JE, KUTOKUSAGWA KWA CHAKULA TUMBONI YAWEZA KUWA CHANZO CHA MAGONJWA MWILINI MWAKO? JE, NINI DALILI NA MADHARA YA TATIZO HILI?

Ndugu mpendwa, na ieleweke kuwa hali ya chakula kutokumeng’enywa tumboni mwako sio ugonjwa, bali ni baadhi ya dalili zinazokupata, kwa mfano;  tumbo kuuma na kujaa mara baada tu unapoanza kula chakula. Ingawa tatizo hili linaonekana kuwa la kawaida sana, lakini tatizo hili linaweza kutokana na vyanzo mbalimbali. Dalili za chakula kutokumeng’enywa unaweza kuzihisi mara kwa mara kila siku.

 

Hali ya kutokumeng’enywa kwa chakula tumboni inaweza kuwa dalili ya ugonjwa mwingine wa usagaji chakula tumboni mwako.

 

Je, Nini Dalili Za Tatizo Hili?

 

 

Watu wengi wenye tatizo hili wanaweza kuwa na dalili moja au zaidi, nazo huwa kama ifuatavyo:

 

  • Tumbo kujaa gesi wakati anapokula chakula

 

  • Tumbo kujaa gesi muda mrefu

 

 

  • Kuhisi maumivu ya tumbo la juu

 

  • Kuhisi kiungulia juu ya tumbo

 

 

  • Tumbo kuunguruma sana mara kwa mara na kuhisi maumivu chini ya kitovu

 

  • Kuhisi kichefuchefu na kutaka kutapika

 

 

NUKUU: Wakati mwingine watu wanaosumbuliwa na tatizo hili pia hupatwa na kiungulia, lakini kumbuka kuwa kiungulia au chakula kutokumeng’enywa tumboni huwa ni hali mbili tofauti. Kiungulia huwa ni moto au maumivu unayoyahisi katikati ya kifua chako ambayo yanaweza kupenya mpaka kwenye shingo yako au mgongoni mwako wakati ama baada ya kumaliza kula.

 

Je, Nini Husababisha Chakula Kutokumeng’enywa Tumboni?

 

Chakula kutokusagwa au kumeng’enywa tumboni husababishwa na vyanzo vingi. Mara nyingi hali hii hutokana na mtindo wa maisha ya muhusika mwenyewe, hasa katika matumizi ya vyakula, vinywaji au madawa ya vidonge anayoyatumia. Visababishi vya tatizo hili huwa kama ifuatavyo:

 

  • Mazoea ya kula kupindukia au kula haraka haraka bila kujali kutafuna chakula vizuri

 

 

  • Vyakula vyenye mafuta mengi sana, kama vile chips, roast, nk.

 

 

  • Vyakula vilivyokobolewa kama vile, ugali wa sembe, maandazi, chapati, nk

 

  • Utumiaji wa nyama mara kwa mara

 

 

  • Vinywaji vyenye caffeine nyingi,kama vile  pombe, kahawa, nk

 

  • Ulaji wa chokleti,

 

 

  • Uvutaji sigara

 

  • Kuwa na wasiwasi

 

  • Matumizi ya madawa ya vidonge vya antibiotic au vyenye kupunguza maumivu mwili mwako kama vile panadol, nk. Yafaa sana kupata ushauri kwanza wa daktari kabla hujatumia madawa hayo.

 

Wakati mwingine hali ya chakula kutokumeg’enywa tumboni husababishwa na magonjwa au matatizo yanayokuwa tumboni mwako kama vile:

 

 

  • Vidonda vya tumbo

 

  • Uvimbe tumboni(Gastritis)

 

 

  • Mawe ya figo

 

  • Kuvimba kwa kongosho

 

 

  • Saratani ya tumbo

 

  • Utumbo kuziba

 

 

  • Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye utumbo mwembamba(intestinal ischemia)

 

 

Je, Nini Madhara Ya Chakula Kutokusagwa Tumboni?

 

 

Kwa kawaida tatizo hili linapodumu kwa muda mrefu bila kufanyiwa ufumbuzi, basi linaweza kusababisha madhara yafuatayo katika mwili wako:

 

  1. Mzunguko wa damu kuharibika na kuwa mdogo

 

  1. Mgongo au kiuno kuuma

 

 

  1. Miguu, au mikono kufa ganzi

 

  1. Mwili kuchoka mara kwa mara

 

 

  1. Kukosa hamu ya kula

 

  1. Macho kushindwa kuona vizuri

 

 

  1. Mapigo ya moyo kwenda mbio

 

  1. Kichwa kuuma

 

 

  1. Kutojisikia raha na kukosa amani

 

 

Tiba Zake

 

 

James Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya chakula kutokusagwa tumboni, nazo ni CARD HERB, ASALI na FRESH HERB.

 

Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hii: 0752389252/0712181626

 

 

Arusha-Mbauda Pepsi

 

Karibuni sana

4 thoughts on “JE, KUTOKUSAGWA KWA CHAKULA TUMBONI YAWEZA KUWA CHANZO CHA MAGONJWA MWILINI MWAKO? JE, NINI DALILI NA MADHARA YA TATIZO HILI?

      1. Nahitaji hii dawa tatizo hili limenianza ila sio muda mrefu linaninyima hata usingizi wakati mwingine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *