JE, MAUMIVU YA NYONGA HUASHIRIA NINI? JE, NINI VISABABISHI VYAKE?

Maumivu ya nyonga yanaweza kutokea kwa mwanaume na mwanamke pia na yanaweza kutokana na maambukizi, hali isiyo ya kawaida katika viungo vya ndani, au maumivu kutoka kwenye mifupa ya nyonga. Kwa wanawake, maumivu ya nyonga yanaweza kusishwa na mfumo wa uzazi. Matibabu yake yanategemeana na kisababishi chake.

NUKUU: Maumivu ya nyonga yanaweza kuwa ishara kwamba kunaweza kuwa kuna tatizo kati ya viungo vya uzazi ndani ya eneo la nyonga za mwanamke.

Ingawa maumivu ya nyonga mara nyingi hutokana na maumivu katika maeneo ya viungo vya ndani vya uzazi, basi maumivu ya nyonga yanaweza kuwepo wakati wa kufanya tendo la ndoa, na yanaweza kutokana na visababishi vingine. Maumivu ya nyonga yanaweza kuwa dalili ya maambukizi au yanaweza kutokana na maumivu kwenye mifupa ya nyonga au katika viungo vya ndani visivyokuwa vya uzazi. Kwa wanawake hata hivyo, maumivu ya nyonga yanaweza kuwa ishara kabisa kwamba kunaweza kuwa na tatizo ndani katika mojawapo ya viungo vya ndani vya uzazi katika maeneo ya nyonga kama vile mfuko wa uzazi(uterus), vifuko vya mayai(ovaries), mirija ya uzazi(fallopian tubes), pamoja na uke(vagina).

Je, Nini Husababisha Maumivu Ya Nyonga?

Visababishi vya maumivu ya nyonga kwa mwanaume na mwanamke huwa ni pamoja na mambo haya yafuatayo:

 

  • Matatizo ya kibofu cha mkojo
  • Kidole tumbo
  • Magonjwa ya zinaa
  • Maambukizi katika figo au mawe kwenye figo
  • Matatizo ya utumbo
  • Matatizo ya mshipa wa ngiri
  • Mifua ya nyonga iliyovunjika

Visababishi vinavyowezekana vya maumivu vya nyonga kwa wanawake tu ni pamoja na:

  • Ujauzito
  • Mimba kutunga nje ya kizazi
  • Mimba kutoka
  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID
  • Yai kupevuka
  • Maumivu wakati wa hedhi
  • Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
  • Uvimbe katika tumbo la uzazi(uterine fibroid)
  • Endometriosis
  • Saratani ya shingo ya kizazi, nk

 

Je, Ni Dalili Gani Zinazoambatana Na Maumivu Ya Nyonga?

 

Dalili nyingi huambatana  na maumivu ya nyonga. Baadhi ya dalili hizi ni pamoja na:

  • Mumivu ya hedhi
  • Kutokwa na damu ukeni, au matone ya damu au uchafu
  • Maumivu wakati wa kukojoa
  • Kukosa choo au kuharisha
  • Tumbo kuungura au kujaa gesi
  • Kutoa choo chenye damu
  • Kuhisi homa au baridi
  • Maumivu katika eneo la hip
  • Maumivu katika eneo la kiuno

Je, Maumivu Ya Nyonga Yanapimwaje?

Unapopima chanzo cha maumivu ya nyonga, daktari atafuatilia  dalili pamoja na historia ya mgonjwa. Vipimo vya mwili au vipimo vingine lazima pia visaidie chanzo cha maumivu ya nyonga. Kipimo maalumu kilichofanyika kitategemeana na mazungumzo na daktari wako. Baadhi ya vifaa vya vipimo ni pamoja na:

  • Vipimo vya mkojo na damu
  • Vipimo vya ujauzito kwa wanawake wenye umri wa kuzaa
  • X-ray
  • Vipimo vya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na pangusa
  • Vipimo vya uzazi(Hysteroscopy)
  • Kipimo cha choo
  • Ultrasound
  • CT scan

 

Katika makala hii, James Herbal Clinic tunapenda kuishia hapa. Hivyo tunakaribisha maswali kwa wale wote wanaopitia makala hii.

 

Je, unahitaji huduma? Basi unaweza kutupigia kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

James Herbal Clinic pia tunatoa elimu kila siku katika JUKWAA(GROUP) letu, hivyo unahitaji kujiunga na darasa letu, unaweza kutuma namba yako ya WHATSSAP au TELEGRAM.

 

Karibuni sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *