JE, KWANINI UGONJWA WA PID UNAWEZA KUJIRUDIA RUDIA?

Maambukizi ya ugonjwa wa PID wakati mwingine yanaweza kusababisha matatizo ya kudumu, hasa ikiwa kama ugonjwa haujatibiwa haraka. Lakini watu wengi wenye ugonjwa huu wanaokamilisha dozi zao kwa dawa za asili, wao huwa hawana matatizo ya muda mrefu.

611 Pelvic Inflammatory Disease Stock Photos, Pictures & Royalty-Free  Images - iStock

NUKUU: Wakati mwingine unaweza kuona hali ya PID inajirudia. Na ufahamu kwamba ugonjwa unaweza kujirudia kama maambukizi ya hapo mwanzo hayakutubiwa yakaisha. Hii mara nyingi ni kwa sababu hukukamilisha dozi ya matibabu yako au mwenzi wako hakuwahi kupata vipimo na matibabu.

Kama maambukizi ya PID yakiharibu mji wa mimba au mirija ya uzazi, inaweza kuwa rahisi bakteria kuathiri maeneo haya baadaye, na kuyafanya yaweze kuendeleza hali ya ugonjwa tena. Hakikisha unakuwa makini sana pale unapopata vipimo na kukuta maeneo kama mirija ya uzazi, nk kuwa vimeharibika!

Ugonjwa wa PID unapokuwa unajirudia huambatana na vihatarishi vya kutokupata ujauzito, navyo huwa kama hivi ifuatavyo:

  1. Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai

PID wakati mwingine inaweza kusababisha mkusanyiko wa majimaji au uteute wenye maambukizi unaoitwa vivimbe maji, hasa kwenye mirija ya uzazi au vifuko vya mayai.

Pathology of the adnexa | Radiology Key

NUKUU: Vivimbe maji vinatibiwa kwa dawa za antibiotic kwa ajili ya kuua bakteria, lakini wakati mwingine upasuaji unaweza kuhitajika ili kutoa majimaji hayo katika maeneo hayo. Uteute huo pia unaweza wakati mwingine kutolewa kwa kutumia sindano.

  1. Maumivu Ya Nyonga Ya Muda Mrefu

Wakati mwingine PID inaweza kusababisha maumivu sugu ya muda mrefu maeneo ya nyonga na tumbo la chini, ambayo yanaweza kuwa vigumu kuyavumilia na yanaweza kusababisha matatizo mengine zaidi, kama vile msongo wa mawazo na kukosa usingizi.

Pelvic Inflammatory Disease: Risk Factors, Symptoms & Treatments

NUKUU: Kama ukiendelea kuwa na maumivu sugu ya nyonga, unaweza kupewa vidonge vya kutuliza maumivu ili kukusaidia kuweza kuvumilia dalili ulizo nazo. Vipimo vya kuweza kubaini tatizo vinaweza kufanyika.

Kama vidonge vya maumivu vikishindwa kuondoa maumivu, basi itakubidi ufike kwa wataalamu wahusika ili uweze kusaidiwa.

  1. Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi

Mimba kutunga nje ya kizazi ni pale yai lililorutubishwa linapojipachika lenyewe nje ya mji wa mimba, mara nyingi kwenye mirija ya uzazi.

Kama PID ikiathiri mirija ya uzazi, basi inaweza kutia makovu kwenye njia ya mirija ya uzazi, na kuyafanya mayai yashindwe kupita.

Ectopic Pregnancy - Expert Chikitsa

NUKUU: Kama yai lililorutubishwa likikwamba na kuanza kukua ndani ya mrija, linaweza kusababisha mrija kupasuka, hali ambayo wakati mwingine inaweza kupeleka kutokwa na damu nyingi tumboni. Kama ukipimwa ukakutwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi, unaweza ukapewa dawa ili kulizuia yai yasiendelee kukua au unaweza kufanyiwa upasuaji ili kuondoa yai hilo.

  1. Utasa Au Ugumba

Kadiri vihatarishi vya mimba kutunga nje ya kizazi vinavyozidi kuongezeka, basi makovu au vivimbe kwenye mirija ya uzazi yanaweza kuzuia kabisa kupata ujauzito ikiwa kama mayai hayawezi kupita kwa urahisi ndani ya mji wa mimba.

What Is Pelvic Inflammatory Disease (PID)? Symptoms, Causes, Diagnosis,  Treatment, and Prevention | Everyday Health

NUKUU: Unaweza kuwa mgumba kutokana na  matokeo ya ugonjwa wenyewe. Kuna vihatarishi vikubwa vya ugumba ikiwa kama ukichelewa kutibu ugonjwa wa PID au kama ugonjwa ukiwa unajirudiarudia.

Nipende kuishia hapa katika makala hii, nikaribishe tu kipindi cha maswali na maoni kwa yeyote.

Unahitaji huduma, unaweza kutupigia kwa namba zetu hizi: 0752389252 au 0712181626.

Lakini pia tuna darasa letu kwa GROUP la WHATSAP ambapo tunajifunza masomo mbalimbali ya afya, hivyo unaweza ukatuma namba yako ukaweza kuunganishwa na darasa letu.

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *