Ndugu msomaji naomba upitie makala hii kwa makini ili uweze kujifunza madhara yatokanayo na maambukizi ya fangasi ukeni.
Maambukizi ya fangasi ukeni ni ya kawaida kabisa japokuwa ni mabaya kama jinsi yasivyohitajika kuwa kwa mtu. Katika wanawake 4, basi wanawake 3 wanaweza kuwa na maambukizi ya fangasi ukeni kwa umri wowote wanaokuwa nao maishani mwao.
NUKUU: Maambukizi ya fangasi ukeni husababishwa na bakteria aina ya Candida albicans, aina ya kawaida kabisa ya bakteria wa fangasi ambao huishi pamoja na bakteria wengine wa wazuri wa asili wanaokuwa kwenye utumbo, na kwenye idadi ndogo inayokuwa ukeni.
Bakteria wa fangasi aina ya Candida albicans huwa hawana madhara zaidi, bali ikiwa kama uwiano mzuri utakuwa umeharibika, basi ndipo idadi ya bakteria wa fangasi wataongezeka na dalili zake zitaendelea kuwepo ikiwa ni:
- Muwasho
- Wekundu kwenye mashavu ya uke
- Mashavu ya uke kuvimba na kujisikia vibaya katika maeneo hayo
- Kuhisi hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa
- Kutokwa na uchafu mweupe kama maziwa mgando.
NUKUU: Maambukizi ya fanagsi ukeni yenyewe hayasababishi hali ya ugumba kwa mwanamke. Lakini kile ambacho wanawake wengi hushindwa kukitambua na hata wataalamu wengine wa magonjwa, ni kwamba maambukizi ya fangasi ukeni yenye kujirudia rudia, au bakteria wa asili wanaolinda eneo la uke wanapokosa uwezo kabisa, basi wanaweza kuathiri kabisa uwezo wa mwanamke kupata ujauzito.
Bakteria Wa Asili Wanaokuwa Ukeni Huamua Jinsi Gani Mwili Wa Mwanamke Unavyoweza Kupokea Shahawa Au Mbegu Za Mwanaume.
Maambukizi ya fangasi ukeni hubadiri muonekano wa ute unaotoka kwenye shingo ya kizazi na kufanya mbegu kushindwa kuingia na kuufikia mji wa mimba(uterus). Katika magonjwa ya maambukizi ya mara kwa mara, bakteria wanaolinda uke huwa hawapo katika uwiano sawa kiasi kwamba shahawa au mbegu za mwanaume hushindwa kuufikia mlango wa shingo ya kizazi.
NUKUU: Uwiano kati ya asidi na alkali ya bakteria wa asili wanaokuwa ukeni mwa mwanamke, unapaswa kuwa kati ya 3.8 hadi 4.5(yaani asidi iwe nyingi) katika mzunguko wa hedhi, na kuongezeka kati ya alkalinie 7 hadi 14 katika kipindi cha yai kupevuka.
NUKUU: Inapotokea hali ya maambukizi ya mara kwa mara ya fangasi ukeni, basi mwili wa mwanamke hupambana kwa kutengeneza mazingira yenye asidi nyingi zaidi, ambayo baadaye huwa adui na mbegu za mwanaume, hata katika kipindi cha yai kupevua. Hali hii ya kutokuwa na uwiano sawa inaweza kuathiri kabisa uwezo wa mwanamke kupata ujauzito.
Je, Kurekebisha Kila Mara Uwiano Wa Asidi Ya Bakteria Wa Asili Wanaokuwa Ukeni Inaweza Kuwa Jambo La Muhimu?
Kama mwanamke anapata matibabu endelevu kwa ajili ya maambukizi ya fangasi yanayojirudia mara kwa mara bila kuweka mlingano sawa wa bakteria wa sili wanaokuwa ukeni, basi inaweza kujenga mazingira ambapo bakteria wabaya husitawi kwasababu hakuna bakteria wa kutosha wa ulinzi.
Kama unasumbuliwa na maambukizi ya fangasi ukeni mara kwa mara, basi jambo la muhimu unalotakiwa kulifanya ni kutibu maambukizi na kuweka mlinganyo au uwiano sawa wa bakteria wazuri wanaokuwa ukeni. Zipo njia nyingi za asili ambazo zitakusaidia kuondoa hali hiyo na kukufanya kuwa na uwezo mkubwa wa kupata ujauzito.
NUKUU: Napenda kuwashauri wanawake wote wenye tatizo la maambukizi ya fangasi ya muda mrefu au yanayojirudia mara kwa mara kuweza kupata tiba mapema bila kuchelewa. Usipende kuufuga ugonjwa wa maambukizi ya fangasi ukeni kwani utakusababishia matatizo makubwa mno kadiri unavyozidi kuongezeka.
Napenda niishie hapa katika makala yetu leo, tutaonana katika makala zingine zijazo. Nikaribishe kipindi cha maswali kwa yeyote mwenye maswali na maoni.
Je, unahitaji huduma na ushauri? Basi wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752 389 252/0712 181 626.
Pia tuna darasa letu zuri kabisa katika mtandao wa WHATSAP, hivyo unaweza ukatuma namba yako ya WHATSAP ukaunganishwa na darasa ili uweze kupata masomo endelevu ya afya.
Karibuni sana!