Wanawake wengi hupatwa na hali ya tumbo kuuma kama vichomi fulani kabla au wakati wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi. Walaki pia mwanamke anaweza kupatwa na change la tumbo.
Maumivu ya tumbo baada ya hedhi kitaalamu tunaita, “secondary dysmenorrheal”. Huwa ni hali ya kawaida kwa mwanamke anapofikia umri mkubwa. Tutaielezea baadaye kwa upana hali hii ili tujue vyanzo vyake.
Je, Unaweza Kuyahisi Vipi Maumivu?
Maumivu ya tumbo baada ya hedhi mara nyingi husikika maeneo ya tumbo la chini na mgongoni. Unaweza ukahisi maumivu pia kwenye maeneo ya nyonga na mapajani.
Hali ya maumivu haya inaweza kuambatana na kichefuchefu na maumivu ya kichwa pia. Pia unaweza ukahisi tumbo kujaa gesi, kukosa choo au kuharisha.
Maumivu yanaweza kuwa makali na yakaendelea kwa muda mrefu kuliko maumivu ya kawaida yanayojitokeza wakati wa hedhi. Maumivu yanaweza pia kuanza mapema kwenye mzunguko wako wa hedhi badala ya kuanza kabla ya kipindi cha hedhi kinachofuata.
Maumivu au vichomi hivi mara nyingi huwa sio vikali sana. Hata hivyo, ni muhimu sana kuvisikiliza hasa pale vinapokaa kwa muda mrefu.
Je, Nini Husababisha Maumivu Haya?
Wakati mwingine maumivu baada ya hedhi huwa sio makali sana. Lakini kama una maumivu yasiyo koma yanayodumu muda mrefu kuliko mzunguko wako wa hedhi, basi inaweza ikawa ishara au dalili kwamba una tatizo mwilini mwako.
Hapa nitapenda nielezee visababishi mbali mbali vya maumivu yanayompata mwanamke baada ya kutoka katika kipindi cha hedhi:
- Ngozi Ya Ndani Ya Tumbo La Uzazi(Endometriosis)
Endometriosis ni ugonjwa ambao hujitokeza wakati ngozi ya juu ya tumbo la uzazi inapovimba . Hali hii inaweza kusababisha maumivu kabla, au baada ya kipindi cha hedhi. Maumivu haya yanaweza kuambatana na uvimbe au maumivu ya nyonga.
NUKUU: Maumivu yanaweza yakawa makali, na yanaweza kujitokeza wakati unapofanya tendo la ndoa au baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa au wakati unapojisaidia haja kubwa au haja ndogo. Maumivu haya endelevu unaweza kuyahisi maeneo ya tumbo la chini au mgongoni.
Dalili za ugonjwa wa Endometriosis huwa kama ifuatavyo:
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
- Maumivu wakati unapojisaidia haja kubwa au ndogo
- Kushindwa kubeba ujauzito(ugumba)
- Kuhisi uchovu
- Kuhara au kukosa choo
- Tumbo kujaa gesi
- Kichefuchefu
- Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja
- Maumivu ya tumbo kabla, au wakati wa hedhi au baada ya hedhi ambayo yanaweza kuambata na maumivu ya tumbo la chini au mgongoni.
- Uvimbe Katika Mlango Wa Kizazi(Adenomyosis)
Adenomyosis ni uvimbe usababishwao na kuota kwa tishu zisizo za kawaida katika mlango wa uzazi. Badala ya kuota ndani ya tumbo la uzazi, tishu hizi huota kwenye mizuli ya tumbo la uzazi. Dalili zake huwa kama ifuatavyo:
- Kutokwa na damu muda mrefu wakati wa hedhi
- Kuhisi maumivu makali ya nyonga wakati wa hedhi
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Damu kuganda wakati wa hedhi
- Kuhisi kitu kigumu maeneo ya tumbo la chini
- Maambukizi Katika Via Vya Uzazi Au PID
Ugonjwa wa PID kama tulivyokuwa tujifunza siku zote, husababishwa na bakteria ambao huambukiza viungo vya uzazi. Bakteria hawa wanaweza kuenea kutoka kwenye uke na kuelekea kwenye tumbo la uzazi, vifuko vya mayai, au mirija ya uzazi.
Hayo ndio maeneo ambayo huathiriwa sana na maambukizi katika via vya uzazi ikiwa kama tatizo hilo halitatibiwa mapema.
PID inaweza isionyeshe dalili hapo mwanzo. Lakini baadaye dalili zinaweza kuonekana nazo huwa kama ifuatavyo:
- Maumivu ya nyonga au ya tumbo la chini
- Kutokwa na uchafu mwingi ukeni
- Kutokwa na damu nyingi wakati wa unapofanya tendo la ndoa
- Kuhisi kama vile una homa au mafua
- Kushindwa kukojoa kwasababu ya maumivu
- Tumbo kuunguruma
NUKUU: PID ni ugonjwa ambao unatibika kwa MULTICURE POWDER, FRESH HERB na VITAMAKA.
Japokuwa PID mara nyingi husababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, lakini kila mwezi wako anahitaji kupata vipimo kwanza kabla hujamuingia ili kuhakiki magonjwa ya zinaa ili kuzuia maambukizi yasijirudie.
- Uvimbe Kwenye Tumbo La Uzazi(Uterine Fibroid)
Uvimbe kwenye kizazi huwa sio saratani bali huwa ni vivimbe vinavyoota kwenye tumbo la uzazi. Wnawake wenye uvimbe mara nyingi huwa hawaonyeshi dalili zozote zile mpaka pale uvimbe unapokuwa mkubwa.
Tumbo la uzazi linaweza likavamiwa na vivimbe kila mahali na likawa na muonekano kama unavyoona hapo juu.
Dalili za uvimbe kwenye tumbo la uzazi huja kutokana na maeneo ulipo, ukubwa wake na idadi ya vivimbe. Dalili zinapojitokeza huwa kama ifuatavyo:
- Maumivu makali ya tumbo
- Vipindi vya hedhi kubadirika badirika
- Kutokwa na damu nyingi ya hedhi kwa muda mrefu
- Kukojoa mara kwa mara au kushindwa kujoa
- Maumivu sehemu za nyonga
- Kukosa choo
- Kutopata ujauzito(ugumba)
- Kichwa kuuma au miguu kuuma
NUKUU: Uvimbe wa Fibroid hutibiwa kwa REDEEMER, VITAMAKA na FRESH HERB.
- Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai(Ovarian Cysts)
Vivimbe ambavyo huota ndani ya vifuko vya mayai vinaweza kusababisha kutokwa na damu kabla ya muda wa hedhi au kuhisi maumivu makali ya tumbo la chini. Vivimbe vingi kwenye mfuko wa mayai hutoweka tu bila kutumia tiba. Hata hivyo, vivimbe vinapokuwa vikubwa vinaweza kusababisha maumivu ya nyonga maeneo ya tumbo la chini.
Unaweza ukaona hapo juu kwenye picha upande wako wa kulia jinsi vivimbe kwenye vifuko vya mayai vinavyokuwa na muonekano huo.
NUKUU: Tumbo lako linaweza kuonekana kuwa limejaa, zito au kuwa linaunguruma. Nakushauri umuone daktari mapema ikiwa kama unapata maumivu makali ya tumbo au nyonga, homa, au kutapika.
NUKUU: Vivimbe kwenye mayai hutibiwa kwa MULTICURE PODWER, CARD HERB na VITAMAKA.
- Mimba Kutunga Nje Ya Mfuko Wa Uzazi(Ectopic Pregnancy)
Mimba kutunga nje ya kizazi ni hali ambayo hujitokeza pale yai lilirutubishwa linapojipachika lenyewe mahali fulani nje ya tumbo la uzazi(uterus).
Unaweza ukaona pia hapo juu upande wa kulia kwenye mrija wa uzazi jinsi yai baada ya kurutubishwa likajikita hapo na kikaanza uumbika kiumbe nje ya tumbo la uzazi.
Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi zinaweza kuanza kama mimba ya kawaida. Hata hivyo unaweza kuendelea kupatwa dalili kama zifuatazo:
- Kutokwa na damu nyingi ukeni
- Maumivu makali maeneo ya tumbo la chini au kwenye nyonga
- Mabega kuuma
NUKUU: Damu itatoka nyingi ukeni endapo kama mrija wa uzazi utapasuka. Hali hii huambatana na maumivu ya kichwa, kuhisi kizunguzungu, na mshituko. Uonapo dalili hizi, hakikisha unafika hospitali haraka bila kuchelewa.
Kumbuka tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi linaweza kutatuliwa kwa kufanyiwa upasuaji.
- Yai Kujipachika
Unapokuwa mjamzito, ngozi ya juu ya tumbo la uzazi inaweza kubanduka na kusababisha kutokwa na matone ya damu nyepesi. Hali hii hujulikana kama kutokwa na damu kwa ajili ya yai kujipachika. Mara nyingi huonekana siku 7-14 baada ya kupata ujauzito.
NUKUU: Maumivu ya tumbo yanaweza pia kujitokeza hasa sehemu ya kwanza ya ujauzito wako. Chukua kipimo cha ujauzito hapo nyumbani kwako, pima mkojo ili kuhakiki kuwa una ujauzito.
Mpendwa msoamji hivyo ndio visababishi vinavyomfanya mwanamke kujisikia maumivu wakati wa hedhi, kabla ya hedhi au baada ya hedhi. Unahitaji huduma, tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha Mbauda
Karibuni sana
Tunaomba mutufahamishe zaidi ili tujinusuru na haya maradhi hatari
Dawa gani itawezana na hili tatizo
Tatizo gani kaka Manfed?