Maambukizi katika njia ya mkojo ambayo kitaalam tunaita UTI ni tatizo linalokuwa miongoni mwa wanawake ambalo husababisha na ukuaji usiohitajika wa bakteria aina ya E.Coli wanaokuwa kwenye mkojo.
Wakati bakteria hawa wanapoondoka mpaka kufika kwenye njia ya mkojo, basi inaweza kutokea maambukizi mabaya ambayo hutambulikana kwa dalili kama vile homa, kichefuchefu, baridi, kutojisikia vizuri na kuhisi hali ya kuwaka moto pale unapokuwa ukikojoa.
NUKUU: Tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo huathiri wanaume na wanawake lakini wanawake ndio hupatwa kwa urahisi sana na maambukzi haya kwakuwa njia yao ya mkojo ni ndogo sana ukilinganisha nay a wanaume. Kwahiyo, wanawake wanapaswa kuwa na tahadhari kubwa sana ili kujiepusha na maambukizi haya.
Je, Inakuwaje Kati Ya Maambukizi Katika Njia Ya Mkojo Na Kutokupata Ujauzito?
Maambukizi katika njia ya mkojo huathiri viungo vya mwili kama vile figo, ini, mfuko wa uzazi(uterus), kibofu cha mkojo ambacho kimsingi hufanya kazi ya kuondoa uchafu wakati mwili unapokuwa ukirekebisha joto la mwili. Kama maambukizi yakiendelea au yakawa yanajirudia mara kwa mara hasa yanapokuwa yakiathiri njia ya juu ya mkojo(yaani figo, mfuko wa uzazi(uterus), mirija ya uzazi), basi yanaweza kuathiri uwezo wa mwanamke kubeba ujauzito.
NUKUU: Hali hii pia inatiwa PID au maambukizi katika via vya uzazi ambayo yanaweza kuharibu vibaya mirija ya uzazi. Ugonjwa sugu wa figo unaweza kuathiri sehemu zingine za mwili na unaweza kuathiri afya yako na mchakato wa upevushaji mayai hali ambayo inaweza kuathiri mchakato wa utungaji mimba.
Je, Maambukizi Katika Njia Ya Mkojo Kwa Wanaume Yaweza Kusababisha Hali Ya Ugumba?
Maambukizi katika njia ya mkojo au UTI kwa wanaume pia yanaweza kusababisha hali ya ugumba. Bakteria hawa huenea tezi ya prostate pamoja na viungo vingine vya uzazi ambavyo vinaweza kusababisha shahawa au mbegu za mwanaume kuwa nyepesi na kushindwa kusafiri kwa mwendo wa kasi.
Maambukizi yanaweza kuathiri sehemu kama vile korodani, na mirija ambapo shahawa hupita. Wakati mwingine yapo magonjwa mengine kama vile kisukari yanaweza kumfanya mwanaume kupatwa na maambukizi ya UTI kwa urahisi na kupelekea kushindwa kumpatia ujauzito mwanamke. Hata hivyo tatizo hili linaweza kutiwa tatrtibu kwa njia ya madawa ya asili.
Je, Ni Njia Gani Rahisi Unazoweza Kutumia Ili Kujikinga Na Maambukizi Haya?
Ikiwa kama una maambukizi katika njia ya mkojo au UTI, basi unapaswa kutumia njia hizi zifuatazo:
- Yafanye Maji Ya Kunywa Kuwa Rafiki Wako Wa Karibu
Kunywa maji mengi na utumie matunda yanayoweza kukusaidia kuondoa sumu mwilini kama vile nanasi au machungwa, nk. Maji hupunguza makali ya mkojo na kuufanya kuwa na asidi kidogo na kuwa na rangi nyeupe. Kwa kutumia njia hii mgonjwa hata hisi maumivu ya tumbo la chini au muwasho wakati anapokojoa.
- Fanya Usafi
Fanya usafi vizuri kabisa, huku ukijiepusha na utumiaji wa mabafu ya pamoja kwakuwa maambukizi huenea kwa kasi mara kwa mara katika shughuli za kawaida. Unapofanya usafi maeneo ya uke, unapaswa kuosha huku ukifuta kutoka mbele kuelekea nyuma ili kuzuia bakteria wanaokuwa maeneo ya njia ya haja kubwa wasiingie ukeni au katika njia ya mkojo.
- Kukojoa Mara Kwa Mara
Usiuzuia mkojo. Tumia bafu popote unapohisi kwenda kukojoa. Hii haitaachia sumu peke yake tu bali itaondoa uzito unaokuwa kwenye kibofu cha mkojo na kukupatia unafuu kutokana na maumivu ya tumbo la chini.
- Vaa Chupi Nzuri
Usivae chupi zenye kubana kwakuwa bakteria hupenda kukaa kwenye maeneo yenye vuguvugu. Kwahiyo jitahidi kuwa unabadirisha nguo zako za ndani mara kwa mara ili kuyaweka maeneo hayo kuwa katika hali ya usafi.
- Epuka kutumia sabuni zenye marashi makali, cream za antiseptic, marashi yenye harufu kali, nk
- Hakikisha unatumia nanasi kwa wingi sana ili kuzuia ukuaji wa bakteria mwilini.
Je, Unahitaji kuondoa tatizo la UTI sugu? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626. James Hebal Clinic pia tunatoa masomo ya afya kila siku katika mitanadao yetu ya TELEGRAM na WHATSSAP. Hivyo unaweza kutuma namba zako za Telegram au Whatssap na tukakuunganisha na JUKWAA zetu ili upate huduma ya afya.
Karibuni sana