Magonjwa ya zinaa huwa ni maambukizi ambayo huenea kwa kufanya ngono na mtu mwenye maambukizi hayo. Unaweza ukapata magonjwa ya zinaa pia kwa mdomo, njia ya haja kubwa au sehemu za siri.
Maambukizi ya magonjwa ya zinaa huwa ni magonjwa mabaya ambayo huhitaji matibabu, haijarishi wewe ni mjamzito au sio mjamzito. Lakini ikiwa kama ni mjamzito, sio wewe tu utakayekuwa katika vihatarishi; magonjwa mengi ya maambukizi ya zinaa hasa yanaweza kuwa yenye kukudhuru wewe pamoja na mwanao tumboni. Baadhi ya magonjwa ya zinaa kama vile Ukimwi, huwa hayatibiki na yanaweza kuwa hatari kabisa katika maisha yako.
NUKUU: Napenda nikujulishe kuwa, muhudumu wako hospitalini atapaswa kupima magonjwa ya zinaa mara ya kwanza unapoenda Kliniki endapo kama utakuwa umefanya mahusiano ya mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Ikiwa kama utaonekana una maambukizi ya magonjwa ya zinaa, basi unapaswa uanze matibabu haraka sana ili kuweza kuulinda mwili wako pamoja na kiumbe kilichomo tumboni mwako.
Je, Kuna Aina Ngapi Za Magonjwa Ya Zinaa?
Kwa kawaida kunaweza kukawa na aina 20 za magonjwa ya zinaa, lakini nitaweza kutaja tu baadhi ya aina za magonjwa hayo yanayowasumbua watu katika jamii, nazo ni kama ifuatavyo:
- Mkanda wa jeshi
- Ukimwi
- Ugwaru(genital warts) ambayo husababishwa na virus vya human papilloma
- Pangusa(Chlamydia?
- Kaswende
- Kisonono
- Malengelenge
- Homa ya ini(Hepatitis B)
Je, Dalili Za Magonjwa Ya Zinaa Zinakuwaje?
Wakati mwingine, kunaweza kusiwepo na dalili za maambukizi ya ugonjwa wa zinaa. Lakini kama dalili zikianza kujitokeza, zinaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Hali ya uvimbe au hali ya wekundu maeneo ya uume au uke
- Harara kwenye ngozi bila kusikia maumivu
- Maumivu makali wakati wa kukojoa
- Uzito wa mwili kupungua
- Kukosa choo
- Kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
- Kichwa kuuma, kuhisi homa au baridi
- Ngozi kuwa ya njano
- Kutokwa na damu ukeni ambayo siyo ya hedhi
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kuhisi hali hali ya muwasho mkali ndani ya uume au uke
- Majipu, vidonda au vigwaru karibu na mdomo, njia ya haja kubwa, uume au uke.
- Kutokwa na uchafu kwenye uume au uke(uchafu unaotoka ukeni unaweza kuwa na harufu mbaya)
Je, Maambukizi Ya Magonjwa Ya Zinaa Yanawezaje Kuathiri Mimba Yako?
Magonjwa ya zinaa kwa ujauzito yanaweza kukudhuru wewe mjamzito pamoja na kiumbe kilichomo tumboni mwako, kulingana na aina ya maambukizi, kwa mfano;
- Ukimwi
Kwanza tumshukuru Mungu kwa kuwapa uweza madaktari wa kisayansi kwa kugundua dawa yenye uwezo mkubwa zaidi katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi visiweze kuhamia kwa mtoto au kiumbe kinachokuwa tumboni mwake
.
NUKUU: Hivyo basi, mama mjamzito mwenye maambukizi ya Ukimwi anaweza akapata tiba ili kuzuia virusi visiweze kuhamia kwa mtoto.
- Kisonono
Ugonjwa wa kisonono huwa ni wa kawaida sana, mara nyingi hupimwa kupitia uchafu au majimaji yanayotoka ukeni. Ikiwa kama maambukizi haya uliyapata wakati wa ujauzito, basi yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu ukeni, kuhisi maumivu makali wakati unapokojoa au tumbo la chini kuuma. Mwanamke mjamzito mwenye ugonjwa wa kisonono ikiwa kama hajatibiwa anaweza kuendelea kuwa na hatari ya kuporomoka kwa mimba au kuzaa kabla ya muda haujawadia.
NUKUU: Mtoto anayezaliwa pindi mama akiwa bado na maambukizi naye pia huwa na maambukizi makali yatakayoendelea sehemu za macho, viunganishi vya mifupa au damu kuchafuka. Mtoto anaweza kuwa na hali ya upofu wa macho kwa baadaye.
Unaweza kuona hapo juu jinsi mtoto anavykuwa na matatizo machoni.
- Vigwarigwaru(Genital Warts)
Huu nao ni ugonjwa wa zinaa wa kawaida. Vigwarugwaru mara nyingi huonekana katika umbo la mboga ya Cauliflower ambavyo vinaweza kuwasha au kuwaka kama moto. Ikiwa mama utapata maambukizi haya wakati wa ujauzito, basi matibabu yanaweza yakasubirishwa kwanza mpaka utakapojifungua. Wakati mwingine homoni kutoka katika ujauzito zinaweza kuvifanya vigwarugwaru kuwa vikubwa zaidi. Ikiwa kama vitakuwa vikubwa zaidi na kuiziba njia ya mtoto kupita, basi mtoto atahitaji kutoka kwa kutumia upasuaji.
- Pangusa
Ugonjwa wa pangusa unaweza kuongeza hatari ya mimba kutoka au kuporomoka au kuzaa kabla ya muda haujawadia. Watoto wachanga wanaozaliwa na mama mwenye maambukizi haya wanaweza kuwa na madhara mabaya katika sehemu za macho na kwenye mapafu.
NUKUU: Hakikisha unarudia kupata vipimo ndani ya miezi mitatu, ili kuwa na uhakika kuwa maambukizi tayari yameshaondoka hata kama mwenzi wako ameshapata matibabu.
- Kaswende
Maambukizi ya ugonjwa wa kaswende mara nyingi hupimwa kwa kutumia damu, ingawa ngozi ya mwenye kaswende inaweza pia ikapimwa. Ugonjwa wa kaswende unaweza ukamfikia kwa urahisi sana mtoto aliyeko tumboni. Ni ugonjwa unaoweza kusababisha madhara mabaya sana kwa mtoto wako. Mara nyingi watoto huwa wanazaliwa kabla miezi haijatimia. Mtoto mwenye maambukizi ya kaswende ikiwa kama hajatibiwa huwa anapatwa na matatizo kwenye ubongo, macho, masikio, moyo, ngozi, meno pamoja na mifupa.
- Malengelenge(Trichomoniasis)
Maambukizi ya ugonjwa wa malengelenge yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu wa njano wenye harufu mbaya au kuhisi maumivu makali wakati wa kufanya tendo la ndoa au wakati wa kukojoa. Ugonjwa huu unaweza ukaongeza hatari ya kuzaa mtoto ambaye hajakamilisha miezi yake tumboni. Ni mara chache sana mtoto hupatwa na maambukizi haya wakati mama anapojifungua na kutokwa na uchafu baada ya kujifungua.
NUKUU: Jitahidi kurudia kupima mara kwa mara ndani ya miezi mitatu ili uweze kutibiwa na uhakikishe unapona kabisa ndani ya miezi hiyo.
Je, Maambukizi Haya Yanatibika Kwa Mjamzito?
James Herbal Clinic tuna dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa maambukiz ya magonjwa ya zinaa kwa mama mjamzito. Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana!