupatie upendo wa dhati ili uweze kujenga ndoa yako.
Na wewe kama ni dada au kaka(mchumba) haijarishi uko chuoni, kazini, au popote pale ulipo, jaribu kujitafakari, je, inampendeza Mungu kweli kuanza mahusiano kabla ya kufunga ndoa? Je, ni mpango wake au ni wako tu?
Je, yawezekana dhambi tunazofanya za uzinzi, uasherati, tamaa mbaya, nk, ndio zikawa vyanzo vya magnjwa yanayotupata, au mateso yanayotusmbua kila siku au matatizo ya kiuchumi, nk?
Hebu tumugeukie Mungu wetu, Yeye anatupenda atatusamehe na atatuponya na magonjwa yote.
Naomba niishie hapa wapendwa nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yenu, tutakutana katika Makala nyingine.
Unahitaji huduma au ushauri, basi tupigie kwa namba hizi: 0768559670 au 0712181626
Arusha-Mbauda.